Uandikishaji Daftari la Wapiga Kura Aibu Tupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uandikishaji Daftari la Wapiga Kura Aibu Tupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchili, Mar 30, 2010.

 1. M

  Mchili JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Matatizo yaliyojitokeza katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura Zanzibar, yamejirudia hapa Bara. Tofauti na Zanzibar ambao walikua na vigezo vya kukataa kuandikisha watu kama kutokua na kitambulisho cha mzanzibar mkazi. hapa Bara watu wamekosa haki yao ya kuandikishwa bila sababu wala maelezo.

  Kwa hapa Dar es Salaam ambako wiki iliyopita zoezi la uandikishwaji na uboreshaji katika daftari la wapiga kura lilikua likifanyika, watu wengi walijitokeza tofauti na matarajio ya Tume ya uchaguzi kitu ambacho kilileta usumbufu mkubwa kutokana na uchache wa vitendea kazi vilivyo kua vimeandaliwa. Pamoja na tume hiyo kuliona hilo mapema, haikuchukua hatua zozote kuongeza vitendea kazi au muda wa kutosha kufanikisha zoezi hilo. Sijui kama ni makusudi au ni upofu wa watendaji wa tume.

  Badala ya kuchukua hatua za kuboresha uandikishaji, mkurugenzi wa uchaguzi alitoa very negative remarks, ati watu wanataka tu vitambulisho kwa vile hawana ajira au inawezekana wanajiandikisha mara mbili hivyo akaongeza siku moja tu. Sijui kwa nini afikirie hivyo wakati ni kazi yake kuratibu shuhghuli za uchaguzi.

  Matokeo yake muda umeisha na watu wengi hawakuweza kupata vitambulisho vya kupigia kura. Kilichotia aibu ni makarani waliokua wanaandikisha kubadili zoezi hilo kuwa mradi wao wa kujipatia hela katika dakika za mwisho. Mfano katika kituo cha Wazo Hill, makarani walikua wanachukua rushwa ya sh. 2000 kuweza kumrahisishia mtu uandikishaji na kufanya kazi ile taratibu sana ili kufanikisha azma yao. Mpaka saa ya kufunga zaidi ya watu 50 katika kituo hicho hawakua wamepatiwa vitambulisho na wakaambiwa zoezi limefungwa. Pamoja na kulalamika kwa mtendaji wa mtaa hawakufanikiwa. Tofauti na Wazanzibar, Wabara hawana mwamko wa kulalamikia haki zao kwenye siasa hivyo ni wengi walikua wamekata tamaa na kususa.

  Swali hawa watu watapata wapi haki yao ya kupiga kura? Hii imepangwa makusudi kupunguza wapiga kura Dar au ni uzember tu wa Tume?
   
 2. W

  WildCard JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Watu wa Dar na Tanzania kwa jumla tuna kawaida ya kufuatilia mambo dakika za mwisho kabisa bila kujali umuhimu wa jambo lenyewe. Tuliambiwa tusajili simu zetu tukapewa zaidi ya miezi sita kufanya hivo. Unajua kilichotokea wakati muda ule ulipokaribia kumalizika! Wanachotakiwa kufanya Tume ni kuangalia upya mfumo huu wa uboreshaji kama unatufaa waTz.
   
 3. M

  Mchili JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wakati mwingine ni kutokana na watu kuwa busy sana hata wanasahau mambo ya muhimu. Uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa ni asilimia ndogo sana walipiga kura kutokana na wingi kuchelewa au kupuuzia kujiandikisha.
   
 4. T

  Tata JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Majibu haya yanafanana sana na majibu ya Tume. Mara zote huwa tunatafuta mtu wa kulaumu badala ya kutafuta majibu ya matatizo yanayotukabili.

  Sawa tukubaliane kuwa watu wa Dar wana kawaida ya kujitokeza siku za mwisho wa zoezi. Swali ni kuwa je Tume walijiandaa vipi kuhakikisha kuwa siku za mwisho wangekuwa na vifaa vingi na waandikishaji wa kutosha ili kukabiliana na ongezeko hilo la watu?

  Kumbuka kuwa zoezi limeanza Jumatatu ambayo ni siku ya kazi na limefanyika mpaka jumapili. Tume walipaswa wajue kuwa watu wangeongezeka siku za mwisho wa week kwa sababu ndiyo siku ambapo watu wengi wanakuwa na nafasi.
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana nawe Tata. Tukubali pia tunalo tatizo la kuzingatia na kutumia vizuri muda kwenye masuala yote sio hili tu.Watuharakishie vitambulisho vyetu hili tatizo litakuwa ni historia. Waruhusu pia vitambulisho vingine halali kama passport, vyeti vya ubatizo, kutumika.
   
 6. M

  Mchili JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii inafanya watu wawe na hisia kwamba tume haikua na nia thabiti kuandikisha watu. Kama wamelazimishwa vile!!!

