Uamuzi wa kusajili simu uligeuzwa kuwa kisiasa na sasa tunaona ubaya wake

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,635
2,000
Watanzania wanafanywa wajinga sana kwenye maswala ya mitandao kuna mambo mawili ambayo watu wengi hawakuyajua

1. Juzi wakati Raisi anafungua kiwanda cha polisi IGP alisema Polisi hawana teknologia ya kutosha. Rais Samia akasema sasa tulivyo andikisha simu kwa vidole ilikuwa na maana gani? swali la msingi
2. Tumeambiwa Taneso mtandao upo chini.

Hivi vyote ni kitu kimoja na nitawaeleza kwa ufupi

1. Kwanza inaelekea mtandao wa Taneso unaosemekana umearibiwa ni kwamba umearibiwa na majambazi wa mitandaoni. Hawa majambazi wanaweza kufanya mawili. Kwanza wanatafuta mbinu za kuingia kweye mitandao yako wakishaingia wanabadilisha password hivyo hakuna mtu anaweza kuingia kwenye mtandao wa hiyo software. kwa ufupi wanateka mtambo halafu wanaweza kuomba pesa au kuaribu mtandao mzima na kubadilisha. Sasa niya yao kubwa ni pesa inawezekana watu binafsi wakawapa pesa ili waaribu mtandao kwa faida zao au wanaingia kwenye mtandao ndiyo waombe pesa kwa kampuni. Mfano wiki iliyopita hapa US hawa jamaa ambao wengi wanaishi Urusi wakichukua system ya ushambazaji wa mafuta na walilipwa mamilioni na kulitokea upungufu mkubwa wa mafuta maana waliuzuia. Hivyo tusije tukashangaa Taneso kwa siri yawezekana wametoa chochote au wanufuja ili mitambo kuwa chini kama wale wala rushwa ndiyo wamewalipa hawa jamaa kufanya kazi. Lakini si kweli kwamba system imeenda kuaribika maana hizi system zinatumiaka dunia nzima sio Tanzania tu!

2. Swala la pili wakati wananchi wanaandikisha kwa vidole nia ya serikali ilikuwa kisiasa zaidi ili wajue watu wanaowasema badala ya kusaidia nchi ! Hakuna sababu yeyote ya kuweka vidole na kuandikisha kama polisi hawana mtambo na ufundi wa kushika wahalifu. Na kwasababu Polisi wanasema hawana ujuzi ina maana usala wa taifa kwa kushirikiana na kampuni za simu walikuwa wamejikita zaidi kurekodi majungu ya maneno ya mitandaoni kumlinda Magu kuliko kusaidia nchi kwenye ujambazi kama huu wa Tanesco. Tatizo ni kwamba hawa ambao wanaitwa wezi wa mitandao sio wezi wadogo ni majambazi wa kimataifa ambao wengi hawakai Tanzania. Lakini kwasababu polisi hawajui chochote na wanajali zaidi majungu na vijimaneno tusishangae matatizo kama ya Tanesco yakaja tena na malipo yakawa ya siri. Ma bank yetu na mashirika makubwa yawe makini sana.

Serikali iangalie zaidi uizi wa mitandao badala ya uhuru wa watu kijieleza na demokrasia. Sisi kama nchi tutapoteza pesa nyingi kama tutatumia usalama na wataalamu ambao wana gharama kubwa kufatilia vijimaneno vya mitandaoni wakati kampuni zetu system zao zinatekwa waziwazi
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
Watanzania wanafanywa wajinga sana kwenye maswala ya mitandao kuna mambo mawili ambayo watu wengi hawakuyajua

1. Juzi wakati Raisi anafungua kiwanda cha polisi IGP alisema Polisi hawana teknologia ya kutosha. Rais Samia akasema sasa tulivyo andikisha simu kwa vidole ilikuwa na maana gani? swali la msingi...
Mbona hili tulilijua mapema sana. Kisa walitaka kujua Simu za Mbowe na Lissu basi. Yaani tanzania tuliingizwa mkenge kwa sababu magufuli alitaka kujua Mbowe na Lissu wanawasiliana na nani kitu gani na wapi.
 
Motoekoppela te

Senior Member
Oct 13, 2014
149
250
Membe aliwahi kuwatahadharisha kuwa siku "wajanja wa duniani" wakijua Tanzania Kuna soko la udukuzi TUTAKWISHA....

"Wajanja" walianza kumdukua mzee baba akiwa anaongea na daktari wake wa Sauzi akimwelezea maswala ya betri,"wajanja" hawakukawia kumchania mkeka wa mitano Tena maamaeeee....
 
