Ubabe hadi Canada? This time you're done

Kama hoja ya mwandishi. Mimi simo sana kwenye siasa, lakini lazima ifike mahali tukubali yako mambo ambayo ni kwa ajili ya national interest. Hata hao mnaowashangiloa huko ulaya kwa wanayotufanyia wana mipaka yao kwenye masuala ya kitaifa. Ni hilo tu mkuu.
 
Mnataka tuwe wazalendo hadi kwenye dhuluma?

Yaani mnalia mkiomba sympathy kwa sababu ya tabia zenu za kutotii utawala wa sheria?

Kumbe tabia haina dawa, mmezoea kuonea Wapinzani na kuwafanyia kila aina ya ubabe, sasa mmelewa na kudhani kila mtu ni wa kuonea tu, safari hii mmekwama kabisa .

Tatizo liko wapi? Kiburi cha kugoma kufuata utawala wa sheria tu? Nyie si mnadaiwa bana? Lipeni deni no way!

Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne zote zilikuwa zikilipa hilo deni kwa awamu, serikali hii ya awamu ya tano ikagoma kulipa na kumtimua Stern Tanzania.

Hii maana yake ni kwamba Stern angekuwa raia wa Tanzania asiye na uwezo wa kukimbilia popote na kujihifadhi angepotea kama Azory Gwanda au Ben Saanane.

Kwa hiyo mmeonewa sana si ndiyo? Yaani hilo deni mmebambikwa tu na watu wenye wivu na maendeleo makubwa ya Tanzania, si ndiyo?

Acheni kulidhalilisha taifa zuri la Tanzania, mbona hata Marekani inadaiwa pamoja na utajiri wake? Nyie ni nani hadi msidaiwe?

Yaani mnaandamana ili kupinga kudaiwa? Kwa sababu mmepanga kudhulumu, mkiitwa shithole mnakuja juu kwa hasira.

South Africa mliweza kucheza sarakasi lakini kwa Canada mmekwama, lipeni deni la watu mtutolee hii fedheha.

Uzalendo sio kudhulumu haki ya mtu.
Kwanza wewe ni mjingaa hunielewi na Wala haujitambui..nadhani utakuwa huna maelewano mazuri na mmeo mama.. chombo gani hapa duniani chenye kutoa Haki ya kisheria..hii nayo hujui..au unadhani mtu anajiamulia tu kwamba halipi Deni...kazi ipo kweli ya kufundisha na sio kuelumisha Hawa manyumbuu..na kazi hii ya kufundisha tutaendelea nayo mpaka mnyooke shwainnnn....yy..eti upinzani..hivi kweli TZ Kuna upinzani au upingaji..wapinzani wa ukweli ni wale walioelewa Nini nchi yetu tunataka, na baada ya kuona yanatekelezwa kwa uzalendo tu wakaamua kujiunga na timu ya Magufuli ili kuunganisha nguvu kwenye mapambano..hao wengine huko no wachumia tumbo tuu..wanatafuta mkate wa watoto..hawana lolote..asilimia 90 ya wananchi wapo nyumba ya jembe ulaya Magufuli,, upooo
 
Ni kuipenda nchi yako kwa dhati ya moyo wako, hivyo kutanguliza mbele maslahi ya taifa kuliko hata maslahi binafsi.

Kama ilivyo katika ngazi ya familia, Baba wa familia akifanya kosa akatiwa ndani, huwezi kufurahia hata kama ni kweli baba yako ni mkosaji.

Hivyo kwenye hili la ndege, japo ni kweli tunadaiwa, lakini Mtanzania Mzalendo wa kweli wa taifa lake hawezi kufurahia, kushangilia, kubeza na kukejeli ndege ya taifa lake inapokamatwa, hili ni janga la kitaifa.
Huu ni uzalendo wa ajabu

P
Mkulima alipwe bwana msije kutufundisha uovu
 
Japo ni kweli tunadaiwa, na siku zote dawa ya deni ni kulipa, lakini kukamatwa au kuzuiliwa kwa ndege yetu ni janga kwa taifa letu. Watanzania tunapaswa kuwa wamoja katika hili, kushirikiana na serikali yetu kwa moral support ndege yetu inasuliwe, lakini kunaonekana kama kuna uzalendo wa ajabu wa watu kufurahia na kuliongelea kiushabiki majanga kwa nchi yako

P
Ushirikiano mzuri kwa serikali yetu usio wa kinafiki, ni kuishauri vizuri serikali yetu. Kutoa ushauri utakaotatua tatizo once and forever.