  Nakubaliana na wewe. Kwa mfano kwenye uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa, kulikua na haja gani ya kuandikisha upya wapiga kura wakati tayari watu walikua na vitambulisho vya kupigia kura?
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,563
  Likes Received: 3,859
  Trophy Points: 280
  Hili swala ni barrier kubwa ya demokrasia nchini. Hili daftari linawafanya wengi wasipige kura, na ukweli ndio huo. Aidha wananchi walaumiwe au tume hajalishi, we have problem at hand
   
 8. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Haya yanatuangusha sana ikifika wakati wa kupiga kura. Utakuta vijana wengi wanashabikia upinzani lakini ikifika kupiga kura hawaendi; kumbe wanakuwa hawajajiandikisha. Vijana wanapaswa kuelewa kuwa uchaguzi ni mchakato na hivyo lazima kuwa makini na mchakato mzima. Uchaguzi si kupiga kura tu - hilo ni hitimisho. Kuna kuandishwa, kuna kampeni nk na hatimae kupiga kura.
  Lililotokea dsm, pamoja na kuilaumu tume kwa kutojiandaa kwa siku ya mwisho, bado sisi wananchi tubebe lawama fulani. Kuanzia jumatatu umetanganziwa kujiandikisha lakini huendi, hadi siku ya mwisho! Je ni kweli kuwa watu wa DSM hawana muda hata wa saa 10 - 12 jioni, labda jumapili tu? Hii chelewa chelewa utaiona hata siku ya kupiga kura. Watu, na hasa vijana, wanafika dakika chache kabla ya saa 10; na kwa kweli wengi wao huchelewana hivyo kutopiga kura kabisa. Umefika wakati wa vijana kuamka, acheni kulala - wazee watawachagulia viongozi hadi lini?
  Nina matumaini kidogo: kuna mahali nilisikia eti waliojiandisha wameshafikia milioni 18. Hawa lazima wengi wao ni new voters kwani traditional voters ni kama milioni 4 hivi. Kama hawa wote au kwa wingi wao watajitokeza kupiga kura, basi kinaweza kuanza kueleweka.
  NGUVU YETU SASA TUILEKEZE PIA KUHAKIKISHA WALIOJIANDIKISHA WANAPIGA KURA.
   
 9. M

  MJM JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Dar es salaam isilinganishwe na miji mingine. Unapotoa wiki moja kwa mikoa mingine usitegemee na Dar es salaam iwe hivyo hivyo. Angalia population, miundombinu nk. angalia foleni wakati wa uandikishaji utaona ilihitajika treatment tofauti na mikoa mingine. Hebu niambie simple mathematics unatoka ofisini saa 11 jioni posta na unakaa Mbezi kituo kinafungwa saa 12 jioni mind you hata Jumamosi ni siku ya kazi kwa baadhi yetu, utaweza? Tume inatakiwa kuwa fair kidogo kwa Dar na if possible wangepanga weekend kadhaa kwa shughuli hiyo. Hata hivyo nina wasiwasi na umakini wa Tume wakati wa kuandikisha maana tusije tukawa tunatendeneza kadi za kuuza uchaguzi ukikaribia ili kutumia 40 billions za Sis Em
   
 10. M

  Mchili JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa maana hiyo Dar es Salaam ni kama wamepewa siku moja. Mimi nina wasiwasi kuwa kuna hujuma. Inawezekana wamefanya makusudi kuzuia watu wengi wasije wakapiga kura kwa wapinzani. Kwa sababu haihitaji degree au Phd kuona kuwa ni tatizo.
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe Mkuu.Pande zote ni za kulaumiwa..
   
 12. M

  Major JF-Expert Member

  #12
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 20, 2007
  Messages: 1,425
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  Siwezi kujisumbua kwenda kujiandikisha wakati kura zenyewe zinahesabiwa na kibatari, kikizimika, umeliwa, na hawarudii kubesabu tena, labda utakapofika wakati wa kupiga kielectronic kama kwa Obama maana hiyo ndiyo komesha, watu wanamaliza tu kupiga kura na baada ya dakika tano matokeo yanatangazwa
   
 13. M

  Mbonafingi Senior Member

  #13
  Mar 30, 2010
  Joined: Apr 24, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waugwana swala hili lisionekane dogo, itafika mahali tukamkumbuka shehe Yahya na utabiri wake, hivi tume kazi yake nini? kama ni kuhakikisha kila Mtanzania aliye fika umri wa kupiga kura anapiga kuna kikwazo gani cha kuhakikisha watu wote wanajiandikisha? na kwanini wawafikirie watu kuwa wanatafuta vitambulisho na wala sio kuwa wananchi wameamka na kujua haki yao ya kupiga kura na kuwaondoa viongozi wabovu ambao ndani ya miaaka mitano wameichakaza nchi kuliko hata enzi za ujima kulipokuwa hakuna maendeleo yoyote.Au tume inatumiwa kukandamiza demokrasia kwa manufaa ya chama fulani? Maana inaonekana kuna woga wa aina fulani kwanini leo watu wajitokeze kwa kiwango hicho katika kujiandikisha. Kazi kwenu waTanzania wameamka na kujua haki zao. Subirini wadai haki yao na uchaguzi uairishwe ndipo viongozi wetu watakapo fumbua macho na kujua nguvu za wananchi ziko wapi.:eek:
   
