Uandikishwaji wa wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa serikali za mtaa umekumbwa na Vurugu

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Uandikishwaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mtaa umekumbwa na dosari za vurugu jijini Dar es salaam.
10806281_644866432291001_4536471804126030372_n.png

Uandikishwaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mtaa katika jiji la D ar es salaam umekumbwa na dosari kadhaa zikiwemo vurugu ambazo zimesababisha mahudhurio hafifu ya watu wanao kwenda kujiandikisha.


ITV imetembelea vituo kadhaa kikiwemo cha mtaa wa Mkunduge kilichoko Tandale ambako kulizuka vurugu zilizo sababisha mtendaji wa kituo hicho kusitisha zoezi hilo tofauti na katika vituo vyaa shule za msingi za Shekilango na Buguruni ambazo zoezi hilo linaendelea kwa utulivu ingawa baadhi ya makarani wa melalamika kuhusu maudhurio hafifu.

Katika kituo cha zahanati ya Tandale ambacho vurugu zilizuka katika siku ya kwanza na uandikishaji, zoezi hilo limeendelea kwa utulivu ingawa lili chelewa kuanza baada ya waandikishaji kuhamishiwa nje kutoka chumba walichokuwa wanatumia.

Baadhi ya wananchi walio hojiwa na ITV kuhusu zoezi hilo na uandikishaji wa wapiga kura wameonesha kutokujua kinachoendelea ,hata baada ya kujiandikisha na wengine wamelalamikia hatua ya zoezi hilo kufanyika katika maeneo ya kutolea huduma za afya na shule hali inayosababisha wananchi kukosa huduma ambazo zingepaswa kutolewa katika maeneo hayo.

Chanzo:ITV
 
Nimejiandikisha leo jina nambari 223 huku malamba mawili. Wachakachue jina langu.
 
Uandishi butu huu... Chanzo cha vurugu ni nini?

Ndo waandishi wetu hao kituo 1 kati ya maelfu vilivyoko dar tayari wanaandika utafikiri ishu imekuwa massive alafu tena tukio lenyewe ni la dakika3 tu ..tembeeni wilaya zote3 ndo mje mripoti siyo mnatawaliwa na negativity hivi hata chanzo chenyewe wala hamsemi
 
Back
Top Bottom