Uandishi wa habari wenye mwendelezo

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,094
3,604
Mimi siyo mtaalamu wa mambo ya habari, lakini nilikuwa nina wazo kwa waandishi wa habari, na watanzania wapenda habari.

Waandishi wa habari jitahidini habari fulani iki-hit nchini, basi muwe mnaifuatilia mwisho wake, hata kama ni baada ya miaka kadhaa!

Kwa mfano, ishu ya kijana shujaa Majaliwa inatakiwa muifuatilie mwaka kesho ili muone kama kijana ameajiriwa au amerudishwa shule kusoma mana ameishia kidato cha pili.

Huo ni mfano tu, ila mnaweza kufuatilia na mambo mengine ambayo yali-hit miaka hiyo ila hatukujua mwisho wake.

Waandishi wa habari mfanye hivyo kwa sababu sisi Watanzania wengine huwa tunasahau sana matukio ndani ya muda mfupi sana!
 
Back
Top Bottom