Uamuzi wa kuishi pamoja: Je ni sahihi mwanaume au mwanamke kuhamia kwa mwenzake....? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uamuzi wa kuishi pamoja: Je ni sahihi mwanaume au mwanamke kuhamia kwa mwenzake....?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 17, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Mmekuwa wachumba kwa takriban miaka miwili hivi, lakini kila mmoja akiishi kwake(mwanaume amepanga nyumba nzima kubwa na mwanamke anaishi kwenye nyumba yake aliyojenga mwenyewe). Mmeshakubaliana kufunga ndoa lakini bado hamjaanza mchakato wa kukamilisha jambo hilo. Baada ya kushauriana mkakubaliana muishi pamoja ili kumudu kutunza fedha kwa ajili ya kukamilisha ndoto yenu ya kufunga ndoa.

  Je ni sahihi mmoja kati yenu kuhamia kwa mwenzake au kutafuta makazi mapya sehemu nyingine na kuhamia hapo kwa pamoja...?

  Je mwanaume, utakuwa tayari kuhamia kwenye nyumba ya mpenzi wako ili kuepuka gharama zisizo za lazima za kulipa kodi?

  Hebu fungukeni wana jamvi...............
   
 2. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mhm kwanza kabisa mambo ya cohabitation ndio yanaleta matatizo kwenye ndoa baadae. so mie naona bora tuendelee kukaa kila mtu na kwake....plus kuhamia kunaongeza uwezekano wa mie kummega kabla ya kufunga ndoa which is not right
   
 3. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mtambuzi wapenda kuleta mada za uchokozi sana.kuhusu mada, kwangu itadepend kama nahitaji kuzuga tu na huyo mwanaume au kama ni wa future .i.e kujenga family
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  napinga kuhamia kwa mwenza, hii husababisha kujibweteka na kusahau kufunga ndoa.....
   
 5. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mi naona sahihi mtakuwa mnaishi kihawara hawara ambapo mapenzi yake yanadumu kwa muda mrefu na ni matamu.
   
 6. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,068
  Trophy Points: 280
  kizazi hiki cha mwisho kwelikweli ..mnafunga ndoa kwanza ama mnaishi kwanza,be clear,wat's ur most primary goal??
   
 7. mzurimie

  mzurimie JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 6,151
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  Nitamwambie aje kwangu.

  Mie sitafikiria mapenzi kuharibika, nitafikiria hiyo pesa ya rent ije ilipe mkopo kama mnao. Kama sina ntafanya tuongelee uzalishaji pesa tulizonazo.

  Then pesa zingine tufanye investment ya kufaudu wote. Kufungua joint acc kila mmoja aweke kiasi fulani kila mwezi.

  Hapo ndipo utamu, na kwenda likizo ya shopping akishaamia.
  Etc

  Mengine mbele kwa mbele.
   
 8. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  inategemea na malezi
   
 9. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Najaribu kufikiria kaka Mtambuzi, bado mko katika hali ya uchumba halafu mwanaume unahamia kwa mwanamke, duuu, sijui naiona imekaaje vile!

  Naona kama kuna hatari ya mwanaume kuonekana umefuata mali za mwanamke (nahisi hayo ndiyo yatakuwa mawazo ya baadhi ya ndugu wa mwanamke na majirani pengine na baadhi ya ndugu zako!) ama la kuna hatari ya mwanaume kuonekana kama binti (Hapa ni kama alivyoimba lady Jay Dee!)

  Kwa mwanamke kuhamia kwa mwanaume sioni tatizo sana endapo uchumba huo utageuka ndoa baadaye, ila ni tatizo kubwa endapo uchumba huo utagoma kugeuka kuwa ndoa na hivyo kumlazimu mke kuanza kutafuta pa kukimbilia, LOL!

  Ni mtazamo tu ...:A S embarassed:
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wanaume wa siku hizi wanavyopenda dezo!
  Atahamia haraka sana zamani ilikuwa ngumu sana kwani wanaume walikuwa wa ukwe .....lol!

  Kwa matazamo mwingine hapo ni kuendeleza na kurasimisha uasherati maana bado hamjafunga ndoa.
   
 11. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,121
  Trophy Points: 280
  Hahahaaa! Mtambuzi naona umeamua kutoniiita nichangie humu!!!! LOOOOO! Sasa ndo nachingia kinguvu!