T2020cdm

Member
Oct 17, 2020
68
150
Nitakufa na ukweli wangu ,wewe unamtetea kivipi niambie samia alikuwa na cheo gani
Sawa kabisa labda nikuulize swali, Kama unajua Sheria za jeshi kwann wanajeshi ambao hawana vyeo hufuata amri za wakubwa wao. Hata yeye alikuwa chini ya mkubwa wake ulitaka afanyeje. Nampongeza Sana kwa hatua anazochukua kwa vitendo kupinga yale yaliyokuwa yanafanywa na mwendazake.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
Watanzania wanafanywa wajinga sana kwenye maswala ya mitandao kuna mambo mawili ambayo watu wengi hawakuyajua

1. Juzi wakati Raisi anafungua kiwanda cha polisi IGP alisema Polisi hawana teknologia ya kutosha. Rais Samia akasema sasa tulivyo andikisha simu kwa vidole ilikuwa na maana gani? swali la msingi...
Je, huenda hayo majambazi ni masalia ya mwenda zake yaliyopewa tenda za siri kufanya installations ya systems wakati wa uhai wake?
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
Membe aliwahi kuwatahadharisha kuwa siku "wajanja wa duniani" wakijua Tanzania Kuna soko la udukuzi TUTAKWISHA....

"Wajanja" walianza kumdukua mzee baba akiwa anaongea na daktari wake wa Sauzi akimwelezea maswala ya betri,"wajanja" hawakukawia kumchania mkeka wa mitano Tena maamaeeee....
😅😅😅hao wajanja tuwape tuzo.
 
Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
Watanzania wanafanywa wajinga sana kwenye maswala ya mitandao kuna mambo mawili ambayo watu wengi hawakuyajua

1. Juzi wakati Raisi anafungua kiwanda cha polisi IGP alisema Polisi hawana teknologia ya kutosha. Rais Samia akasema sasa tulivyo andikisha simu kwa vidole ilikuwa na maana gani? swali la msing...
Mkuu Kamundu umeongea mambo machache lakini mazito sana kiusalama.
 
Livejr

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
1,833
2,000
Huyo Samia ni mnafiki yeye alikuwa ni mshauri wa mwendazake hana jipya anafurahisha watanzania
Unamshauri vipi JIWE, linashaurika Jiwe kweli.

Samia angetumia ushawishi gani kumshauri mtu aliyesema KICHAA? Anaweza kumshauri kichaa kwenye vikao lakini kitendo cha kutoka tu pale anakuwa na akili za Kichaa.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Nziiri

JF-Expert Member
Jul 23, 2020
448
500
Huyo Samia ni mnafiki yeye alikuwa ni mshauri wa mwendazake hana jipya anafurahisha watanzania
Sidhani Samia alikuwa na furaha kufanya kazi na Magufuli. Alikuwa na tabia mbaya hata ktk mahusiano baina ya mtu namtu. Hakuwa na hashima. Alikuwa hashauriki.

Samia kuwa mvumilivu imemlipa. Kama angeachia ngazi (fununu zinasema alijaribu kuachia system ikamkatalia) pengine leo ungekuta tuko na dikteta mwingine. Magufuli angeweza hata kumteua Sabaya awe makamu wake.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,466
2,000
Membe aliwahi kuwatahadharisha kuwa siku "wajanja wa duniani" wakijua Tanzania Kuna soko la udukuzi TUTAKWISHA....

"Wajanja" walianza kumdukua mzee baba akiwa anaongea na daktari wake wa Sauzi akimwelezea maswala ya betri,"wajanja" hawakukawia kumchania mkeka wa mitano Tena maamaeeee....
Hahaha! Umenikumbusha juu ya kachero mbobezi, mzee wa "niguse ninuke".

Halafu hao wajanja waliodukuwa mpk mazungumzo ya mzee baba na madaktari wake kisha kuzima betri wapewe ulinzi
 
Hechinodemata

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
1,186
2,000
Mzee kwa rais kujua nani ana awasiliana na nani ni kitu kidogo sana, hakuwa na haja ya watu kujisajili simu. Sema tu hujui kitu unagesi
Mbona hili tulilijua mapema sana. Kisa walitaka kujua Simu za Mbowe na Lissu basi. Yaani tanzania tuliingizwa mkenge kwa sababu magufuli alitaka kujua Mbowe na Lissu wanawasiliana na nani kitu gani na wapi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom