Uamuzi wa kuruhusu mabasi kutembea usiku, Hongera sana Waziri Kangi Lugola.

ChiefmTz

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
2,937
938
Habari wana jukwaa. Mnyonge mnyongenj, haki yake mpeni.

Natoa pongezi nyingi sana kwa Mh Waziri Kangi Lugola kwa uamuzi wake uliojaa utu na busara wa kuwaagiza Ma RPC kutozuia mabasi kutembea usiku kwa sababu za kiusalama.

Uamuzi huu unapaswa kupongezwa kwa sababu umetuondolea aibu kama Taifa ya watu wote kulala kwa kuhofia majambazi. Kwamba majambazi yanasababisha Taifa kulala huku tuna vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwamba uamuzi huu umetuondolea aibu ya kusimamisha saa ili kuokoa muda. Pia kwa uamuzi huu tunakwenda kushuhudia maendeleo ya haraka kwa Taifa kwa sababu utatupunguzia muda wa kulala na kuongeza muda wa kufanya kazi.

Kwa sasa mtu anaweza kutoka Dodoma usiku akaenda Dar akafanya shughuli zake na kugeuka siku hiyo hiyo na hivyo kuokoa muda na fedha.
 
Pia uamuzi unaondoa sintofahamu ya gani iliyotumika kuzuia mabasi kutembea usiku.
 
Ni uamuzi mzuri. Lakini wakiruhusu mabasi wazuie na malori. Madereva wengi wa malori wanaendesha hovyo sana usiku wanaweka full light na wengine wana usingizi - ni rahisi kusababisha ajali

Polisi kwa kutafuta ulaji kwenye marufuku marufuku kazi kweli kweli. Hapa inatafutwa nyingine toka kwa malori.
NWanaita bandika bandua. Kapona basi aingie japo lori.
 
Ni muda muafaka kwa SUMATRA kufanya rescheduling ya ratiba zao. Mtu akiomba ratiba ya usiku asinyimwe kwa sababu security wise hakuna kikwazo.
 
issue sio kusafiri usiku..issue kubwa ni hao madereva kusababisha ajali..maana kama mchana tu wanasafiri na bado tunashuhudia ajali ..itakuaje usiku..
 
Na haraka zenu mtachinjwa sana usiku sio na majambazi mtachinjwa na speed..
Usiku watu wanajiachia kinoma afu wengi wanaendesha fahamu ipo nusu sababu ya usingizi
 
Hii issue naona bado haijaeleweka kwa wengi, Hawajaruhusu kutembea usiku (ILA) kwa mabasi yaliyopo njiani kuelekea kule yanakokwenda na yanafika sehemu yanazuiwa ili kwa sababu hizo.

Mfano:
Dar to Kigoma
Musoma to Dar
Dar to Bukoba
Kigali to Dar
nk.
 
Usiku una mambo mengi sana wale dreva ni binadamu pia, kuna kupitiwa na usingizi kama wanadamu wengine; si tutaomboleza misiba ya kitaifa
 
Kama kweli ni hivi basi na mimi nilikuwa kundi la ambao hawajaelewa. Asante
Hii issue naona bado haijaeleweka kwa wengi, Hawajaruhusu kutembea usiku (ILA) kwa mabasi yaliyopo njiani kuelekea kule yanakokwenda na yanafika sehemu yanazuiwa ili kwa sababu hizo.

Mfano:
Dar to Kigoma
Musoma to Dar
Dar to Bukoba
Kigali to Dar
nk.
 
Habari wana jukwaa. Mnyonge mnyongenj, haki yake mpeni.

Natoa pongezi nyingi sana kwa Mh Waziri Kangi Lugola kwa uamuzi wake uliojaa utu na busara wa kuwaagiza Ma RPC kutozuia mabasi kutembea usiku kwa sababu za kiusalama.

Uamuzi huu unapaswa kupongezwa kwa sababu umetuondolea aibu kama Taifa ya watu wote kulala kwa kuhofia majambazi. Kwamba majambazi yanasababisha Taifa kulala huku tuna vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwamba uamuzi huu umetuondolea aibu ya kusimamisha saa ili kuokoa muda. Pia kwa uamuzi huu tunakwenda kushuhudia maendeleo ya haraka kwa Taifa kwa sababu utatupunguzia muda wa kulala na kuongeza muda wa kufanya kazi.

Kwa sasa mtu anaweza kutoka Dodoma usiku akaenda Dar akafanya shughuli zake na kugeuka siku hiyo hiyo na hivyo kuokoa muda na fedha.
Kama sababu za kuzuia mabasi kusafiri usiku zilikuwa sahihi si busara kuzipuuza. La sivyo huko mikoani watu watalala misituni kwa ubovu wa magari na barabara.
 
Back
Top Bottom