Uamuzi wa kesi ya Uchaguzi, Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila dhidi ya Husna Mwilima na AG!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Ile Kesi iliyofunguliwa na aliyekuwa mbunge wa kigoma kusini Ndg David Kafulila dhidi ya mbunge wa sasa wa jimbo hilo Ndg Husna Mwilima, inatarajiwa kutolewa maamuzi yake leo.

Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na iko chini ya Jaji Ferdinand Wambari.

Katika kesi hii upande wa mlalamikaji (Kafulila) unaongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) unaongozwa na wakili Kenedy Fungamtama pamoja na mawakili wa serikali upande wa mwanasheria mkuu.

Hoja za pande zote zimekamilika na sasa uamuzi wa mahakama ndio unasubiriwa leo hii,

STAY TUNED.

=============================
UPDATES.

Mahakama imemtangaza Ndg Husna Mwilima kuwa ndiye mshindi halali wa uchaguzi huo na hivyo kumbwaga Mlalamikaji ndg Kafulila.

Hata hivyo Kafulila hajaridhika na uamuzi huo na hivyo anakusudia kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
 
Kafulila anarudi Bungeni...kwa kishindo na anarudi na escrow yake kama kawa!! Tumbili katika ubora wake....! Kila la kheri Tumbili
 
Mahakama itende haki kwa huyu jamaa hapo huwa naamini goli la mkono lilihusika....mr.kafulila i wish you well!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ni Kweli aiseeee Kafulila ameshindwa ile kesi! Kama siamini hivi!!! It's not fair kwa kweli! Ile kesi Kafulila alitakiwa ashinde!!
 
MMkuu hukumu imeishatoka au ni ndoto tu za mchana?
na kama ni ndoto hautatumbuliwa jipu kwa kulala usingizi kazini?
Mimi siandikagi uzushi kama nyumbu. Hukumu tayari na Kafulila kashindwa
 
Ni Kweli aiseeee Kafulila ameshindwa ile kesi! Kama siamini hivi!!! It's not fair kwa kweli! Ile kesi Kafulila alitakiwa ashinde!!
Ile ni kesi ya wenyewe kwahiyo kushindwa kwake ni mpango maalum uliosukwa kwa ustadi sana....siasa za Afrika zizi la nguruwe lina nafuu
 
Mchangieni hela akakate rufaa... Maana keshapoteza kama 100m hivi
Tutamchangia akiitisha harambee, bado tunaamini ushindi wake upo na umeshikiliwa na kundi la wanaoishi kwa hofu ya kuumbuliwa. Kafulila anatakiwa awe bungeni!
 
Back
Top Bottom