uandikishaji wa kupiga kura - je nifanyeje?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

uandikishaji wa kupiga kura - je nifanyeje??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by msm, Mar 28, 2010.

 1. m

  msm Member

  #1
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  baada ya kukaa ng'ambo kwa mda mrefu nimerudi na kukuta zoezi la kuandikisha kupiga kura na leo ndio siku ya mwisho.
  nimekwenda kituoni kwa nia ya kujiandikisha lakini watu ni wengi sana. mpaka saa 12 jioni watu zaidi ya 300 walikuwa wanasubiri kujiandikisha bila mafanikio yeyote.
  nilipomuuliza muandikishaji akaniambia wanasubiri tamko la serikali lakini leo ndio mwisho
  kituo changu kipo eneo la mbizi beach, je nifanyeje au nani naweza kumcontact ili nipate aki yangu ya msingi??

  kwa nini ni week 1 moja tu kujiandikisha, je wanasia inakuwaje mnakubali hili? ng'ambo unaweza kujiandikisha kwa kutumia post,inperson au internet lakini bado hawatoi week 1. huku sio kuwanyima watu haki yao ya msingi
   
 2. m

  miner Member

  #2
  Mar 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole MSM, Hii ndio nchi yako Tanzania usituletee mambo yenu ya Ughaibuni. Tume yetu ya Uchaguzi ni idara ya Serekali ambayo haitaki kuondoka madarakani siku 7 zinatosha kwani serekali yako haina pesa mwandishi mmoja kituoni anatosha kufanya kazi zote kuandikisha na kupiga picha bila kujali kama utakaa foleni kwa masaa zaidi ya 6 au uiishie zako. Muda kwetu si mali kama mnavyojua nyinyi huko ughaibuni wala kupiga kura si muhimu pia.

  Utatusaidia sana kama ulivyolalamikia haki yako ya msingi ya kupiga kura nenda MAHAKAMANI ndio chombo pekee cha kutoa haki kwa mujibu wa Katiba yetu.na kwa taarifa ya ziada kwako wanakijiji wanatembea km 10 au zaidi kufuata kituo cha kujiandikisha au kupiga kura.Fungua ukarasa utakumbukwa na taifa lako haki si hisani haki hudaiwa kulalamika ni hulka ya kukata tamaa. Fight for your right
   
Loading...