benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,032
Kwa muda mrefu baada ya kusomwa kwa ripoti za CAG miaka ya nyuma huwa wabadhirifu na wale wote waliotajwa hujificha kwenye kivuli cha uwajibikaji wa kisiasa. "Yaani mhusika anatumbuliwa na mara nyingi inakuwa imeishia hapo na pengine baada ya miaka michache anarejea tena kwenye mfumo."
Maagizo ya Rais Samia kwamba Katibu Mkuu Kiongozi ahakikishe Makatibu Wakuu na Watendaji Wakuu wote wa Taasisi za Serikali wanaipitia kwa kina tarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kujibu na kuzifanyia kazi kwa haraka hoja zote zinazogusa maeneo yao ni maagizo sahihi kabisa
LAKINI KUBWA NA LA KUPONGEZWA ZAIDI NI MAELEKEZO KWAMBA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUHUSIKA NA UBADHIRIFU NA UZEMBE WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA.
HILI LINATUONDOA KATIKA UWAJIBIKAJI WA KISIASA USIO NA TIJA SANA NA KUTUPELEKA KATIKA UWAJIBISHWAJI SAHIHI.