Uandishi wa ushahidi wa jaji katika kesi ya tundu lissu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uandishi wa ushahidi wa jaji katika kesi ya tundu lissu.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Mar 29, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  [h=1]Jaji aacha kuandika ushahidi katika kesi ya Tundu Lissu[/h][h=1]Leo siku nzima kulikuwa na majibizano ya kisheria kati ya wakili wa waleta maombi na wajibu maombi, lakini vitu vya muhimu vilivyojitokeza katika kesi hiyo ni haya yafutayo.[/h][h=1]1. Jaji Moses Mzuna anayesikiliza kesi hiyo alionekana kuacha kuandika maswali na majibu yaliyoulizwa na Lissu kuhusu rushwa alizotoa Mgombea wa CCM Jonathan Andrew Njau wakati wa kura za maoni. Shahidi alikuwa ni aliyekuwa katibu wa CCM wa Wilaya ya singida vijijini wakati wa uchaguzi Mkuu wa 2010 Bw. Cosmas Kasangani,. Mojawapo ya vitu vilivyoulizwa na Tundu Lissu kwa msisitizo ni barua alizoandikiwa shahidi na wagombea wawili walioshiriki katika kura za maoni za CCM, Mdimi Emanuel Hongoa, na Miraji Mtaturu. Wagombea hao walimtuhumu Bw. Njau kwa kutoa rushwa wakati wa kura za maoni za ndani ya CCM kwa kumtumia Shabani Itambu Selema, ambaye ndiye mlalamikaji wa kwanza katika shauri hili.[/h][h=1]2. Jaji vile vile alionekana kutoandika ushahidi wa Takwimu za matokeo ya uchaguzi ulioonyesha kwamba , Jonathan Njau hakuwa anaungwa mkono katika maeneo mengi ya Jimbo la singida Mashariki. Kwa mfano: kati ya kata 12, za Jimbo la singida Mashariki Njau wa CCM alishinda kata 4 tu, na Lissu alishinda kata 8. Vile vile katika maeneo 54 ya Uchaguzi, (polling Centres), Njau alishinda maeneo 17, wakati Tundu Lissu alishinda maeneo 37. Na katika vituo 124 vya kupigia kura Njau alishinda vituo 39, wakati Lissu alishinda vituo 84, na kituo kimoja walifungana. Aidha Jaji alionekana kusita kuandika kwamba Njau alishindwa hata nyumbani kwao alipozaliwa.Ushahidi huo unaonyesha Njau alikuwa hakubaliki kwa wapiga kura ndani ya CCM, na Nje ya CCM hata nyumbani kwao. [/h][h=1]3. Jaji hakuandika Njau alipata kura ngapi katika kura za maoni za CCM. Wapiga kura katika kura za maoni za CCM katika Jimbo la singida mashariki walikuwa 7200, yeye akapata kura 3400, idadi ambayo ni chini ya nusu ya wapiga kura walioshiriki Licha yakutumia rushwa kama alivyotuhumiwa na wagombea wenzie wawili ndani ya CCM hakupata hata nusu ya kura za maoni .[/h]
   
 2. Papa D

  Papa D JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe unathibitishaje kuwa Jaji hakuandika? Huenda habari yako ipeleke katika gazeti la Risasi ndiko italeta mantiki!!
   
 3. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mtoa mada alikuwa anasema kuwa kulikuwa na majibizano kuhusu ushahidi wa Lissu kutonukuliwa. Wewe unachotaka kusema ni nini? Unaweza kuuliza maswali ya namna hiyo wakati alichoeleza mtoa mada ni kuwa kulikuwa na majibizano yakuhusu ushahidi na maswali ya Tundu Lissu na hayo yanaashiria kutokuandikwa kwa ushahidi wa Tundu Lissu.

  Mbona unaonekana uko kimagamba zaidi?
   
Loading...