Uandikishaji vitambulisho vya uraia unakwenda mrama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uandikishaji vitambulisho vya uraia unakwenda mrama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 26, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  25 July 2012 | Mwananchi

  ZIPO dalili lukuki hivi sasa zinazoonyesha pasipo shaka kwamba zoezi la kuandikisha wananchi ili wapewe vitambulisho vya uraia halitafanikiwa, labda itokee miujiza. Wahenga waliposema kwamba siku njema huonekana asubuhi walipatia kabisa usemi huo kwani jambo lolote ambalo huanza shaghalabaghala mwisho wake huwa shaghalabaghala. Ni msemo unaofanana na ule usemao kwamba ukipanda bangi lazima utavuna bangi.

  Pengine baadhi ya watu watasema tumevuka mipaka kwa kutoa misemo hiyo ya mitaani kama kielelezo cha hali ilivyo katika zoezi linaloendelea la kuandikisha wananchi kwa lengo la kuwapatia vitambulisho vya uraia kutokana na uzito na unyeti wa zoezi lenyewe kwa usalama na mustakabali wa nchi yetu. Lakini tukiwa sehemu ya jamii ya Watanzania hatuoni aibu na hakika tunao wajibu wa kuonyesha uzalendo kwa kuonyesha mapungufu na kufichua uozo unaoweza kukwamisha zoezi hilo muhimu lenye manufaa kwa taifa na ustawi wa watu wake.

  Kama moja ya habari zilizopamba ukurasa wa kwanza wa gazeti hili leo inavyosema, yapo matatizo makubwa yanayokwamisha zoezi hilo na tatizo kubwa ni kwamba Serikali Kuu haionyeshi dalili zozote za kufahamu nini kinaendelea katika mchakato mzima wa mpango huo. Zoezi hilo nyeti linaonekana kuachwa katika mikono na mamlaka za chini za Serikali za Mitaa ambazo kwa kweli hazina uwezo wala nyenzo za kulifanikisha, huku wananchi wakiachwa njia panda kutokana na mazingira ya mateso na taratibu zenye mkanganyiko.

  Kama hiyo haitoshi, Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA) imeonyesha udhaifu mkubwa kwa kushindwa kufahamu kuwa, ilipaswa kwanza kuendesha programu kubwa ya uhamasishaji kwa kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kupitia vyombo vya habari na kwamba waandikishaji wote walipaswa kupewa mafunzo stahiki ili kuepusha makosa na ubabaishaji tunaoshuhudia hivi sasa.
  Uwezo wa waandikishaji wengi umeonekana kuwa chini ya kiwango na imegundulika kwamba wengi wao hawana elimu ya kutosha, matokeo yake ni kukosea majina ya wananchi wanaokwenda kujiandikisha, jambo ambalo linaonyesha bayana kwamba vitambulisho vingi vya uraia vitakuwa na majina yaliyokosewa. Hivyohivyo, tatizo hilo limekuzwa na idadi kubwa ya wananchi ambao wamegundulika kutojua kusoma wala kuandika na kufanya zoezi hilo kuwa gumu.

  Kutokana na usimamizi usioridhisha wa NIDO, wananchi wameonekana kutokuwa na uelewa wa taarifa gani wanazotakiwa kuwa nazo katika ujazaji wa fomu, kwani baadhi ya waandikishaji wamekuwa wakiwataka walete lundo la vitambulisho, huku katika sehemu nyingine wametakiwa kuonyesha kitambulisho kimoja tu.

  Kasi ndogo ya uandikishaji imesababisha misururu mirefu katika vituo vya uandikishaji kiasi cha watu kushindwa kujiandikisha, huku ukikosekana utaratibu wa kuwahudumia watu wenye ulemavu, mama wajawazito au wenye watoto wadogo. Tumeshuhudia mateso makubwa kwa watu hao kutokana na idadi ndogo ya waandikishaji na mazingira yasiyoridhisha katika vituo vya kujiandikisha.

