Ubabe wa kuminya Demokrasia ndani ya Chadema

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,373
6,084
Pamoja na kujitangaza kwamba Chadema ni chama kinachofuata siasa ya demokrasia ndani ya chama lakini kwa maoni yangu ni kwamba Chadema sio chama cha kidemokrasia.
Wakati wa kumtafuta mgombea urais wa chama hicho mwaka 2015 tuliona jinsi mgombea urais wa chama cha Chadema kupitia jina la Ukawa ulivyopatikana mpaka ukasababisha mmoja wa waasisi wa chama hicho Dk.Slaa akiamua kuondoka kutoka kwenye chama hicho, huko Musoma Wananchi kwa ujumla walikuwa wameshachoka na siasa za kisanii za Vicent Nyerere na hakuwa chaguo lao. Kamati kuu ya Chadema ikalazimisha yeye awe mgombea ubunge wa jimbo la Musoma mjini matokeo jimbo la Musoma mjini likabebwa na mgombea kutoka chama cha Mapinduzi, ulipofika wakati wa kumpata katibu mkuu wa chama hicho akateuliwa huyo katibu mkuu bila taratibu za kidemokrasia kuchukua mkondo wake.
Tukiangalia jinsi wanavopatikana wabunge wa viti maalum na hapo pia hakuna demokrasia ni viongozi waandamizi wa Chadema kila mmoja anakuja na mtu ambaye amtakaye awe mbunge wa viti maalum, mwisho ni huu uchaguzi uliofanyika Iringa kumtafuta Mwenyekit wa kanda ya Nyasa jina la mgombea Patrick Ole sosopi lilikatwa na Mwenyekiti wa Chama Freeman Mbowe alinukuliwa akisema uamuzi wa kumkataa Sosopi umefikiwa kwa maslahi mapana ya chama.
Leo chama cha CCM chini ya mwenyekiti wake mpya wameameua kukisuka hicho chama upya na kwasasa kiongozi yeyote ndani ya chama hicho harusiwii kuwa na nafasi mbili kwa wakati mmoja na bado mabadiliko makubwa yanendelea kufanyika ndani ya chama hicho.
Kufikia uchaguzi wa mwaka 2020 chama cha Chadema isipoangalia itaingia kwenye uchaguzi ikiwa kama cha kisichokuwa cha demokrasia wakati chama Chama CCM kikiwa ni chama kilichojirekeisha kikamilifu chini ya Mwenyekiti wake Rais Magufuli kwahiyo ushindi wa CCM utakuwa mkubwa sana na tutegemee vyama vya upinzani kupoteza majimbo mengi.
 
Back
Top Bottom