  Mwanaume haipendezi kabisaa kuhamia kwa mwanamke sababu kuu 3

  1. Unaonekana umeolewa, japo watu hawakuchani live!!!!
  2. Ndugu zako wataisoma namba kuishi hapo, weeee! Wakutane na ndugu wa wife wataonekanaje maskini wa kutupwa?
  3. Siku mkikorofishana utaambiwa haya TOKA KWANGU UPESIII!!!!!
  4. Wakwe watakuwa wanakuchukulia kwa wasiwasi sana kama mpenda vya bure flanii!

  Mwanamke ni haki yako ya msingi kabisa kwenda KUJIPOSITIPON NDANI YA TERRITORY YAKO!!!! Zubaaa zubaaa utakuta mwana si wako!!!! Ohoooo!
  Hata kama waona aibu kuhamia jumlala kaweke SURVEYORS MARK au Bench Marks kuonesha territory imepimwa na inammiliki legit. Hapo tunaongelea kutupi MIPICHU yako(USED), SIDIRIA, LIPSTIC, HANDBAG, KHANGA N.K ilihali waianika kabisa ili mtu akija asione kaokaota fuko la hela kwenye maandamano, AJUE HIZO NI ANGA ZA WENYEWE!!!!!!!!!!! Kimbembe mkiachana, mi siendagi kufata hivo vitu wala nini, akitaka avichome tu!!!! LOL!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. mdida

  mdida JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  LOh yote nilikuwa nayo umeshasema Lara1 hata nakupa like 6
   
 13. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Pia kuna uwezekano mkubwa mkajisahau kabisa na hiyo ndo msije kufunga na mkaishia kuibariki tena kwa shinikizo...

  Halafu na sie huwa tunapenda makomplikesheni..Hivi kufunga ndoa lazima kuwe na matarumbeta na uvae shela?Si mnaenda tu watu 4 na ndoa inafungwa na maisha yanaendelea????Tatizo huwa tunapenda kufanya mambo ambayo watu wanataka na sio sisi tunataka..
   
 14. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi nimekumisijiee i hope umepata japo maji ya kunywa kimtindo!
  :focus:hili la kuhamia kwenye nyumba ya mpenzi awe wa kike au wa kiume sio yenyewe bana!
  mambo ya kuanza kujuana kiasi hicho kabla ya kufunga ndoa sio mazuri mara nyingi ndoa hazifingwi kwa sytle hii!mtu anaona sa nioe au niolewe ili kiwe nini?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,606
  Trophy Points: 280
  Suala la kuishi pamoja kabla ya ndoa si sahihi haijalishi unaishi kwa mwanaume au mwanamke.
  Lakini kuishi pamoja baada ya ndoa kwa mwanaume kujimuvuzisha kwa mwanamke binafsi sioni tatizo lolote as long as hiyo nyumba huyo bi shost alikua akiishi alone.
   
 16. c

  christmas JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,603
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  mtambuzi inategemea na makubaliano yenu wote wawil hakuna cha kusema mmejisahau, kama ni tutaishi pamoja then after 3 months tunaoana na mambo yanapangwa upya me sion tatizo kabisa. lla sio mipango mingi utekelezaji 0
   
 17. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kwa mwanaume inatakiwa mwanamke ahamie kwako
  nyumba yake apangishe
  pesa muingize kwenye matumizi mengine
   
 18. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Mmmh, eti kuhamia kwa mwanamke au mwanamme ni uasherati, hii kitu ipo na itaendelea kuwepo.
  Ndo maana hata makanisa yana option ya kubariki ndoa.

  Afu naona watu wanachohofia sana ni "ndoa" kuliko maelewano ya uhusuano huo
  ndoa ingekuwa ndio suluhisho la furaha au kuishi pamoja kusingekuwa na 'divorce'
  Ndoa inaku-guarantee kuvumilia matatizo zaidi ya uhusiano kuliko kuishi heregeni

  Afu, hii dhana ya mwanamme hakuna kuhamia kwa mwanamke inaniudhi mno.
  Hivi tukapange wakati nyumba ipo?, eti sababu tu ya ego ya mwanamme, why?
  Mie kama mwanamme haniamini kiasi cha kushindwa kuhamia kwangu na ATAMBAE MBELE
  Nitatafuta atakayejiamini kukaa kwangu.

  Kwa hiyo mwanamke kama hajaolewa asijenge, inahu!!!!!
   
 19. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  utatafuta mpaka uchoke, yaani mie mbaba mzima na ndevu zangu nibebe masanduku na kuhamia kwa mwanamke, kuwa serious mama. no way.
   
 20. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Sitafuti, kama wanawake wanavyowahitaji wanamme, na wanamme wanawahitaji wanawake hivyo hivyo.
  Why should I suffer kuwatafuta???

   
Loading...