Uandikishaji wa kura ya uchaguzi mkuu - Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uandikishaji wa kura ya uchaguzi mkuu - Zanzibar

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bikirembwe, May 26, 2010.

 1. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakati uandikishaji wa wapiga kura nchini umemaliza katika sehemu zote mbili za nchi yetu yaani Bara na visiwani kuna kitu ambacho bado sijapata ufumbuzi wake.Kwa kawaida katika uandikishaji wa kura huku visiwani kuna uandikishaji wa aina mbili; wa kwanza ni wa Rais wa Zanzibar, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani ambao washiriki wao ni wale wenye sifa ya UZANZIBARI MKAZI na wa pili ni ule wa Rais wa Jamhuri ambao huwashirikisha WATANZANIA wanaotoka Bara ambao hawajatimiza ile sifa ya Uzanzibari. Lakini kwa uchaguzi huu sijasikia kama kuna uandikishaji wa aina hii na badala yake wananchi wote wamejiandikisha kupitia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwa ajili ya Rais wa Zanzibar.

  Jee hii ni kwa sababu hakuna tena wahamiaji kutoka Bara huku Zanzibar au ZEC imekuwa ni wakala wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) au CCM wameamua kuwapa haki watanzania wote kushiriki katika uchaguzi wa Zanzibari?

  Mwenye taarifa atudokeze!
   
Loading...