Uamuzi Wa Spika Makinda Siyo Sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uamuzi Wa Spika Makinda Siyo Sahihi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tatanyengo, Jul 29, 2012.

 1. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Spika Anne Makinda kwa kutumia mamlaka ya Kibunge alisema: 'Nitaivunja kamati ya Nishati na Madini na baadhi ya kamati nyingine ambazo baadhi ya wajumbe wake wanatuhumiwa kupokea rushwa'.

  Je kwa kutamka kwamba 'Nitaivunja' ndiyo tayari alikuwa ameivunja? Na hizo kamati nyingine ambazo zinatuhumiwa alizivunja au la? Kama hazikuvunjwa ni kwa nini wakati nazo zinatuhumiwa kwa kosa linalofanana na lile la kamati ya Nishati na Madini? (Kamati hizo ni ile ya Mashirika ya Umma POAC inayoongozwa na Zitto Kabwe pamoja na ile inayoongoza na Mh. Augustino Mrema).

  Yawezekana uamuzi wa Mh. Spika ulikuwa wa kukurupuka.
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Siasa jumatatu...leo MMU,T&S
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jul 29, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mkuu ingekuwa ni wewe ungefanyaje?
   
 4. N

  NICE LAMECK JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Napita lakini ngoja tuone kesho
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu tatanyengo sijui kama ulifuatilia Bunge au ulipata habari za kuvunjwa hiyo kamati kwa kusoma magazeti tuu.
  Spika alisema hivi "Ninakubali kuivunja Kamati ya Nishati na Madini na zingine ambazo zitatajwa kwenye tuhuma hizo. Nalipeleka pia suala hilo kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, halafu kama ni kutajwa (wabunge hao), basi tutapata mwongozo wa kamati hiyo."
  Makinda ana mapungufu yake lakini katika hili tuseme tu ukweli jamani, amefanya uamuzi wa busara na kishujaa.
   
 6. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Katika mjadala wote sikuona mahali ambapo wajumbe wa poac wakimtetea muhando ukiondoa kabwe, ushahidi ni jinsi kangi lugola ambaye ni mjumbe wa poac alivyochangia, kwa tunaoelewa mafisadi wanataka kujibanza kwenye kimvuli cha kuwa zitto altimeter muhando ili kuihujumu poac ambayo imekuwa mwiba kwa watu Kama Akina mkulo, kwa taarifa za ndani poac haijawahi kukaaa kuijadili tanesco, zitto kakurupuka yupo dar anasema kumtetea muhando hata wenzake hajawashirikisha, abebe Mzigo wake poac iendelee bana.
   
 7. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Yoote yatakayofanyika ni sawa lakini tujiulize wanasiasa wanapokuwa na makosa kama hayo kuondolewa kwenye kamati ndo mwisho? nchi hii utawala wa sheria bado ni mbovu sana na kinachoonekana hapo ni kuendelea kulindana, tujikumbushe mambo mengi yaliyotokea na hao viongozi hakuna hata mmoja aliyewahi kuhukumiwa mfano(Chenge, Mramba, Yona, Ngereja, Malima, Maige na wengineo ambao kwa njia moja au nyingine wamelitia hasara taifa hili lakini wameishia kuondolewa kwenye nafasi zao na kuendelea kutumbua fedha walizoliibia taifa hili, lakini kwa sisi tusio wanasiasa kosa moja linashikiwa bango na kuhukumiwa huku hakimu akisema iwe fundisho kwa wengine, naomba kama wanataka watanzania tuamini kuhusu na uwajibikaji wa kamati ya maadili ya Bunge basi tukianzia mawaziri wote waliondolewa kipindi kilichopita na hawa wabunge wa hizi kamati kama watabainika kuchukua Rushwa au kulisababishia Taifa hasara wapelekwe Mahakamani na sheria ichukue mkondo wake lakini kama si hivyo itakuwa biashara ileile ya kulindana na tutaendelea kuiita hii serikali DHAIFU.
   
 8. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,105
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  zito alikurupuka peke yake. Poac ya kina filikunjombe iendelee na kazi kama kawaida. Tunataka walioomba rushwa watajwe! Inaonekana pia ccm wameegemea kwenye kauli ya zito ili kujificha na kumchafua. Kutoa kauli sio kupokea rushwa japo vyote viwili vinawezekana. Kama zito alipokea rushwa basi atapata stahili yake ila awe makini ccm siyo watu wa kuside nao kama unapigania mabadiliko ya kweli.
   
 9. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Utamsikia akidai kuwa hata vunja kamati nyingine kwa kuwa mjumbe mmoja ana kesi mahakamani!
   
 10. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #10
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mama Gwalihenzi una maneno!

  Kamati karibu zote hazina uadilifu. Zichunguzwe zote. Tatizo sijui nani atazichunguza hizo kamati kwa kuwa Bunge Letu Tukufu limejivua utukufu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #11
  Jul 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mama Gwalihenzi una maneno!

  Kamati karibu zote hazina uadilifu. Zichunguzwe zote. Tatizo sijui nani atazichunguza hizo kamati kwa kuwa Bunge Letu Tukufu limejivua utukufu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...