Uanachama wa CHADEMA kwa njia ya SMS/INTERNET na Kutumia mawakala vijijini


Mpasuajipu

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Messages
838
Likes
7
Points
0
Mpasuajipu

Mpasuajipu

JF-Expert Member
Joined Oct 22, 2010
838 7 0
Kwanza kabisa napendakutoa shukrani za dhati kwa Dr.WP.Slaa kwa ushindi mnono alioupata pamoja na wabunge, na madiwani wote wa CHADEMA licha ya matokeo ya maeneo mengi kuchakachuliwa.
Napenda kutoa mchango wangu wa kuweza kukiimarisha chama kwa kuwa na wanachama hai na sio wazungumzaji tu na hasa kuweza kupata wanachama wengi zaidi maeneo ya vijijini ambako ndio CCM imejikita na huwa inaibukia huko kila miaka ya uachaguzi.

Licha ya kwamba sasa mabadiliko yameanza kujitokeza, bado kuna haja kubwa kuweka "special strategy" za kuzoa wanachama zaidi kwa kuziweka wazi sera za Chama maeneo ya vijijini ambako uelewa bado si mkubwa na bado kuna ushabiki wa CCM kama ilivyo simba na yanga

Napenda bila kuwachosha kupendekeza yafuatayo na wengine mtachangia:

1. Kuanziasha mfumo wa kujiunga na chama kwa njia ya sms tena mitandao yote siyo zain na voda tu ambapo wale watakaojiunga watatoa michango yao direct either kwa M-pesa au kukatwa kiwango kodogo kidogo hadi kutimiza ada ya uanachama kamili. Mwanachama akitimiza masharti yote apewe maelekezo ya kwenda ofisi iliyokaribu naye kuchukua kadi yake tena iwe imechapishwa siyo ya kuandika na mkono kama za CCM. Apeleke picha na iwe scanned km kuna huo uwezekano.

2. Kuuboresha mtandao wa internet wa CHADEMA amabao ni www.chadema.or.tz kuwe na sehemu yafomu za maombi ya uanachama au "application form" za wanachama wapya ambao wanataka kujiunga na kutoa michango yao na kuonyesha idadi ya wanachama hai hadi sasa. Ingawa hii kuonyesha wanachama inaweza kuwapa maadui mwanya wa kujua nguvu ya chadema, basi angalau iwe katika asilimia kwa kila jimbo bila kutaja idadi kwa namba.

3. kuanzishwe matawi vijijini ndani ndani kabisa ambako sumu ya usisiemu imekolea na kuwe na mawakala wa uhakika tena walikula viapo vya kweli na wanaofahamika kuwa ni wazawa wa chadema kweli ili kuepuka kuweka mamluki wa vyama vingine. Mawakala watembelee vijiji na kushajihisha jamii "community sensitization" kwa kuwaelimisha umma sera, katiba na mambo yote yanayohusu chama kwa ujumla. Vijijini baadhi ya watu waliowengi hawajafahamu hadi sasa kuwa kuna vyama imara kama CHADEMA chenye sera safi za kulikomboa taifa hili ktk dimbwi la umaskini. Huko ndio tuanzie kabisa.

Mie nimeanza na haya, nadhani wachambuzi wazuri zaidi wanaweza kusaidia kuongezea au kuweka sawa pale ambapo sijagusia au sikuweka sawa.

Ahsanteni napenda kuwasilisha kwa michango zaidi.

Ndimi DR. Bingwa wa Kupasua Majipu.
:israel:Mwaka 2015 ni CHADEMA TUU
 
Speaker

Speaker

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2010
Messages
6,356
Likes
27
Points
135
Speaker

Speaker

JF-Expert Member
Joined Aug 12, 2010
6,356 27 135
Asante sana mkuu,ila dah maandishi yamebanana balaa
 
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2010
Messages
12,556
Likes
2,368
Points
280
The Son of Man

The Son of Man

JF-Expert Member
Joined Feb 9, 2010
12,556 2,368 280
Poa mwana ila iedit kidogo kwa kuitengenezea paragraphs!
 
NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Messages
1,675
Likes
6
Points
0
NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2010
1,675 6 0
Jambo la msingi ni kwa Chadema kufungua mtandao mpana katika maeneo mbalimbali ambayo wafurukutwa wa mageuzi (tunaoamini yanatokana na mfumo nje ya chama kilichoua mfumo wa utawala wenye kutokujali wananchi) tutaweza kujiunga na kutimiza wajibu wetu katika kuyaleta mabadiliko haya
 

Forum statistics

Threads 1,237,453
Members 475,533
Posts 29,289,121