Uamuzi mdogo kuhusu kesi ya Lissu na Gazeti la Mawio Waahirishwa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Jana kesi inayomkabili Tundu Lissu na wahariri gazeti la mawio iliahirishwa baada ya Tundu Lissu kumchachafya vibaya sana shahidi namba moja wa Jamhuri.

Kesi hii imeendelea leo ambapo..

Hakimu Mkazi Thomas Simba wa Mahakama ya Kisutu, amewaambia watuhumiwa wenye kesi namba 148, 2016 inayomkabili Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kuwa Rulling ya kesi hii itakuwa Feb 23, kisha Machi 8,na 9 Machi tutaendelea na Hearing.
---
Rulling ni kwa ajili ya suala la Zanzibar na Uchaguzi wake liendelee kujadiliwa au la. Likiruhusiwa ndio hearing inaendelea. Majibizano hayakuwepo leo.
 
Mkuu vipi Leo hukuwepo mahakamani?maana umeiandika kifupi sana,Leo hapakuwepo majibizano ya kisheria?
 
Nahisi kama vile sirikali inajifunza sheria kupitia njia ya kumpeleka Tundu Lissu mahamani. Hii naona ni njia ya sirikali kupata "Tuition" ya bure toka kwa Lissu. Naomba Lissu aanza kuwatoza hela ya "Tuition". Hakuna cha bure.

Siku chache zilizopita mkuu wa kaya alisema majaji huwa wanaahirisha kesi ili angalau mawakili wa sirikali wajipange lakini wakili awamu nyingine wanakuja vibaya zaidi kwa kusahau hata walichosema jana yake.
 
Hapo wanachezea kodi zetu hamna kesi mawakili upande wa serikali na mashahidi wao wanatia huruma wanashindwa hata kujibu hoja zao wenyewe ni aibu sana.

Nadhani very soon Prof Kabudi ataanza kusimama ktk hizi kesi kwa niaba ya serikali kwani hizi aibu zinatuchefua makada wa CCM, kumbuka pia yule wa jana ktk suala la Manji kaita media kwa mbwembwe kabisa ili kufyatua masuala ya sheria akseh niliBROOOW sana jinsi alivyoshusha na kutamaraki out of pwenti
 
Loooh!!Kweli siku ya kutembea uchi ndio unakutana na mkweo!Leo nimekimbia mapema kukaa kiti cha mwanzo kuona Kamanda wa Polisi anavyotekenywa,lkn hakukuwa kama jana.

Nimeambulia kumuona bwana mdogo Yericko Nyerere na Kibatala....

Ila Lissu ni "Online Open University",unapata "tuition" bila ada!!Kupitia Wakili Tundu Lissu nimejifunza kuwa kumbe mkiwa mahakamani polisi wanakuwa "wadogo kama piliton" unaweza kuwageuza geuza kama chapati ya maji.

Nimeamini vijijini,watu wengi hufungwa kwa woga tu wa Poisi kuwa shahidi wa kwanza!!
 
Maji yamezidi unga
pastpast [/IMG]
Nadhani very soon Prof Kabudi ataanza kusimama ktk hizi kesi kwa niaba ya serikali kwani hizi aibu zinatuchefua makada wa CCM, kumbuka pia yule wa jana ktk suala la Manji kaita media kwa mbwembwe kabisa ili kufyatua masuala ya sheria akseh niliBROOOW sana jinsi alivyoshusha na kutamaraki out of pwenti
 
Attachments

  • IMG_20170213_135053.jpg
    IMG_20170213_135053.jpg
    8.1 KB · Views: 9
Hahahaaa..!!!!!...kweli hii inaonekana kabisa kuwa wanatakiwa kunolewa tena....sasa wanaweza kumlipa huyu Lissu stahiki zake zote kweli.! Ifike mahali serikali iache mapambano yasiyokuwa na mbele wala nyuma. Wakiibua kesi iwe na mashiko na si kutegemea ubabe wa kupindisha sheria na katiba au kuiteka mahakama kama tunavyoona kwenye baadhi ya kesi. Hivi watawala (na si viongozi) hawajajua tu bado kwamba wananchi wengi nyakati hizi wapo makini kufuatilia yanayotendeka na ni vigumu sana kuwadanganya? SERIKALI ACHENI MANENO WEKENI MUSIC...SOMENI ALAMA ZA NYAKATI..si kila mahali kuboronga hata paspotakiwa kama yalojitokeza kwenye mapambano muhimu na hatari ya DAWA ZA KULEVYA
 
Mkuu vipi Leo hukuwepo mahakamani?maana umeiandika kifupi sana,Leo hapakuwepo majibizano ya kisheria?
Ameandika kwa kifupi sana, lkn na wewe umesoma kwa kifupi zaidi. Maana kama ungesoma mpaka mwisho ungeona sehemu aliyoandika kuwa majibizano hayakuwepo leo.
 
Jana kesi inayomkabili Tundu Lissu na wahariri gazeti la mawio iliahirishwa baada ya Tundu Lissu kumchachafya vibaya sana shahidi namba moja wa Jamhuri.

Kesi hii imeendelea leo ambapo..

Hakimu Mkazi Thomas Simba wa Mahakama ya Kisutu, amewaambia watuhumiwa wenye kesi namba 148, 2016 inayomkabili Tundu Lissu na Wahariri wa Gazeti la Mawio kuwa Rulling ya kesi hii itakuwa Feb 23, kisha Machi 8,na 9 Machi tutaendelea na Hearing.
---
Rulling ni kwa ajili ya suala la Zanzibar na Uchaguzi wake liendelee kujadiliwa au la. Likiruhusiwa ndio hearing inaendelea. Majibizano hayakuwepo leo.
Chachu, leo nilikuwa na kimuhemuhe kweli nisikie kuanzia ilipoishia jana. Lakini utabiri wangu ni kwamba ruling itakayotoka ni kwamba suala la Zenji lisijadiliwe ila kesi ya msingi iendelee. Ikiruhusiwa ya Zenji yajadiliwe yatakuwa kama ya Thriller ya Michael Jackson. Makaburi yatafukuliwa na mazombi kutoka.
Hata kama Jamhuri haitakuwa na hoja ya mashiko kutokuruhusu ya Zenji kuongelewa, "busara" itatumika kuyaondoa. Hata hivyo uweupe wao ushaonekana. Time will tell.
 
Back
Top Bottom