"Uamuzi Wa Busara" Kitabu kilichofuatia "The Torch on Kilimanjaro"

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
Ndugu zangu baada ya kitabu hiki "The Torch on Kilimanjaro," kuhujumiwa nikajituliza.

OUP wakanirudishia kwa masikitiko makubwa mswada wangu mpya niliowapa wakaniambia kuwa inaelekea sipendeki kwetu kwa hiyo vitabu vyangu haviwezi kusomwa katika shule za Tanzania.

Nikashukuru nikawa katika subra.

Haukupita muda mrefu nikajikuta nimeingizwa kwenye mradi mpya wa kuandika kitabu cha historia nyingine ya Tanzania.

Publisher mmoja kutoka Kenya akaniomba niandike kitabu kuhusu Uamuzi wa Busara wa Tabora wa mwaka wa 1958 maarufu kama Kura Tatu.

Nikampa mswada na akachapa kitabu.

Kura Tatu kama wengi tujuavyo iligawa TANU katika mapande mawili makuu.

Sheikh Suleiman Takadiri Mwenyekiti wa Baraza la Wazee alikuwa upande mmoja na Zuberi Mtemvu wakipinga kushiriki uchaguzi wakiungwa mkono na wanachama wengi wa TANU.

Julius Nyerere alikuwa upande mwingine akitaka TANU iingie katika Kura Tatu.

Hoja ilikuwa ili TANU ipate viti ndani ya Baraza la Kutunga Sheria (LEGCO) ni lazima wachaguliwe kwa kura.

Lakini tatizo Waingereza waliweka masharti magumu ya kibaguzi ambayo yaliwatoa Waislam waliokuwa mstari wa mbele katika kupambana na Muingereza katika kugombea nafasi na pia katika kupiga kura.

Walitakiwa wagombea na wapiga kura wawe na elimu ya kidato cha 12 na wawe na kazi inayotambulika na yalikuwapo masharti mengine pia.

Waislam kwa masharti haya wakajikuta wametupwa nje ya ulingo wa siasa juu ya wao kuunda TANU kuijenga nk. nk.

Hii ilileta matatizo ndani ya TANU.

Kisa kirefu.

Kitabu nikakiandika na mhariri kalamu yake ilikuwa kali sana kwangu mwandishi.

Mchapaji alikusudia kitabu hiki kiandikiwe utangulizi na Rais Kikwete na kiwe kama kumbukumbu ya miaka 50 ya kukumbuka Azimio la Busara la Tabora na kukumbuka jinsi Baba wa Taifa kwa busara kubwa kabisa aliukwepa mtego wa Waingereza na TANU ikaibuka na ushindi mkubwa wa kuzoa viti vyote na chama kikabaki kikiwa na nguvu haba jana.

Ndoto ya publisher haikutimia.

Kitabu kilichapwa na yote aliyofikiria Publisher hayakuwa.

Picha: Jalada la kitabu, picha ya pili kulia inamuonyesha kushoto Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia na Julius Nyerere.

Picha ya tatu kushoti upande wa kulia ni Sheikh Suleiman Takadir na huyo.kijana aliyeshika tama ni Zuberi Mtemvu na mwisho kushoto ni John Rupia ambae amemziba Julius Nyerere.
Screenshot_20201125-181002.jpg
Screenshot_20201125-191047.jpg
Screenshot_20201125-190658.jpg
 
Ina maana Nyerere alishirikiana na wakristu tu baada ya uamuzi huo wa waingereza kuhusu kura tatu?
Rogo...
Hapana TANU iliibuka na nguvu zaidi baada ya Kura Tatu na ikashinda vyama vilivyokuja kuundwa kuipinga kama Congress na AMNUT.
 
Congress ya Zuberi Mtemvu na AMNUT chama cha waislamu!!!
Bulesi,
AMNUT hakikuwa chama cha Waislam labda kwa hilo jina tu.

AMNUT ilipigwa vita na kila Muislam hadi kufikia kushindwa hata kulipa kodi ya ofisi yao iliyokuwa Libya Street ikahama ikaja Kariakoo.

Waislam kama walikuwa na chama basi ni TANU.
 
Ilikuaje waislam ndo wawe waasisi wa kila jambo halafu kila andiko unasema hawatambuliwi
 
Back
Top Bottom