  NIDA imewaruhusu wajumbe wa mashina ya chama tawala kuwajazia fomu za utambulisho wananchi wanaoishi katika maeneo yao ili waweze kuorodheshwa na serikali za mitaa na hatimaye kupewa vitambulisho vya uraia.

  Lakini baadhi ya wajumbe hao wametumia nafasi hiyo kujitajirisha kwa kutoza Sh2,000 (Dah!) kwa kila fomu na inadaiwa pia kwamba wametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanachama wa chama chao kujiandikisha kwa wingi ili washinde katika chaguzi zijazo.

  Ni vigumu kuelewa kwa nini Serikali Kuu na NIDO hazikuona umuhimu wa kuhakikisha kwamba vifaa kama karatasi, kalamu, huduma za kupiga picha na kurudufya zinapatikana bila malipo kama ilivyokuwa wakati wa kujiandikisha kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2010. Matokeo yake ni wananchi wanaofika kujiandikisha kudaiwa rushwa ya Sh2,000 kwa kisingizio cha Serikali kutoweka vifaa hivyo na huduma nyingine. Ndiyo maana tunasema zoezi hilo limekwenda mrama kwani siyo wananchi wote wataweza kulipa fedha hizo. Tunayo kila sababu ya kulifananisha zoezi hilo na kitendo cha kupanda bangi ambacho mavuno yake hayatakuwa mengine isipokuwa bangi.
   
 2. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii ni weapon of mass destruction
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Zaidi nimeona hao vitambulisho vya taifa wakicheza ngoma na gari kubwa kule mnyamala.lol!
  Madaia yao waTZ hawaendi hadi kwa nyimbo na Ngoma.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Mkuu NATA ni vitu vya kustaajabisha sana. Wanakurupuka katika kila jambo matokeo yake ni kujikanyakanyaga kwa hali ya juu. Wametumia zaidi ya shilingi bilioni 300 lakini angalia zoezi lenyewe jinsi lilivyo shaghala baghala. Halafu wakiitwa DHAIFU wananalama.

   
 5. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ili nalo ni janga lingine kwa serikali yetu,jaman ivi nini hii serikali inaweza na kuwa makini navyo? so inabidi tufunge biashara siku nzima na kuomba day off makazini mana unakaa foleni 6hrs,4hrs KWELI?
   
 6. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  BAK halafu hii umeikazania sana, hawa si dhaifu wanatumia janja ya nyani wote ni walaji kwa kwenda mbele.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Katika hizo bilioni 300 wameshachota nyingi sana. Kama utakumbuka baadhi ya Mawaziri walikuwa wanapigana vikumbo vya hali ya juu kila mmoja akitaka nafasi ya Wizara yake ndio ipewe kazi ya kutafuta kampuni ya nje ya kuingia mkataba wa kutengeneza hivi vitambulisho. Kama hali hii ikiendelea kwa wiki nzima bila ya kuwepo mabadiliko makubwa katika uboreshwaji wa zoezi zima litakuwa limeshindwa vibaya sana.

   
 8. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye blue,nimekumbana na kadhia hiyo siku ya jumatatu
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ni kweli hili nililiona kituo kimoja huko Mwananyamala Mchangani,,,,,,:wacko:
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  foleni ni kero,kwanza ujue kuwa watu wana stress zao,halafu unawawekea foleni,i used 3 hours kukamilisha mchakato,halafu naambiwa kuna siku ntarudi kwa kupiga picha na finger print:alien:
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mimi nina passport ambayo wana information zangu zote including fingerprints, nina driving licence ambayo wamechukua fingerprints na wana photos na all the details sasa ID tena ya nini...ah hizi mbili zinatosha..mi nimewagomea ka ni kunikamata wacha wanikamate
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  hahahahahaaaa,nilikumbana na kadhia ya mwananyamala jumatatu,maeneo ya mchangani
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  jela itajaa na wafungwa wa sensa na vitambulisho
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280
  Ndio matatizo ya kukurupuka Mkuu, halafu cha kusikitisha zaidi mpaka sasa hakuna juhudi zozote zinazofanywa na "Serikali" ili kuboresha zoezi hili.
   
