Uamuzi wa Raisi Juu ya Mgomo wa Madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uamuzi wa Raisi Juu ya Mgomo wa Madaktari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kingengame, Jul 2, 2012.

 1. K

  Kingengame Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ni uwamuzi wa Busara, uliojaa upendo, huruma na msamaha kwa vijana wake Madaktari. Rahisi ametanguliza maslahi ya sisi tulio wengi kuliko kundi moja tu la watumishi. Hotuba ya Raisi imewahabarisha watanzania juu ya sakata hili kwa ujumla wake. Watanzania tumeyaelewa mahitaji ya msingi ya madaktari wetu na wala hatuyapuuzi, tumeuona uwezo na dhamira ya Serikali kuya-address hata kama kwa awamu. Sasa wito wangu kwa Madaktari ni kwamba muitumie nafasi hii kurudi kazini tupunguze vifo visivyo vya lazima wakati serikali ikilishughulikia suala la mafao ya wafanyakazi kwa ujumla wake. Mrejeshe mahusiano yenu mazuri yale ya awali kati yenu na wagonjwa/ wananchi. Madaktari na baadhi ya wananchi msiendelee kudanganywa na wanaharakati/ Wanasiasa hapa Dar es Salaam. Wananchi walio wengi nchini hususan wale waliopoteza ndugu zao kwa kukosa matibabu, wana hasira na watumishi wa sekta ya afya. Wanaharakati hawakufanikiwa kuwashawishi watu wote kuwa serikali ndio iliowauwa. Mgonjwa akija hospitali anamuona Daktari na sio kiongozi wa serilkali. Wananchi wanajua sasa dhamira na mchango wa serikali yao katika kuboresha hali ya huduma zetu za tiba; na mifano wanayo. Waliziona picha za Dr. Ulimboka akiwa ICU, wapo wanaosema miaka 10 iliyopita ICU haikuwa vile. Sasa hivi wananchi wanaeweza kuandamana dhidi yenu mkiendelea kuwa na shingo ngumu. Nawaomba msiwaamshe wananchi waliolala wasije wakafanya tathmini yao na kuwasha hasira ya uma dhidi yenu. Halafu msiwadanganye watanzania kuwa nyie mnataka zaidi kuboreshwa kwa mazingira ya kazi kuliko mishara yenu. Wananchi sikuhizi wanaelewa sana. Na huwezi kirahisi tu kuwa-blind kwa kelele za wanaharakati au wanasiasa. Hata hivyo: Mheshimiwa Raisi amewarahisishia wale ambao hawako tayari, waacha wenyewe, hivyo basi hatutegemei tena kuona huduma zikisimama. Ndugu zetu madaktari; sisi wananchi tunawependa mno, ninyi ndi mawakili wetu kwa mwenyezi Mungu, mnatutetea kila tunapokata rufaa ya kifo kwa kututibu. Maana baadhi ya magonjwa bila tiba ya haraka mtu hufa. Mnapotutibu ndio mnatuktatia rufaa tusife. Tusaidieni. Na ndi maana serikali inaendelea kusomesha madaktari bure ili tuwe nao wengi watuponye. Na kwa Serikali; tafadhali tunawaomba muyatekeleze yale mliokiri kuwa mnayamudu kwa haraka zaidi. Tuendelee kuwa nchi ya kipekee hapa Afrika na Duniani kwa busara na kujaliana kwetu kwa kutumia kwa haki rasilimali zetu kwa faida ya wote.

  Kila la kheri Madaktari.
   
 2. K

  Kingengame Member

  #2

  Last edited by Kingengame; Today at 09:57. Reason: Indicating /adding government responsibility ​
   
 3. A

  Anold JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Huo ndiyo ukweli!
   
Loading...