 14. W

  WaMzizima Senior Member

  #14
  Mar 30, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata wangepewa mwezi mzima bado baadhi ya watu wangelalamika eti ooh muda hautoshi au nilikuwa safarini...ukweli ni kuwa watu (sisi watz) ni wazembe especially sisi vijana. Tunataka mabadiliko lakini hatutaki kujishughulisha ili mabadiliko yatokee. Hapa Dar watu wengi kijiweni walikuwa wanasema muda bado na hawa ni vijana wa misheni tauni wala si swala la kwenda kazini week days...ila wote ilipofika Jumapili saa 10 ndio wanaenda kituoni ,what do you expect. Ukweli unabaki palepale watz hatujali muda, hilo ndio tatizo...swala la msingi sasa ni kuhakikisha kuwa watu wengi wanapiga kura na si kubaki home kisha baadae kulalamika viongozi hawafai kama siku zote.
   
 15. F

  Froida JF-Expert Member

  #15
  Mar 30, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama kuna mtu yeyote anauhakika wa kina kuhusu wana Dar kuchelewa kwenda kujiandikisha haya ni majibu ya kijumlajumla ambayo Jaji Makame aliyajibu alipoulizwa na kituo kimoja cha television ukweli wenyewe ni kwamba wana Dar hawajatendewa haki umati wa milioni nne huwezi kulinganisha na wakazi laki nane wa mikoa fulani au milioni mbili,utaratibu mzuri ungewekwa mapema sio kukurupuka tuu,ukosefu wa kamera upungufu wa vitendea kazi na uchache wa waandikishaji vinahusika vipi na watu kwenda vituoni ,ukweli ni kwamba mkakati wa Tume ya Uchaguzi na serikali ya CCM uliwekwa makusudi kupunguza idadi ya wapiga kura wa DSM,basi,na Tume ,wanabahati wana Dar ni toto lala sehemu nyingine wangehakikisha tume inawaandikisha kwa namna yeyote ile ni haki yao ya kikatiba
   
 16. Bernard Rwebangira

  Bernard Rwebangira R I P

  #16
  Mar 30, 2010
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchili, hakika hii ni aibu kwa NEC lakini pia yaweza kuwa si aibu ikiwa walipanga iwe hivyo kwa makusudi, majibu ya Kiravu wakati akiojiwa na Majura yanaonesha kiburi tu ya NEC,

  Wengi wa wakazi wa Dar hawakuweza kujiandikisha si kwa sababu hawakutaka bali mengi yamechangiwa na utendaji wa waandikishaji na ukiangalia karibu kote matatizo yanafanana lakini Kiravu hilo halioni.


  Nitatoa mfano wa Kituo kimoja kule Kimara Temboni, kuna watu walifika siku ya Ijumaa saa saba wakitaraji kuandikishwa na kupanga foleni lakini hawakuweza kwani ilipofika saa 12 kituo kilifungwa, keshoyake walienda saa tatu na kukuta utaratibu wa kupewa namba na kisha kusubiri kuitwa, walipewa namba ktk 250 hivi, lakini mpaka saa 12 ya siku hiyo ni watu pungufu ya 100 ndo waliandikishwa kwa siku nzima, ndipo NEC wakaongeza siku moja, hata hivyo nayo hawakuweza pia kwani spidi ya uandikiswaji ilikuwa ni ile ile.

  Tatizo kubwa spidi ya uandikishaji na vifaa kwa kweli vinakatisha tamaa. Wakazi wengi wa Jiji wamenyimwa haki yao ya msingi ni vyema tume ikafanya namna ya kurejea uandikiswaji DSM.
   
 17. K

  Kinyikani Member

  #17
  Mar 30, 2010
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kuna uchaguzi tanzania ni ujambazi mtupu wa CCM na tume yake ya uchaguzi. hizi ni njama zipepagwa makusudi na NEC wakishirikiana na CCM.
   
 18. M

  Mchili JF-Expert Member

  #18
  Mar 30, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwa hali hii Mkuu kuna haja ya wananchi na vyombo vya habari kishikia bango suala hili ili walioshindwa kujiandikisha wapate haki yao ya kikatiba. Huu ni uvunjaji wa katiba.

  Huyu Mzeee kiravu alikua anajibu kama babu anawagombeza wajukuu zake sijui kama hakujua ni suala nyeti linalompa au kumnyima mwananchi nafasi ya kuchagua viongozi wake.
   
 19. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #19
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Ni mbinu chafu wanayoifanya hawa jamaa purposively
   
 20. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #20
  Mar 30, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,246
  Trophy Points: 280
  Uandikishaji wenyewe uko manual sana, kiasi kwamba unachukua muda mrefu sana. Hayo makaratasi hata accuracy na handling yake ni ngumu sana. Hapo hata ukiwauliza details za tuliojiandikisha zamani sijui kama zaweza kuwa retrieved!! Mie nilijiandikisha 2005, kitambulisho kiliandikwa kwa kalamu ya wino. Leo kimeshafutika, hata hakionekani genuine. Suluhisho ni electronic data base, iwe na details zote za mtu ili kuepuka kughushi. Ngoja tusubiri hizo driving licence mpya.
   
Loading...