mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,767
- 7,115
Wana jf
Mwanzoni watu walilalama sana uamuzi wa serikali kuuza nyumba zake, hii imeleta matokeo chanya na faida nyingi.
Kwanza imewaondolea watumishi wa umma hadha ya kufukuzwa katika nyumba hizo kwani walikuwa wanajisahau sana kwa kupewa kila kitu bure. Sasa hivi kila mtumishi wa umma anaogopa aibu akipata vipesa vyake ukimbilia kujenga na kufanya maendeleo mengine. Oysterbay na maeneo mengine ambaya ni makubwa tulishuhudia watu wakiyafanya makazi haya kuwa ya mifugo ili kuongeza kipato.
Mandhari ya majumba yanayojengwa kwa sasa katika mji Wa kibiashara Dar, Oysterbay na masaki na msasani yemechomoza majengo mazuri muno yamepambika sana kiasi cha kuwa kivutio.
Uuzwaji Wa nyumba hizi umeondoa ule ubabe Wa vijana ambao walikuwa wakijimwambafai kuwa wamezaliwa kwenye maeneo hayo ya heshima sasa hivi ukiwa na fedha unanunua apartments au unapanga.
Vizazi vilizaliwa maeneo haya vilikuwa vizazi vya ubwanyenye ndio walikuwa na tabia za kifisadi kutokana kwamba katika serikali za awamu ya kwanza mpaka ya tatu watu wakiingia kwenye nyumba wanakaa hata miaka 50 utadhani ya kwao.
Serikali imefaidika kuziuza mapema kwani ilipoamua kuamia Dodoma hata majengo yangebaki magofu kwani ni ya zamani na yalikuwa yamechakaa sana hivyo ingekuwa vigumu kupata wapangaji.
Mwisho Watanzania tuache lawama kuwa serikali inatumia Pesa nyingi kuwakodishia watumishi Wa umma majengo badala yake wale waajiriwa waweke bidii nao kuwa na sehemu zao. Hata hivyo watumishi hawa imeowaondolea kujitenga sana na jamii hivyo maendeleo tunayafanya kwa pamoja