Ubabe wa El-chapo achimba handaki la chini kwa chini mpaka Marekani

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Mbabe wa Mexico kwenye biashara ya madawa ya kulevya ambaye ni mmiliki wa genge hatari la El Chapo Sinaloa Cartel.. Alijenga handaki la chini kwa chini kwenda marekani kwa ajili ya kusafirisha madawa ya kulevya.. Handaki hilo lenye reli yake na lift liligunduliwa kwenye mpaka wa Mexico na Marekani mwaka 2019 August

Handaki hilo lenye urefu wa 4300ft,limejengwa kwa kandarasi ya El Chapo Sinaloa cartel linasemekana kuwa refu kuwahi kutokea linaloenda chini kwa chini mpaka marekani kama njia ya kusafirisha madawa ya kulevya

Handaki hilo lina kina cha 70ft toka usawa wa ardhi na urefu wa ft 6 kwa ndani na upana wa 2 ft.. Limeripotiwa kuwa na mfumo hewa safi, mfumo wa umeme mkubwa na mfumo wa kukausha maji

Kwa mujibu wa gazeti la Mirror handaki hilo lilianzia eneo la viwanda mpakani mwa Mexico mji wa Tijuana na linaishia jirani na mji wa San Diego California Marekani ambapo maingilio yake yamefunikwa na viroba vya mchanga

Kwa mujibu wa gazeti hilo la mirror.. El Chapo alituma vijana wake kwenda Ujerumani kujifunza namna ya kutengeneza mahandani ya namna hiyo

Ujenzi wa handaki hilo umesemwa kipimo cha akili ya binadamu anapotaka kufanya kitu, muda uliotumika na gharama zake pia ni vitu vinavyoacha tafakuri kubwa

Kwa sasa El Chapo wa Sinaloa cartel yuko kifungoni Marekani.... Kifungo cha maisha na hiki ni kifungo cha pili baada ya kile cha 2016 alichotoroka gerezani pia kwa kutumia handaki lenye reli lililochimbwa mpaka usawa wa chumba chake gerezani

Jr
 
.
20200201053308_-4880255_480_302_webp.jpeg
20200201053308_2049467340_320_426_webp.jpeg


Jr
 
Back
Top Bottom