Uanaume ni ubabe au ujasiriamali?

mashishanga

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
611
427
Nije kwenye mada, inawezekanaje mwanamke uliyekua unampenda, unamjali ambaye ulikua unahisi bila yeye maisha yako hayawezi kwenda, anafanya kakosa kidogo badala yakukaa kuongea, basi unaanza kurusha matusi, dharau, makofi na ngumi?

Tena kipigo na hizo dharau unazionyesha mbele ya watoto, wakati mwingine mwanaume anachukua fimbo anaanza mchapa kama mtoto! Niulize, hivi wanaume hufanya hivyo kumlinganisha mkeo na mtoto au ni uonevu kwakuwa mwanamke hawezi kurudisha ngumi? Au kupiga na dharau ndio uanaume unajulikana?

Nimeleta hili maana ninaona threads nyingi watu wanajisifia kupiga wapenzi wao. Mara utasikia "mke bila kupiga hakuna penzi". Ni nini kinasababisha asilimia kubwa ya wanaume kufanya hivi? Hivi ukimwambia mkeo/mwenzio kuwa sipendi hichi hawezi kuelewa? Maana wako wanawake wamepata vipigo kwa wapenzi wao na waume zao hadi wakafa.
 
Lijali...... Pwani yetu!
 
Sio uungwana ila wengine ni nature yao mfano Wakurya wao kupiga ni lazma hata mke wa kikurya asipopigwa anasema hapendwi
 
Kwan mwanaume ukimwambia mwanamke kosa Lake Bila kupiga uanaume wako unaisha?
 
Wallah tunatofautiana binadam

Tupo tukipigwa n mtiti

Tupo Bila kupigwa unaona mapenzi hayanogi

Binafsi naona mnapokua wazi kuekana sawa Kwa maneno Kwa kuongea pamoja ndio solution
 
Kwa sisi wachaga kipigo kidogo kama kakofi kamoja na mkwara ni sehemu ya mapenzi.

Sema sasa kidogo hii imetowekaa, ila umkute mchaga anepiga vyombo lkm mke apate kipondo.

Kwa upande wangu sipendi vijidharau vya hovyo toka kwa mwanamkee.
Ila kaukofi kidogo ukiniletea nyodoo nakuzabaa
 
Mzee mmoja alituhadithia kuwa alikuwa na mkewe wa kwanza mbabe mnoo. Kijiji kizima walimjua. Wao ni kupigana daily. Matokeo yalikuwa hayatabiriki kwani ushindi uliweza kwenda kwa yeyote. Wakaenda mwishoe wakaachana kwa kuwa watu walikuwa wanamsema sana yule mwanaume kuoa mke mbabe. Akaoa mke mshika dini mnyenyekevu na mpole. Lakini kwa huyu mzee alikinai mapema kwani alimuona kapooza. Na bibi nae kumbe alikuwa anamiss ule ubabe wa babu. Mke na mume mpole wakaachwa na wawili hawa kurudiana. Sometimes mazoea yana tabu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom