Uandaliwe Mdahalo wa Kiingereza kati ya Spika Job Ndugai na Jenerali Ulimwengu kuhusu siasa za ubepari

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Ili kumaliza kelele ni nani anaweza kutoa Maelezo kwa ufasaha kuhusu siasa zetu, Tumetoka wapi na tupo wapi na tunaelekea wapi ni vyema ukawekwa Mdahalo kwa lugha ya Kiingereza live tushuhudie kati ya Jenerali ulimwengu na Mheshimiwa Job Ndugai

Mdahalo huo utamaliza na kuweka wazi ukweli ni nani mwana ccm mwenye hoja kwa lugha ya Kiingereza kati ya Ulimwengu na Ndugai


Mwambieni Spika Ndugai mwana ccm mwezangu atamke kwa kiingereza maneno HAYA"BUNGE HALICHEZEWI, BUNGE LIMEDHARAULIKA "

Napenda kuona watu wakifokeana kwa kiingereza

Kuna wana ccm kelele nyingi lakini wakifika kwenye Kiingereza utasikia

The...... The.......
Mmmmmh....

mmm, Of course


Yes,...


Yes

Wengi ya wana ccm Kiingereza ni shida sana

Hakika tutakukumbuka Benjamin Mkapa kwa Kiingereza safi, Uliweza kufoka kwa Kiingereza, Hawa wa sasa kelele za kiswahili tu ukiwa weka na Beberu toka ulaya hamna kitu
 
Ahaaaa

Bunge zima lile Tundu Lissu na Mbowe ndio waliokuwa wanajua Kiingereza cha kuongea fluent

Kinrara wao alikuwa Dk Mahiga, Dk Mahiga alikuwa ndio nguli wao wa kuongea fluent English

Acha kumfananisha Jenerali Ulimwengu na Spika

Jenerali ni balaa kwa kiingereza

Soma makala zake au Mahojiano yake
 
Ahaaaa

Bunge zima lile Tundu Lissu na Mbowe ndio waliokuwa wanajua Kiingereza cha kuongea fluent

Kinrara wao alikuwa Dk Mahiga, Dk Mahiga alikuwa ndio nguli wao wa kuongea fluent English

Acha kumfananisha Jenerali Ulimwengu na Spika

Jenerali ni balaa kwa kiingereza

Soma makala zake au Mahojiano yake
Kiingereza ni lugha tu, uelewa upo kichwani mwa mtu.
 
Kwa kuwa wote ni watanzania, mdahalo uwe wa kiswahili, kinachoangaliwa ni "point" na sio lugha. Wachina wakibishana kwa kiingereza tunaangalia point na sio lugha.
 
Fikra sahihi huja kwa lugha sahihi. Huu utumwa mnaoukimbatia unawasahaulisha kwamba mko huru.

Tufike pahali tujue lugha ni nyezo tu ya mawasiliano na wala si uwezo wa kuchanganua na kupambanua mambo.

Anyways
Ndugai ana shida zake kama Twaha alivyo na uzandiki na chuki zake dhidi ya utawala
 
Kama lugha tu kwanini inatumika Sekondari Tanzania mpaka Chuo kikuu

Kama lugha tu mbona kila mzazi anampeleka mtoto wake International school au English Medium

Kama lugha tu mbona Interview wanahoji kwa kiingereza

Buyer be aware
Mkuu una matatizo eee?
Asa hayo uliyoyasema yanabadilisha nini kuwa kiingereza ni lugha tu.....
 
Bai bai JF. Ulikuwa msitu wa elimu, jukwaa la wachambuzi, gwiji la tafakuri, kisima cha ujuzi, n.k, n.k.
Ona sasa aina za mada zinazoletwa. JF unaanza kuwa masikini, kipofu na uchi. Kila mtu analofikiria, hata kama ni la kipuuzi anakuja kulisema hapa JF ambaye ulikuwa ni kilele cha maarifa. Buriani JF wa ukweli. Karibu JF kanjanja uliye ghushiwa.
 
Kimsingi Ndugai hana uwezo tena wa midahalo iwe kwa kiingereza, kiswahili ama kigogo. Kuna siku walikuwa kwenye kipindi ITV na Tundu Lissu, siku ile ndio nilijua jazba na udhaifu wa Ndugai. Ile ndio siku rasmi Ndugai alijenga uadui na Tundu Lisu. Alipoingia Magufuli madarakani ndio akazimzidishia Ndugai chuki yake kwa Lisu. Ukimuweka Ndugai na Ulimwengu ni dhahiri Ndugai atapotezwa, ila kutokana na ulevi wa madaraka, tegemea uadui mkubwa utatokea.
 
Huo mdaharo mujenge magril yakutenganisha Ayoub anapojibu hoja.
Itakuwa kama ya Trump na Biden
 
Kama lugha tu kwanini inatumika Sekondari Tanzania mpaka Chuo kikuu

Kama lugha tu mbona kila mzazi anampeleka mtoto wake International school au English Medium

Kama lugha tu mbona Interview wanahoji kwa kiingereza

Buyer be aware

Lugha ni utamaduni, kama utamaduni wako hauendani na lugha yako, basi utaendelea kuwa mtumwa wa usicho kijua. Kiingereza siyo lugha yetu, hivyo siyo utamaduni wetu. Ndiyo maana inaishia madarasani na maofisini, ukitoka nje ya hapo hukikuti kiingereza. Hata wataalam wa mambo ya jamii, wanasema lugha yako lazima iwe sehemu muhimu ya maisha yako. Inakuzunguka pande zote na muda wote. Hata ukilala usiku unaota ndoto kwa lugha yako. Kwa sababu ni sehemu ya maisha yako. Binafsi naota ndoto, aghalabu kwa lugha ya malkia, kwa mambo ya kiufundi au taaluma. Lkn nikija kuota kuhusu mahari, harusi, gulio, mtoni, shambani, ngoma za kienyeji, n.k. naota kwa lugha mama. Hivyo usikione kiingereza kuwa cha pekee sana. Bali ona mila na desturi kuwa ndiyo upekee wetu.
 
Back
Top Bottom