Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,478
- 30,140
Wiki iliyopita Mwenyekiti wa Chadema, Mheshimiwa Freeman Mbowe, alilitangazia Taifa kuwa wabunge wa Chadema, hawataendelea tena na vikao vya Bunge na wameamua kujiweka karantini kwa siku 14, ili kuangalia afya zao kama wameambukizwa ugonjwa huu wa COVID 19 au laa
Ni uamuzi wa busara kabisa waliochukua wabunge hao na ndiyo unaosisitizwa sana na shirika la afya la dunia (WHO) wa kujali afya yako na ya wengine.
Sasa kituko kimekuja baada ya hao Chadema kutoa tamko hilo, ambapo lilipokelewa kwa vitisho vya hali ya juu kutoka kwa watawala wetu
Alianza Rais Magufuli akiwa kijijini kwake Chato, wakati anamwapisha waziri wa sheria na Katiba, jumapili iliyopita alipotamka hadharani kuwa amemuagiza Spika wa Bunge, awakate posho zao wabunge wote waliosusia vikao hivyo!
Akaja Spika Ndugai mwenyewe, akawaambia wabunge hao warudishe posho hizo za per diem na sitting allowances, kabla hajalikabidhi suala hilo kwa vyombo vya usalama, ili waweze kushughulikiwa kama wahalifu wengine wa jinai!
Akafuatia Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda, ambaye alikwenda mbali zaidi, kwa kutoa amri kwa wabunge wote wa Chadema, waliokuja jijini kwake, warudi Bungeni kwao ndani ya saa 24, ama sivyo atawakamata kama wazururaji, aliowafananisha na machangudoa!
Hapo ndipo ninapojiuliza maswali kadhaa, hivi hawa wabunge wa Chadema, si wamechukua hatua hiyo ya tahadhari ili kuokoa maisha yao na ya wale wanaokaribiana nao, ambalo ndilo jambo linalisisitizwa sana na WHO??
Tukumbuke pia hao wabunge wa Chadema ndicho kilikuwa kilio chao kikubwa sana kwa kumuomba Spika wa Bunge aruhusu wabunge wote wapimwe ugonjwa wa COVID 19 kabla yya kuendelea na vikao hivyo na Spika Ndugai, akawagomea!
Hivi kwa mazingira hayo ya Bunge kupoteza wabunge wake 3 ambao wamefariki katika kipindi kisichozidi wiki 2 hivi kwa uamuzi waliochukua wabunge wa Chadema, bado unaonekana siyo wa busara kweli??
Kwa maoni yangu uamuzi uliochukuliwa na wabunge wa Chadema ni wa busara sana kwa kuokoa maisha yao na ya wale wanaokutana nao kila siku