Uamuzi wa kukomoana ni ufisadi - Tendwa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Imeandikwa na Hellen Mlacky; Tarehe: 19th December 2011 @ 22:11


MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amevitupia lawama vyama vya siasa kwa kufanya uamuzi wa kukomoana na kusababisha gharama zisizo za lazima kwa taifa na kutolea mfano gharama za Uchaguzi Mdogo ambazo zinasababishwa na kuvuana uanachama, akizifananisha na ufisadi.

Kauli yake imetokana na hatua ya mwishoni mwa wiki ya chama cha NCCR-Mageuzi kumvua uanachama mbunge wake wa Kigoma Kusini, David Kafulila, hatua ambayo ina maana amepoteza kiti hicho cha ubunge na sasa taratibu za Uchaguzi Mdogo zitafuatwa kwa mujibu wa Katiba.

Tendwa amesema ingawa yeye siyo mhusika wa gharama za uchaguzi, lakini Uchaguzi Mdogo una gharama kubwa ambazo alisema si chini ya Sh bilioni 19 na uchaguzi kama huo unakuwa ni gharama kwa kuwa haukupangwa kufanyika.

Msajili huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana baada ya kutoa mada ya uongozi kwenye mafunzo ya viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa kuhusu uongozi, uwajibikaji na utawala bora.

Alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kuvuliwa uanachama kwa Kafulila, Tendwa alisema Katiba ya sasa hairuhusu mtu anapovuliwa uanachama kujiunga na chama kingine kuendelea na ubunge wake, hivyo ni lazima ufanyike Uchaguzi Mdogo kujaza nafasi hiyo.

"Sasa hizi bilioni 19 nani atakuwa amesababisha? Maana nyie ni mahodari wa kuandika mafisadi na hili je ni ufisadi au ni nini?

Maana tusiwe mahodari wa kuisema Serikali, bali pia vyama vya siasa vinapaswa kuisaidia Serikali badala ya kuisababishia hasara," alisema Tendwa na kuongeza:"Chama kufanya hivyo ni kupoteza sifa, nafikiri kuna adhabu nyingi ambazo zingeweza kutumika tofauti na kumfukuza uanachama, maana hii ni hasara.

Sisi hatuingilii uamuzi wa chama, ila huo ni ushauri maana hata walichokuwa wakijadili kwenye vikao hatukijui."

Tendwa alivitaka vyama vya siasa kutumia busara katika kufanya uamuzi badala ya kufanya uamuzi wa kukomoana katika vikao vyao na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa taifa ambazo si za lazima.

Msajili huyo alisema Kafulila anaweza kuomba rufaa ndani ya chama, lakini nje ya chama, pia anao uhuru wa kwenda mahakamani na atakaposhinda kesi atakuwa mbunge wa wananchi wake.

Akizungumzia suala hilo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye alisema yeye si muumini wa kuwafukuza wanasiasa vijana kwenye vyama vya siasa, bali ni muumini wa kuvitumia vyama vya siasa kuwalea vijana.

"Sisi tunategemea vijana wanakosea ila tukijenga utamaduni wa kuwafukuza wanasiasa vijana katika vyama vyetu nani atawalea na nani atawaelekeza vijana?

Mimi si muumini kabisa, mtu mzima utasema sasa huyu ameshindikana, lakini vijana hapana," alisema Nape na kuongeza: "Kijana akikosea leo afundishwe.

Sasa angalia suala la Kafulila, aliondoka Chadema na wakamuita sisimizi na majina mengine ya ovyo, baadaye amekwenda NCCR nao wamemfukuza, sasa aende wapi?"

Mafunzo hayo ya siku mbili yanawashirikisha viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa kwa lengo la kuwaelekeza kuhusu mahusiano yao na wanachama, kuona ni jinsi gani vyama vinawajibika katika ulinzi na usalama wa taifa pamoja na kuangalia maadili ndani ya vyama vya siasa.

Kwa upande wake, Kafulila akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, alisema hana tatizo na uamuzi uliotolewa na chama chake, bali anatulia.

