Uamsho waijibu UVCCM na Steven Wassira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uamsho waijibu UVCCM na Steven Wassira

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Revolutionist, Jun 6, 2012.

 1. Revolutionist

  Revolutionist Senior Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku chache baada ya UVCCM kudai kuwa uamsho wamo serikalini, taasisi hiyo ya Uamsho imeibuka na kujibu hoja hizo kama ifuatavyo:
  ---------
  Tunawajibu Stiphen Wasira na UVCC

  Jana tulisikia kauli zenu na mkasema Uwamsho wapo Serikali, sisi tunayakubali maneno yenu na tunakiri kuwa ni kweli Muamsho wapo Serikalini.

  Nyinyi mmeshindwa kuwataja kwa majina sisi tutawataja kwa majina na vyeo vyao.
  ...
  Muamsho wa kwanza ni Kikwete, yeye ametuamsha na ametwambia wazi Wazanzibar kuwa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba haitoratibu Muungano hivyo ametuamsha na kutueka bayana Wazanzibar kuwa Tume haituhusu, sisi Wazanzibar kinachotuhusu kwenye Katiba ni Muungano hivyo katuamsha kuwa Tume hii ya Katiba si ya Muungano.

  Kikwete huyo huyo ametwambia kuwa Muungano ushavunjwa na CCM NEC, na alisema NEC imeshaamuwa kuwa Rais wa Zanzibar asiwe Makamu wa Rais wa Muungano, hivyo ametuamsha kuwa NEC imeenda kivyume na Hati ya Muungano na kwenda kivyume na makubaliano ni kuyavunja makubaliano, hivyo NEC imeuvunja Muungano.

  Muamsho Mkubwa ni Pinda nae ametuamsha pakubwa tena akatutowa kwenye usingizi mzito pale alipotwambia kuwa Zanzibar si Nchi na alipoambiwa ni nchi amekosea akasema sijakosea wala sijalewa Zanzibar si nchi, ametuamsha pakubwa Pinda.

  Muamsho mwengine ni Nyerere alitwambia amechoka na sisi Wazanzibar na hapa namnukuu "tumechoshwa na Wazanzibar na Uislaam" kama si Muamsho nani?

  Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, yey katuachia uswiya na alitwambia Muungano kama koti likikubana livuwe nae pia ni Muamsho.

  Muamsho mwengine ni Mansour Yussuf Himid nae katuamsha sihaba pale aliposema ndani ya Baraza la Wawakilishi kuwa Serikali moja hataki kuisikia, mbili ni butu, anataka Serikali tatu au vyenginevyo.

  Amani Karume wa Pili nae katuamsha tena haitoshi akatuletea Umoja wa Kitaifa na Mabadiliko ya Katiba ya 10 ya Katiba ya 2010 tena akaifanya iwe shoka la kuvunja Muungano, isomeni vizuri Katiba ya Zanzibar na hapo mtajuwa kuwa ni Muamsho au si Muamsho.

  kwa hiyo Stiphen Wasira na UVCCM hamjakosea kusema Muamsho wapo Serikalini, ni kweli, tena wapo serikali ya Chama chenu, wala msimtafute mchawi, wachawi wenyenu.  [​IMG]
  SOURCE: http://www.facebook.com/UamshoJumuiyaYaMihadharaYaKiislamuZanzibar

   
 2. S

  Senator p JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanayoyasema ni kwel,2 maneno n uchawi tosha,ndio maana sijawah sikia mganga wala mchawi bubu.
   
 3. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Tusubiri UVCCM watawajibu.
   
 4. Aza

  Aza JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 1,672
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  yani nimecheka,so wote hao ni uammsho
  waunguja raha sana
   
 5. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,024
  Likes Received: 198
  Trophy Points: 160
  hii ni movie ya kihindi..mwisho wa siku sterling lazima afe......
   
 6. majorbuyoya

  majorbuyoya JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,815
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Magaidi wameamua kutoa tamko, ok safi sana na tumsubiri Nepi nae atatoa 'Season' inayofuata. Hapa wanaweza wakatoa kibao kimoja kikali sana cha Mipasho maana wamekutana wote watu wa mipasho.
   
 7. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #7
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...ama kweli jina la hiki kikundi(uamsho) limekaa kimtego-mtego...Wasirra "ukijua huu wenzio wanjua ule!"...
   
 8. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #8
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,389
  Likes Received: 6,565
  Trophy Points: 280
  kichefu chefu
   
 9. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Timed Bomb. mark my words!!!!!!.

  Nina tabiri hili bomu kulipuka kabla ya mwisho wa mwaka huu. CCM kubalini yaishe.
   
 10. m

  mamajack JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
   
 11. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Tik... tok... tik.. tok.. tik. tok. *******BOOOM******
   
 12. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Is this Indian, Chinese or American movie?
   
 13. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Duh..amakweli "ukijua huu wenzio wanajua ule!"
   
Loading...