jimbo la mlimba
New Member
- Oct 29, 2019
- 1
- 0
mh rais amekuwa akizitika taasisi mbalimbali za uma kusogeza huduma zao karibu na wananchi badala ya kukaa mijini,ambapo baadhi ya maeneo yamekuwa mgumu kwa wananchi kuzifikia huduma kutokana umbali mrefu.Halmashauri ya kilombero ni miongoni mwa halmashauri ambayo serikali kupitia kwa waziri wa tamisemi alitoa agizo kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhamisha makao makuu ya halmashauri hiyo na kiipeleka inje ya ifakara,sababu mojawapo ni kuwepo kwa halmashauri hiyo ya wilaya na mamlaka ya mji mdogo wa ifakara sehemu moja,kingine ni jiographia ya eneo husika ambalo hupelekea wananchi wa maeneo ya mbali kwa mfano mlimba,utengule,chita na mngeta kulazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kiofisi.makubaliano ya awali yalifikiwa makao makuu ya wilaya yawe mngeta na kikao cha kwanza cha balaza la madiwani kimafanyika hapo,na maene ya wapi ofisi ziwepo yalishafafikiwa muwafaka,lakini sintofahamu imetokea ghafla na wilaya hiyo keendelea kubaki ifakara,hali ambayo imeleta mkanganyiko mkubwa na sintofahamu kwa wananchi.Rai tunakuomba mh Jaffo kama msaidizi wa rais na waziri mwenye dhamana kuingilia kati swala hili ili dhamira ya ya mh rais wetu iweze kutimia.