Kwa mfano, jirani yako ikija kwako kukuomba ushauri. Akakueleza kuwa kuna mtu wa kijiji cha jirani, nilichukua mazao yake, nikashindwa kumlipa, baadaye nilimwomba niwe nalipa taratibu, nikawa nalipa. Ila mwaka huu nikaacha. Sasa mdai wangu ameenda mahakamani, mahakama imeniita mahakamani, sikwenda. Sasa polisi wananitafuta ili wanikamate nifikishwe mahakamani kwa nguvu, unanishauri nini?

Utakuwa mshauri mjinga na mnafiki kama utamwambia, 'rafiki yangu, tafuta wanakijiji kama 50 hivi hapa kijijini, uende nao pale mahakamani, wakati kesi ikiendelea wawe wanapiga kelele kuwa wewe hudaiwi, huyo anayekudai ni jambazi'. Na wewe kwa ujinga ukauchukua huo ushauri na kumwona huyo ndiyo mshauri mzuri na rafiki wa kweli.

Mwingine, akakuambia, 'rafiki, tafuta wazee wenye hekima, wawaketishe pamoja na mdai wako. Kwanza umwombe msamaha mdai wako kisha umwombe urudi kwenye utaratibu wa zamani wa kulipa kidogo kidogo. Na umwombe pia akubaliane nawe kuondoa riba. Akikubali, atayaondoa madai yake mahakamani'. Baada ya hapo ukainuka na kusema, huyu mshauri wa pili ni mjinga, tena beberu anayeshirikiana na mdai wako kwa kigezo kuwa kwa nini anakushauri kulipa deni? Tena ukaendelea kunena kuwa mshauri huyu wa pili ni adui mkubwa wa maendeleo yako, hana uzalendo wa kweli kwa wewe mwanakijiji mwenzake!
 
Ehh Mwenyezi Mungu umtangulie mkulima Stern apate haki yake.🙏🏾
Haki gani mama bana..Haki inapatikana mahakamani na sio huku mitaani..Kama mahakamani anashindwa kupata Haki hiyo anayoidai Basi tunaamini hakuna Haki yoyote hapo... Lingekuwa Deni Halalli lingeandikwa kwenye vitabu vya madeni tangu kipindi Cha baba wa Taifa..Sasa iweje Leo liwe halali na wakati wa Nyerere sio halali..kwanini hawakumalizana mahakamani kipindi hicho...tumegundua na Haina shaka kabisa hii ni biashara ya mabeberu ya kutaka kuturudisha nyuma..they want to shake our economy..and this will never happen under the current leadership..
 
Pascal Mayalla,
Huwa nasikia waswahili wanasema, adui yako muombee njaa, nadhani wanaofurahia ni wale wanaye muombea Rais Magufuli njaa.

Ndege ni zao au zetu? Huwa naona kila zikija wanachama wa ccm ndio hualikwa, nahisi hawa ni zao, sasa wale wanaokosa mualiko nadhani ndio hufurahia.

Haya mambo ya jinsi gani watu wanapokea nadhani yako binafsi sana, hata wanaofurahia au kushangilia mtanange huu hawabadili chochote, the fact kwamba tunadaiwa.

Nadhani wangelipa tu ili kuondokana na fedheha hii.
Unadhani kwanini Kama Deni lipo halikuweza kulipwa katika awamu nne zote zilizopita..tuanzie hapo.kudadavua kabla hatuja shauri Sasa kulipwa kwa Deni hewa Hilo.
 
Mkuu inafika mahala unafiki haulipi.
Mtu wa kawaida atajiiliza yafuatayo;
  • Kuna deni au hakuna deni?
  • Je huko Sauzi ndege iliachiwa on technical grounds ya kesi yenyewe au Mkulima alionekana hatudai?
  • Kuikamata ndege sasa huko Canada si Mkulima alikuwa na grounds ku convice mahakama huko Canada kufanya hiyo?
  • Je, Serikali yetu imesha kaa chini na huyu Mkulima ku settle out of court?
  • Kuna uhakika gani kuwa ndege nyingine haitakamatwa katika mazingira ya kupuuza madeni ambayo korti za nchi nyingine zinaona ni halali?
  • Kuingiza siasa kuwa eti tuwe na uzalendo dhidi ya ubeberu mi naona hapa si mahali pake, watu hawafanyi kazi watarajiwayo kufanya, bla bla aint making it.
Kwa kifupi Pasco, hapo inahitajika akili ya ziada na uzalendo hautairudisha ndege bali strategic business thinking.

