Uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi uende sambamba na kuanzisha Mahakama ya Kikristu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi uende sambamba na kuanzisha Mahakama ya Kikristu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Nov 18, 2010.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa kuwa sasa Serikali imeifanya Tanzania nchi yenye Dini kinyume na sheria(Katiba) basi ianzishe pia Mahakama ya Kikristu.Serikali isiwachanganye watanzania kwa kusema Tanzania haina dini huku ikiendekeza udini.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mr Invisible, thread zangu .......
   
 3. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  waislamu wengi waliipigia kura ccm na wakristo wengi chadema, sasa mahakama ya kadhi ni sera ya ccm waliouziwa waislamu hivyo ni haki yao kuipata na wakristo kama nao wanataka mahakama ya kikristo ambayo naamini haipo kiuhalisia basi nao wanahaki kuwa nayo lakini ni kichekesho kwa wakristo kudai hiyo mahakama mara tu waislamu watakapoipata!!!

  hii ni sawa na tabia ya watoto wadogo ambao huoneana wivu ikiwa mmoja kamuomba baba ake amnunulie chupi ya rangi nyeupe na mwingine atataka anunuliwe chupi kama hiyo!!!!
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Kwanza ni lazima iwekwe wazi sababu ya kutaka mahakama ya kadhi ianzishwe? Then hapo tunaweza kuanza kuongea mengine, mahakama ya wakristo inaweza kutengenezwa pia, na hii ya kawaida waachiwe wapagani.

  Ni matusi kusema waislamu waliipigia kura CCM na wakristo waliipigia kura CHADEMA. Kuna waislamu wengi walioipigia kura CHADEMA na wakrito wengi waliipigia kura CCM. Sera ya udini si nzuri.
   
 5. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Katiba yetu inasema nchi yetu haina dini. Siungi mkono kujadili masuala ya kidini kwa mtizamo huo. Suala la mahakama ya kadhi waliongelee waislam wenyewe kwenye misikiti yao siyo humu jf wala mitaani.
   
 6. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2010
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,171
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  biashara ya udini kalasi inatumiwa na mafisadi ili waibe na kuifisadi tanzania na watanzania wachache wasio jitambua wanaupigia debe Biashara iliyopo sasa ni kati ya walio nacho na wasio nacho hii biashara itatugharimu haibagui dini kabila chama au rangi maana wanaotesa na kuteseka ni hao hao huteseki kwa kuwa ni mkristo au mwislamu ima cuf au chadema MAVUVUZELA WA MAFISADI JITAMBUENI maana mchuma janga HULA NA WANAE!
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Islamic law na canon law zote zipo kwenye sheria zetu sasa kwanini kuwepo na mahakama ya kadhi?
   
 8. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  siamini kama ni tusi kusema waislamu wengi waliipigia kura ccm na wakristo waliowengi waliipigia kura chadema ni kiwa nasababu zifuatazo:

  1)ccm ilipata kura nyingi sana maeneo wanamoishi waislamu wengi, mfano; mkoa wa pwani, tanga, dar, zanzibar, tabora, singida, dodoma, mtwara, lindi na ruvuma.
  2)ccm ilizoa kura nyingi za urais baadhi ya maeneo ya mijini wanamoishi waislamu wengi,mfano; kondoa, morogoro,same mjini, mwanga mjini, moshi mjini, arusha mjini, bukoba mjini, iringa mjini, mwanza mjini, kigoma mjini, singida mjini, na dodoma mjini.
  3) chadema walipata kura nyingi sana maeneo wanamoishi wakristo wengi, mfano, kilimanjaro,arusha, mwanza, shinyanga, mara, kagera, iringa, kigoma, rukwa, na maeneo wanamoishi wakristo wengi ktk jiji la dar, mfano; kinondoni na kawe.
  4) chadema walipata kura chache sana ktk maeneo wanamoishi waislamu wengi , mfano; zanzibar, na mikoa yote ya ukanda wa pwani!
  5) kufungwa kwa nyumba za ibada siku ya uchaguzi ni dalili tosha za kuegemea upande wa chadema kwa sababu kipindi cha kampeni kulitolewa kauli nyingi toka kwa viongozi wa makanisa kuwaelekeza waumini wao ni kiongozi gani anaefaa kuchaguliwa!

