Ubabe: Vyama, Ofisi ya Msajili wa Vyama, Serikali Ukemewe

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,226
35,151
Ofisi ya Msajili wa Vyama na Msajili wana wajibu kwa vyama kama ilivyo kwa vyama, kwao. Hii pia ni kama ilivyo kwa serikali na wote hawa.

Yote hiyo iko kwa mujibu wa sheria wazi na bayana katika katiba.

Migongano inayotokea ni kwa sababu tu ya ukiukwaji katiba, ambapo hayupo aliyejuu ya katiba.

Pasipo kukemewa kwa hali hizi ni pigo kwa utawala wa sheria.

Pasipo na kuzingatiwa kwa sheria na kila mdau katika mukthadha huu, ni pigo kwa utawala wa sheria.

Kutaka kuzalisha mapya yasiyokuwamo kwenye katiba baina wadau (yaani ya serikali, vyama na ofisi ya Msajili) ni pigo kwa utawala wa sheria.

Mambo yasiyo kubalika asilani!

Wakemewe wote wanaotuletea mitafaruku kwa kutokuzingatia sheria kama vilivyo.

Washindwe "vingwendu" wote wanaotaka kufanyia katiba usanii wowote katiba badala ya kuizingatia.

Sheria zipo kwa ajili ya kuheshimiwa. Si zaidi, wala pungufu.
 
Nchi haina utawala wa sheria kila mpuuzi anaweza kuibuka na upuuzi wake hata kama ni kinyume cha katiba ili tu kuhakikisha maccm yanaendelea kuminya haki za Watanzania, vyama vya siasa na pia vyombo vya habari.

Msajili kafanywa kuufyata na chama kimoja.

Maajabu ya Mussa.
 
Halafu baada ya uvunjaji wao wa sheria makusudi, anaibuka Waziri Mkuu kutaka mazungumzo na vyama vya siasa kama vile yeye ndie mahakama ya kutafsiri sheria.

Kama sheria iko wazi vyama vya siasa viko huru kufanya kazi zao, viachwe vifanye, sio kuwazuia kwa maslahi binafsi ya CCM, halafu kiongozi wa CCM anataka awe msuluhishi, hizi ni bangi.
 
Ninakazia: "hizi ni bangi 😁😁."
 
Naunga mkono vyama vya siasa vilivyokataa kukutana na msajili , IGP pamoja Waziri Mkuu , hawa hawana uwezo wa kusuluhisha lolote

Kumbe wangapi basi wanaokumbushiwa kutokuwa na kazi katika utekelezaji wa lolote katika uhuru wao?

Ni mahakamani, CAG, au bungeni? Au ndiyo yale ya ule mhimili uliojichimbia zaidi?

Hivi CCM na kina Majaliwa ni kwa kutuona je haswa? Ni uvumilivu kiasi gani ambao wangetaka tuwe nao?

Hii nchi imechezewa sana.
 
Ofisi ya Msajili wa Vyama na Msajili wana wajibu kwa vyama kama ilivyo kwa vyama, kwao. Hii pia ni kama ilivyo kwa serikali na wote hawa.

Yote hiyo iko kwa mujibu wa sheria wazi na bayana katika katiba.

Migongano inayotokea ni kwa sababu tu ya ukiukwaji katiba, ambapo hayupo aliyejuu ya katiba.

View attachment 1979131

Pasipo kukemewa kwa hali hizi ni pigo kwa utawala wa sheria.

Pasipo na kuzingatiwa kwa sheria na kila mdau katika mukthadha huu, ni pigo kwa utawala wa sheria.

Kutaka kuzalisha mapya yasiyokuwamo kwenye katiba baina wadau (yaani ya serikali, vyama na ofisi ya Msajili) ni pigo kwa utawala wa sheria.

Mambo yasiyo kubalika asilani!

Wakemewe wote wanaotuletea mitafaruku kwa kutokuzingatia sheria kama vilivyo.

Washindwe "vingwendu" wote wanaotaka kufanyia katiba usanii wowote katiba badala ya kuizingatia.

Sheria zipo kwa ajili ya kuheshimiwa. Si zaidi, wala pungufu.
Kama CCM inaweza kumfukuza kazi MSAJILI wa VYAMA ITASHINDWAJE KUMWELEKEZA aiandikie Barua Chadema kuwa isifanye Mikutano
 
Ndo Hawa wamesababisha mpasuko ndani ya taifa, ipo siku Kama sio kesho watahukumiwa KWa matendo yao,

Hii nchi inahitajika total overhaul (katiba mpya). Vinginevyo tunakoelekea haihitaji nabii kujua kuwa kitaumana.

Zambia, Malawi, Kenya, DRC, Afrika Kusini na wa namna hiyo haya hayawezi kutokea.

Ila kwa hizi vyenge hapa: Uganda, Burundi, Rwanda, Zimbabwe.

Compare and Contrast. Kwanini sisi kwani si hao wengine.

Tuna ya wazi ya kujifunza tutake tusitake.
 
Tutalaumiana Sana ila mwisho wa siku Katiba ndo suluhu.lakini ni vyema CCM wakaona aibuuuuu inakuwaje wao wanasimamia uchaguzi kwenye mfumo wa vyama vingi?? Yaani mtendaji,mkurugenzi na wasimamizi wote wa uchaguzi ni makada wa CCM alafu baada ya uchaguzi tunatangaziwa CCM imeshinda kwa kishindo kwani huwa wanashindana na nani??
 
Aibu zaidi ni kuwa wanataka kutuaminisha kinachotendeka kuwa ni haki kama vile sote hatuoni.

Hivi ukiwa mnufaika wa katiba iliyopo, huo ujasiri wako kutuongelea sisi wengine tusiokuwamo unaupata wapi?

Wanatumbukiza kusiko hawa ndugu. Ya vyama waongee wa vyama Majaliwa huku hahusiki.

Ninakazia:

"baada ya uchaguzi tunatangaziwa CCM imeshinda kwa kishindo kwani huwa wanashindana na nani??"
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom