Uamuzi wa Rais Magufuli kuhamia Dodoma kwa wakati huu ni sahihi, aungwe mkono

matunge

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
442
426
Natumaini hamjambo ndungu zangu,

Nami napenda kutoa maoni yangu kuhusu uamuzi wa Mhe. Magufuli kuihamishia Dodoma Serikali yote kabla ya kumaliza awamu yake (sehemu ya kwanza) ya uongozi ifikapo 2020.

Uamuzi huu ni muhimu sana kwa sasa kwa sababu zifuatazo;

1. Wazo la kuhamia Dodoma lililoasisiwa na Mwl. Nyerere limekuwa ni la muda mrefu sana hivyo ni wakati muafaka sasa kwa serikali kulitekeleza.

2. Serikali kuendelea kuwa Dar es Salaam kumedhoofisha kama si kuua kabisa utekelezaji wa maamuzi ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.

3. Dodoma bado ni mji mdogo hali inayotoa fursa kwa serikali kuupanga vizuri kwa kufuata master plan bila kutumia gharama kubwa ikiwamo fidia kwa wananchi.

4. Kuendelea kukaa Dar es Salaam kunavuta kundi kubwa la watanzania kukimbilia katika jiji hilo hali inayolifanya kuwa na idadi kubwa ya watu hali inayosababisha kuwa na ujenzi holela na hivyo kulifanya kuonekana kama KIJIJI KIKUBWA KULIKO VYOTE DUNIANI.

5. Tunahitaji kuendeleza miji mingine ili kutoa uwiano wa maendeleo kwa manufaa ya watanzania wote.

6. Hatuhitaji kujiandaa ili kuhamia Dodoma; mahitaji yote ya kimsingi ikiwamo miundo mbinu itaendelea kujengwa kwa umakini na ubora zaidi ikiwa MZEE WA KAYA AKIWA NDANI YA DODOMA MUDA WOTE.

7. Dodoma ina hali ya hewa nzuri na nyepesi hivyo kuvutia wageni wengi. Dodoma inafanana na Gaborone. Wageni wengi hupata shida wawapo Dar es Salaam kutokana na unyevunyevu na mgandamizo wa hewa. WAWEZA SEMA UKO KWENYE STEAM BATHING. HAKUVUTII KABISA.

8. Nchi yetu itafanana na Kenya (Dar es Salaam = Mombasa; Dodoma = Nairobi); mawasiliano ya miji hii yatakuwa; watu wataweza kufanya biashara kwa kasi zaidi.

9. Kufuatia ujenzi wa standard gauge unaotarajiwa kuanza hivi karibuni hali ya usafiri kati ya miji hii miwili utakuwa mara 1000 na hivyo kuchochea maendeleo.

MIMI MATUNGE NIMEPATWA NA FURAHA KUU; NAMPENDA RAIS WETU KUTOKANA NA MAMBO ANAYOYAFANYA
WITO KWA SERIKALI

  • Tuache kuukarabati uwanja wa ndege wa Dodoma badala yake ujengwe uwanja mkubwa wa kimataifa mfano wa OR Tambo wa Afrika ya Kusini umbali wa kama km 30 kutoka katikati ya Dodoma.
  • Kujengwe station kubwa ya treni Dodoma itakayounganisha bara na pwani.
  • Mifuko ya hifadhi ya jamii ijenge majengo ya kisasa ya ofisi za wizara zetu zote katika eneo moja kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma muhimu.
  • Mradi wa maji ya ziwa victoria ulifikie jiji la Dodoma; maji ya ziwa ni baridi yasiyo na chumvi hali itakayovutia watu kuishi Dodoma.
Nawasilisha
 
Si shida na ni mawazo mazuri.shida ni sentensi ya kuhamamisha makao makuu ndani ya miezi miwili ijayo.Mukulu alisema mpaka ifikapo 2020 na alikuwa na mahesabu yake.Sasa mtu wa chini yake anasema huko mbali siku 60 tu zinahamisha nchi.Uliyetoa mada hujaongelea mashule,hospitali,zahanati,masoko na huduma nyingine nyingi tu ukiachilia miundombinu kama barabara,capacity ya umemeiliyopo na ongezeko la demand n.k

Nakubaliana na Mh Rais kwa kauli yake ya kuhamia rasmi ifikapo 2020 lkn lakini hawa wanaotaka kuhama ndani ya wiki,mwezi sidhani kama inawezekana
 
Natumaini hamjambo ndungu zangu,

Nami napenda kutoa maoni yangu kuhusu uamuzi wa Mhe. Magufuli kuihamishia Dodoma Serikali yote kabla ya kumaliza awamu yake (sehemu ya kwanza) ya uongozi ifikapo 2020.