  sasa sijui ni ushahidi gani mwingine utakaokuridhisha! Na huu uoga sijui watu wengine wanaupata wapi! Yaani ukitaja dini fulani tu, hapo ni kosa!! Unaambiwa wewe ni mdini, au unataka kuleta chuki na vita vya kidini!!! Yaani nashindwa kuelewa!! Tanzania ukitaja vitu viwili ni mwiko!!! Dini na muungano!!!! Na sijui ni nani alieturoga na vitu hivi viwili!!!

  umefika wakati sasa wa kujadili mambo haya kwa uwazi kabisa bila ya uoga na kigugumizi kwa sababu tuna katiba yetu inayolinda dini na watu wake!!
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  hivi Halima James Mdee ni dini gani? Naye ataheshimu mahakama ipi?
  na Mbona (kama nilivyoambiwa) Pinda ameapa bila kushika Kurani, Bible au katiba. (mimi niko porini na sina umeme aliyeona vizuri anirekebishe ikiwa nimekosea)
   
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  sidhani kama wakristo waliipigia kura chadema wakti wakristo hao hao walikuwa wanasema ccm ni chaguo la Mungu. hapo hamueleweki...toka lini shehe alishawai kumsema vizuri candidate yeyote wa kikristo?...
   
 11. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 853
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80
  Matusi acha kijana... Hiyo mahakama ya kadhi muianzishe kama taasisi ndani ya dini yenu wenyewe kwa gharama zenu wenyewe... Thats all... Lakini sio serikali iipitishe kisheria na kikatiba...maana nyie mnachotaka ni eti serikali igharamie kila kitu...

  Serikali yetu ni ya ki-secular mkuu...kamwe haiwezi kuwa serikali ya waislam pekee.
   
 12. B

  Baba mlezi JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2013
  Joined: Apr 22, 2013
  Messages: 238
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Vipi mahakama ya kadhi imeshapatikana au bado CCM iliwalaghai na mkaamini kuwa itaanzishwa,lol wajinga ndo waliwao
   
 13. super nova

  super nova JF-Expert Member

  #13
  Feb 1, 2015
  Joined: Aug 12, 2014
  Messages: 1,218
  Likes Received: 750
  Trophy Points: 280
  And now is endless debate of mental slavery idelologies...people are blind of reality...you hate someone because of what you belive? Nonsense....how much are you sure that the white man or the arab man ideology is true..what was your ideology before slavery..why are you christian or muslim? What if you was vorn to a different family belief? Religions debates sucks...
   
 14. M

  Mbarikiwa Mollel JF-Expert Member

  #14
  Feb 1, 2015
  Joined: Jan 13, 2015
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu akubariki, akupe maisha marefu kama aliyompa nabii musa, miaka 120 huku anaona vizuri kama kijana wa miaka 20! Umefafanua kwa kirefu na kwa upana ambao mtu mwenye ufahamu mzuri ni lazima aelewe ili kuepusha machafuko ktk nchi yetu, hakuna kitu kizuri kama kufanya shughuli zako ukiwa huru, hukohuko tumeozeshana, ni marafiki, bussinespatner, tutaangalianaje!? ulaku wa madaraka usitugawe watanzania, tuwe sawa kwenye madaraka, kuna watu wanashabikia bila kujua madhara yake, hawajifunzi na majirani zetu, mwisho wa ugomvi wa vita vya kidini kitachofuata ni ukanda na ukabila, MUNGU IBARIKI TANZANIA TUBAKIE NA AMANI YETU, AMEN.
   
 15. P

  Penguine JF-Expert Member

  #15
  Feb 1, 2015
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Serikali haina dini. Japo kuwa Wananchi wanazo dini zao. Kuingiza mahakama za dini fulani katika mifumo ya Serikali ni kuifanya Serikali kuwa na dini. Tena dini ya imani ya hiyo mahakama ya mahakama ya dini itakayoanzisha.

  Sasa hoja ni utawazuiaje Mabudhist wakitaka kuanzisha Mahakama za Dini yao? Wakristo kadhalika?

  Waislam ndugu zangu anzisheni Mahakama hizo kwenye mfumo wenu wa Kiislam huko misikitini.

  Kamwe pasitokee Mkristu mwenye kudai uchuro huo wa migawanyiko. Eti Mahakama ya Kijesuit!
   
 16. Ishmael

  Ishmael JF-Expert Member

  #16
  Feb 1, 2015
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 15,061
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Kadhi court is diabolical and inhumane
   
Loading...