Kina Kabudi kujipiga kifua haisaidii sana.
Mkuu Jidu,una akili sana,komenti yako hii imeshiba sana,.huyo Pascal Mayala siku hizi kazeeka,haoni mbele.
Mimi nimekuelewa Sana.
 
Pascal Mayalla,
My brother pascall, we were not happy coz of our plane being detained in south africa, no no no, we were happy coz this awamu ya tano thinks that they are clever than even God himself, if you see a president who kills, orders 37 bullets to be pumped into an opposition mp, orders the military to buy korosho yet korosho is nowhere near things like rockets, sumarines or fighter jets,a president who denies people right to express themselves, what else do you expect from the majority of those who such a dictator president is opressing??? i can tell you pascal my brother for free, lots of us will be more than happy if God sends this person(you know who i am talking abaut) to hell fire where he RIGHTFULLY BELONGS, nice weekend bro
Accounts to God's words,nawe wafaa uende hukohuko...
 
kwa bahati mbaya mno, wapinzani hapa nchini bado hawajatambua majukumu yao kama vyama vya upinzani, sasa ukiwa na watu wa aina hii ambao bado hawajajitambua ni hatari.
Majukumu ya wapinzani hapa Tz ni kuchukua tahadhali wasibambiwe Kesi Mahakamani, wasitekwe au wasimiminiwe risasi na watu wasiojulikana, wasikamatwe na kuswekwa ndani kwa kosa la vikao vya ndani.
 
Mtu mwenye akili na anayeipenda nchi ya Tanzania kutoka moyoni na mpenda haki hawezi kuwa na furaha kipindi hiki. Sijafanya utafiti lakini kwa maono ya kawaida watu wametawaliwa na hofu, hasira na hawana furaha moyoni. Wengi wanajifanya tu kuwa wako sawa kama yule mfalme wa Abunuwasi aliyejifanya kupendeza ndani ya suti hewa na wananchi kumsifu kupendeza huku hawaioni suti. Kisa chote ni hofu ya kuwambiwa wana dhambi.
Watu wanaofia kuitwa wasaliti kwa hiyo wanakiri kisichokuwepo
 
Mnataka tuwe wazalendo hadi kwenye dhuluma?

Yaani mnalia mkiomba sympathy kwa sababu ya tabia zenu za kutotii utawala wa sheria?

Kumbe tabia haina dawa, mmezoea kuonea Wapinzani na kuwafanyia kila aina ya ubabe, sasa mmelewa na kudhani kila mtu ni wa kuonea tu, safari hii mmekwama kabisa .

Tatizo liko wapi? Kiburi cha kugoma kufuata utawala wa sheria tu? Nyie si mnadaiwa bana? Lipeni deni no way!

Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne zote zilikuwa zikilipa hilo deni kwa awamu, serikali hii ya awamu ya tano ikagoma kulipa na kumtimua Stern Tanzania.

Hii maana yake ni kwamba Stern angekuwa raia wa Tanzania asiye na uwezo wa kukimbilia popote na kujihifadhi angepotea kama Azory Gwanda au Ben Saanane.

Kwa hiyo mmeonewa sana si ndiyo? Yaani hilo deni mmebambikwa tu na watu wenye wivu na maendeleo makubwa ya Tanzania, si ndiyo?

Acheni kulidhalilisha taifa zuri la Tanzania, mbona hata Marekani inadaiwa pamoja na utajiri wake? Nyie ni nani hadi msidaiwe?

Yaani mnaandamana ili kupinga kudaiwa? Kwa sababu mmepanga kudhulumu, mkiitwa shithole mnakuja juu kwa hasira.

South Africa mliweza kucheza sarakasi lakini kwa Canada mmekwama, lipeni deni la watu mtutolee hii fedheha.

Uzalendo sio kudhulumu haki ya mtu.
Nieleweshe kidogo mkuu, ndege imekamatwa tena kwasababu ya deni la mkulima au ni deni lingine?
 
Ni kuipenda nchi yako kwa dhati ya moyo wako, hivyo kutanguliza mbele maslahi ya taifa kuliko hata maslahi binafsi.

Kama ilivyo katika ngazi ya familia, Baba wa familia akifanya kosa akatiwa ndani, huwezi kufurahia hata kama ni kweli baba yako ni mkosaji.