Aidha, Kafulila amesema baada ya siku mbili kuanzia jana, ndipo atakapozungumzia kwa undani suala hilo kwa kuwa kwa sasa kuna taratibu zinazoendelea kufuatwa.

"Isingekuwa vizuri kuzungumza kwa sasa, najua wengi wangependa kunisikia zaidi, lakini sisemi kwa leo (jana)," alisema Kafulila aliyevuliwa uanachama Jumamosi iliyopita na Halmashauri Kuu.

 
Gharama zisizo za lazima ni pamoja na yale mabilioni ya pesa yaliyotumika ktk sherehe za miaka 50 ya ushuru.
Huyu Tendwa anataka vyama vya siasa hasa vya upinzani visifanye maamuzi magumu ili vizidi kutetereka na CCM izidi kubaka demokrasia.
Vipi kuhusu gharama za uchaguzi zisizo za lazima zitakazosababishwa na wabunge watakaoamua kujivua uanachama na ubunge kwa ridhaa zao wenyewe baada ya kuchoshwa na siasa uchwara ??
 
Huyu Tendwa naye asilete za kuzeleta kwani lini ameishaiwhi kuifuta hiyo sheria ya kipuuzi? Kama kweli angekuwa na uchungu si angesema sheria ni mbaya ibadilishwe hata Januari?
Huyu ni mpiga filimbi wa ccm. Hana lolote la maana zaidi ya kelele zisizo na maana. Achana naye tusije mrushia tusi kwa hasira.
 
huyu ni mpiga filimbi wa ccm. Hana lolote la maana zaidi ya kelele zisizo na maana. Achana naye tusije mrushia tusi kwa hasira.

njia ya kukabiliana na hili ni ndogo tu; ruhusu sheria ya mgombea binafsi. Katika sheria hii mbunge au rais anaruhusiwa kuhama chama na bado anakuwa na wadhifa wake. Ukikumbuka vema kwa kutumia sheria hii rais bingu wa mutharika wa malawi alihama chama na still akaendelea na kibarua. Mtikila anaifahamu vema hii sheria. Ruhusuni na acha kupayuka ovyo. Loser
 
Gharama zisizo za lazima ni pamoja na yale mabilioni ya pesa yaliyotumika ktk sherehe za miaka 50 ya ushuru.
Huyu Tendwa anataka vyama vya siasa hasa vya upinzani visifanye maamuzi magumu ili vizidi kutetereka na CCM izidi kubaka demokrasia.
Vipi kuhusu gharama za uchaguzi zisizo za lazima zitakazosababishwa na wabunge watakaoamua kujivua uanachama na ubunge kwa ridhaa zao wenyewe baada ya kuchoshwa na siasa uchwara ??

Umemaliza mkuu asante sana kwa ukweli usiopingika.
 
Ni aibu kwa Tendwa; hizo gharama anaziona kwa suala la Kafulila lakini kwa RA hakuziona! Double standard!
 
Huyu Tendwa ndiye fisadi mkubwa tena FISADI NYANGUMI. Na kujivika u-mouth speaker wa
CCM ndiyo tunazidi kumfahamu vizuri. Tendwa anajua kabisa tatizo liko kwenye katiba
mbovu tuliyonayo. Kama kweli ana uchungu na hizo billion 19 za by election awambie CCM
wenzake hata kesho wapeleke mswaada bungeni wa kufuta hiyo sheria inayolazimisha mbunge
awe mwanachama wa siasa au mbunge anapovuliwa uanachama basi asipoteze ubunge wake
kwani amechagulia na wananchi wote. Huo ndiyo mworobaini wa tatizo hili la kuvuana unacahama.
Kama kweli kuna political will hili wala halihitaji katiba mpya.

Lakini Tendwa badala ya kuwa mlezi wa vyama vya siasa ambaye angetetea ustawi wa demokrasia nchini,
amejivika u-mouth speaker wa CCM wa kuviza demokrasia nchini.

Poor Tendwa huyo ushauri wako kawapatie MAFISADI wenzako, tuondolee hapa hiyo childish argument.
 
Back
Top Bottom