 15. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Bajabiri aisee nachukia foleni za kizembe kama izi vibaya sana,kwaza unapoteza muda wa kutafuta fedha,unapoteza wateja,yani ni kero,sasa umaana wa zile finger prints ktk leseni za udereva vipi?haiwezekani kukonekti matukio basi wawe wanapata izo prints TRA?me nafikiri ntakua ktk zoezi watakaloludia baada ya kuona turn-out ya watu ni ndogo kama ivokua ishu ya benki(ukomo wa zoezi)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Hivi Masha aliweza kupenyeza ile Kampuni yake maana yeye nadhani alionyesha wazi kutaka kujinufaisha na huu mradi.
  Kweli TZ huliwa na wenye meno kunahaja ya kubadili serikali, halafu wote weka keko na segelea au magereza ya mbali kabisa na bongo wakafie uko.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,607
  Likes Received: 82,181
  Trophy Points: 280

  Hata sijui ni nani alishinda sakata lile, Membe naye alikuwa mstari wa mbele katika kupigana vikumbo.
   
 18. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 60

  nakukubalia mdau, huyu mtendaji mkuu wa NIDA ni dhaifu hana mikakati na mbinu na mikakati ya dhati keleta ufanisi.Kwanza zoezi si la kielektroniki, hivyo ufanisi wake unatia hofu, maandali duni,watendaji dhaifu, ufanisi butu.Mi leo siku ya tatu sijajaza fomu , na lini sasa watu watapigwa picha na kupewa vitambulisho
  ?na je watakapokuja kupiga picha watu waliojaza fomu wote watakuwepo?
   
 19. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Serikali ingeweza ku- incorporate Shirika la Posta likafanya kazi hii vizuri sana maana ni hao pia wangehakikisha kuwa kila mtu ana adress kamili ya anaishi wapi. Bila kila mtu kuwa na physical address ni kujichanganya sana katika hiyo data base siku za usoni. Na posta iko kila wilaya hapa nchini, tena inaishi kwa kunyong├│nyea hivyo watumishi wake wangeweza kuisaidia vizuri sana hii NIDA
   
 20. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,149
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni kwamba watanzania walio wengi ambao sasa hivi wanasajiliwa ni wale wasiokuwa na ajira maalum kama vile wafanyakazi wa serikali au taasisi zingine za umma. Watu hawa hawana elimu ya kutosha na hawana ufahamu hata wa majina yao wenyewe. Wengi wamezoea kuitwa baba fulani au mama fulani. Wanapofika kwa karani wa nida na kutaka kutaja majina yao baba zao na mama zao wanaona kama wameulizwa swali gumu sana na la siri kiasi kwamba huchukua muda mwingi kukumbuka majina hayo. Pia wengi hawana vitambulisho halali hata vya kuzaliwa hata kama wamezaliwa miaka ya 90 na 80. Kuandika kwa ufasaha hawawezi wanaandika ule mwandiko wa kuku mchanganyiko wa herufi kubwa na ndogo ambayo huharibu kabisa ile fomu ya kujaza. Nashauri nida watafute kwa maafisa watendaji watu wenye uwezo wa kuandika kwa ufasaha ili waweze kusaidia kumaliza zoezi hili. Wamebana pesa na kuwapa vijana ambao hata majina ya waomba uraia yanawashinda kuandika. Tupo wengi tu wenye moyo wa kujitolea kuhudumia jamii yetu hasa waliosoma social work, sociology na community development kwa sababu tumefundishwa listening and counselling skills hasa unapodeal jamii kama yetu. Mwisho nida mtafute kiwanja kikubwa chenye viti na meza kwa ajili ya kufanya zoezi hili la kusajili raia. Msipofanya hivi mtapoteza raia wengi sana kwa kuwa watu wanachoka foleni ndefu ambazo hazina mwisho. Mnabana pesa na ajira kazi inawashinda. Kila la heri. Tutaona mwisho wake. Hii ni kuorodhesha itakapofika kupiga picha itakuwaje?
   
Loading...