Hivyo kwenye hili la ndege, japo ni kweli tunadaiwa, lakini Mtanzania Mzalendo wa kweli wa taifa lake hawezi kufurahia, kushangilia, kubeza na kukejeli ndege ya taifa lake inapokamatwa, hili ni janga la kitaifa.
Huu ni uzalendo wa ajabu

P
Mkuu Paskali! Kama katika ngazi ya familia baba kalewa madaraka ya ubaba, watoto kila siku mnatukanwa na kula kichapo kila siku akitokea mmbabe wa baba yako Huwezi kwenda kujificha Jamiiforums kumfurahia mmbabe wa baba yako?
 
Credit ya wajinga haina mashiko

Ninyi ni taifa la wajinga
Wewe ni mjinga kweli kweli, hata hai mnaowalilia wana mipaka. Yaani mmekuwa wajinga kiasi hiki kwa siasa za kishenzi. Sasa hakuna Tanzania tena bali ni kundi la panya road. Mnawekana jchi kwa mambo ya chumbami, kisa kutofautiana mitazamo?
 
Ehh Mwenyezi Mungu umtangulie mkulima Stern apate haki yake.🙏🏾
Kati ya ujinga unaowaandama wanaoitwa wapinzani ni kuona kama fedha zinazolipwa au majanga yakitokea zinaathiri viongozi wakuu wa awamu ya tano. Enyi wajinga, waathirika wakubwa ni nyie! Na ugumu wa maisha unazidi kuangukia kwenu. Mkulima akilipwa ni fedha amabyo angalau ingenunua dawa ya malaria ya kumtibu ndugu yako au wewe mwenyewe. Unajionea janga mwenyewe? Halafu watu wa aina hii ndiyo wanasema wanataka uchaguzi uwe huru na haki ili waingie madarakani. Mtu mwenye akili finyu kama wewe akipewa madaraka nchi ataipeleka wapi kwa ubinafsi ulivyomjaa? Serikali ina haki zote kuhakikisha wabinafsi kama ninyi mnapotea kwenye uhai wa siasa za nchi.
 
Serikali ya awamu ya 5 walipofungua kesi mahakama kuu hapa kwetu, walipaswa kuomba maoni ya wananchi maana hilo ni deni letu.
Walipofungua shauri la kukwepa kulipa deni, Jaji wa Tanzania alitoa hukumu kwamba lazima tulipe. Kwenye kesi ya Afrika Kusini tuliambiwa tumeshinda kesi na hakuna malipo yaliyotoka, na hadi bungeni tukaziona tambo.
Leo mtu yuleyule, mwenye kesi ilelie tuliyoshinda amekamata tena ndege yetu(na obviously ni kwa hukumu ileile ya Tz)
Hapa kweli tutakuwa kitu kimoja? Gharama ya wanasheria kwenda SA kwa nini hatukulipa sehemu ya deni?
Ifike mahali tuonyeshe dunia kwamba na sisi ni watu wazimaaaa. Otherwise dunia inatushangaaa.
Japo ni kweli tunadaiwa, na siku zote dawa ya deni ni kulipa, lakini kukamatwa au kuzuiliwa kwa ndege yetu ni janga kwa taifa letu. Watanzania tunapaswa kuwa wamoja katika hili, kushirikiana na serikali yetu kwa moral support ndege yetu inasuliwe, lakini kunaonekana kama kuna uzalendo wa ajabu wa watu kufurahia na kuliongelea kiushabiki majanga kwa nchi yako

P
 
Ni lazima watu wajifunze kusema kile kilicho moyoni hata kama hakimpendezi mfalme. Na mfalme ni lazima awe na ujasiri wa kusikiliza kile kinachotoka mioyoni mwa watu na tu si kile anachopenda yeye kusikia. Kwa kuwa binadamu wana mitizamo tofauti watatoa maoni tofauti pia.
Yule mfame wa abunuwasi alituma wasaidizi wake wakaangalie suti aliyokuwa akishona Abunuwasi. Naye abunuwasi alishasema asiyeiona suti ana dhambi. Kwa hiyo wasaidizi wakarudi kumwambia mfalme suti anayoshona abunuwasi ni ya ajabu japo kimsingi hawakuiona. Mfalme naye akaingia mkenge kuvaa suti hewa.
Mfalme atalaumiwa kidogo lakini wasaidizi wake wangepaswa kutupwa jela.
Kwa nini wasaidizi wanaingia huu mtego wa kutompa mfalme taarifa sahihi? Kwani kazi ya washauri ni kumshauri au kimsifia, na je mfalme anataka wasaidizi wa kumsifia au kumshauri?
Wengi nikiwemo mimi pia tunasema hadharani hiki lakini moyoni ni kingine sababu ya hofu.
Kibwa cha kujiuliza ni kwa nini tumeingia kwenye huu mtego.
 
Back
Top Bottom