Uamuzi huu ni muhimu sana kwa sasa kwa sababu zifuatazo;

1. Wazo la kuhamia Dodoma lililoasisiwa na Mwl. Nyerere limekuwa ni la muda mrefu sana hivyo ni wakati muafaka sasa kwa serikali kulitekeleza.

2. Serikali kuendelea kuwa Dar es Salaam kumedhoofisha kama si kuua kabisa utekelezaji wa maamuzi ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.

3. Dodoma bado ni mji mdogo hali inayotoa fursa kwa serikali kuupanga vizuri kwa kufuata master plan bila kutumia gharama kubwa ikiwamo fidia kwa wananchi.

4. Kuendelea kukaa Dar es Salaam kunavuta kundi kubwa la watanzania kukimbilia katika jiji hilo hali inayolifanya kuwa na idadi kubwa ya watu hali inayosababisha kuwa na ujenzi holela na hivyo kulifanya kuonekana kama KIJIJI KIKUBWA KULIKO VYOTE DUNIANI.

5. Tunahitaji kuendeleza miji mingine ili kutoa uwiano wa maendeleo kwa manufaa ya watanzania wote.

6. Hatuhitaji kujiandaa ili kuhamia Dodoma; mahitaji yote ya kimsingi ikiwamo miundo mbinu itaendelea kujengwa kwa umakini na ubora zaidi ikiwa MZEE WA KAYA AKIWA NDANI YA DODOMA MUDA WOTE.

7. Dodoma ina hali ya hewa nzuri na nyepesi hivyo kuvutia wageni wengi. Dodoma inafanana na Gaborone. Wageni wengi hupata shida wawapo Dar es Salaam kutokana na unyevunyevu na mgandamizo wa hewa. WAWEZA SEMA UKO KWENYE STEAM BATHING. HAKUVUTII KABISA.

8. Nchi yetu itafanana na Kenya (Dar es Salaam = Mombasa; Dodoma = Nairobi); mawasiliano ya miji hii yatakuwa; watu wataweza kufanya biashara kwa kasi zaidi.

9. Kufuatia ujenzi wa standard gauge unaotarajiwa kuanza hivi karibuni hali ya usafiri kati ya miji hii miwili utakuwa mara 1000 na hivyo kuchochea maendeleo.

MIMI MATUNGE NIMEPATWA NA FURAHA KUU; NAMPENDA RAIS WETU KUTOKANA NA MAMBO ANAYOYAFANYA
WITO KWA SERIKALI

  • Tuache kuukarabati uwanja wa ndege wa Dodoma badala yake ujengwe uwanja mkubwa wa kimataifa mfano wa OR Tambo wa Afrika ya Kusini umbali wa kama km 30 kutoka katikati ya Dodoma.
  • Kujengwe station kubwa ya treni Dodoma itakayounganisha bara na pwani.
  • Mifuko ya hifadhi ya jamii ijenge majengo ya kisasa ya ofisi za wizara zetu zote katika eneo moja kuondoa usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma muhimu.
  • Mradi wa maji ya ziwa victoria ulifikie jiji la Dodoma; maji ya ziwa ni baridi yasiyo na chumvi hali itakayovutia watu kuishi Dodoma.
Nawasilisha
Una mawazo mazuri ila umeya-dilute kidogo na point namba nane hivi Kakenya ndo kanchi ka kukafanya kama benchmark?? ndiyo maana hawa jirani zetu wanatucheka sana. Pia itakua ni kosa sana kuziweka ofisi za serikali eneo moja kwasababu tutarudia makosa yaleyale yaliyopo Dar, suala la watu wote asubuhi kuelekea eneo moja na jioni kurudi majumbani tukitokea eneo moja ndo chanzo kikubwa cha adha ya foleni jijini. Dodoma itakaa vizuri iwapo Mawizara yatatawanyika
 
Back
Top Bottom