Ubabaishaji wa tanesco unaua shirika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ubabaishaji wa tanesco unaua shirika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwanaharakati2, Nov 9, 2010.

 1. m

  mwanaharakati2 Member

  #1
  Nov 9, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  TANESCO likiwa moja ya makampuni machache ambayo bado serikali inayamiliki kwa njia moja au nyingine.

  Kampuni hii ilitakiwa ijiendeshe kwa faida sana ukizingatia ime-monopolize hii huduma ya kusambaza umeme kwa muda mrefu. Cha ajabu utakuta sehemu ina wakazi wa kutosha ambao wanahitaji umeme ( tena ktk maeneo rasmi ya mradi wa viwanja vya vilivyopimwa na serikali) umeme haujasambazwa.

  Hii inalikosesha shirika mapato kwani watu hawa wote wanaoishi maeneo haya wangekuwa wanalipia hii huduma. Ukifuatilia kule TANESCO ktk zone husika mara utaambiwa contractor atakuja ku-sambaza tender ilishapita nk, wanatengeneza mazingira ya rushwa.

  Hivi hali hii itakwisha lini ktk hili shirika letu? Hata hapa Dar sehemu ambazo zina wakazi wa kutosha bado kusambaza umeme inakuwa tatizo!

  Kama kazi imewashinda ni bora tulibinafsishe hilo shirika.
   
 2. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  simply: Change the government and tanesco will not be the same:
  Serikali haiwezi kubinafsisha mashirika yote maana watakosa sehem ya kula.haya mashirika yanaendeshwa kwa matakwa ya watu na si maslahi ya shirika.angalia atc ipo wapi sa hivi??upupu mwingi sana serkalini watu wanacheza kiduku afu mkuu anacheka tu!uswahiba unauwa nchi hii
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Tungekuwa na viongozi bora kama waziri wa nishati aliyemakini na mbunifu basi rushwa ingeisha kwa kufanya yafuatayo

  1. Maombi yote ya kuwekewa umeme mkoa wa Dar yanafanyiwa wizarani kwa kuweka mfumo maalum wa watu kulog online na kujaza form maalum online kisha wanapewa code ya maombi yao baada ya kusubmit

  2. Ndani ya wiki mbili anapata barua ya survey kutoka wizarani na kopi yake kupelekwa Tanesco

  3. Baada ya kupata barua ndani ya wiki mbili Tanesco wanatakiwa kuwa wamefanya survey na kumjibu muombaji. Kama Tanesco wamekataa kwa sababu wanazozijua wao muombaji anakata rufaa wizarani na wizara kutoa jibu la mwisho. Mchakato huu wote unafanyika ndani ya siku 60.

  4. Ikiwa Tanesco wamezembea basi wahusika wanawajishwa haraka iwezekanavyo, kwa ama kufutwa kazi au kushushwa vyeo. Lakini utaratibu huu unataka mtu kama Magufuli siyo tu waziri cheo wa kuvizia vikao na padiem za safari.
   
 4. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  umenena vema mkuu,ila kumbuka hata wizara yenyewe si salama sawasawa tu na Tanesco, na watendaji ni hao hao!!
   
Loading...