Uamsho waendelea kusota rumande.

Bangoo

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
5,597
1,005
Viongozi wa kikundi cha kiislamu cha uamsho cha zanzibar wamefikishwa tena leo ktk mahakama ya mwanakwerekwe znz na kururudishwa rumande kwa kuendelea kukosa dhamana.

Wakili wao ameendelea kulalamika kutokana na wateja wake kuendelea kunyimwa dhamana,

ktk hali nyingine wakati viongozi hao wakitoka mahakamani walitamka maneno yafutayo (mnataka muungano? Walikuwa wanawauliza baadhi ya wafuasi wao waliojitokeza, na wale wafuasi walijibu hawautaki muungano!

Itv habari
 
Walau kidogo zenji kumetulia ni jukumu la shein kuendelea kukandamizia hawa jamaa hukomahabusu ili aendelee kuwa na amani au awaachie huru waje kuhubili chuki vurugu na uchomaji wa makanisa uanze tena.
 
Hii kesi ipigwe kalenda hadi baada ya 2015, baada ya hapo awe convicted, afungwe miaka 10 jela!
 
Hii kesi ipigwe kalenda hadi baada ya 2015, baada ya hapo awe convicted, afungwe miaka 10 jela!

itajwe tena mpaka 2015, Rais akiapishwa ndio isikilizwe kuepusha uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi,dhamana isitolewe kwa usalama wao manake hawatakiwi uraiani.
 
Hivi ya Ponda ni lini wakuu? Hii ndio isikilizwe baada ya rais wa awamu ya tano kumaliza kipindi cha kwanza yaani 2020 halafu no dhamana.
 
Kisheria kila mtu ana haki ya kupata dhamana, isipokuwa muuaji na mbakaji na wangine wanaofana na na hao, watu wanaotaka tuuane wenyewe kwa wenyewe wanafaa kuwa rumande.
 
Kama maoni ya Great thinkers ndiyo kama haya! sijui small thinkers maoni yatakuwaje!
 
This guy played the wrong cards....hakukua Kikwete sio muoslam bali rais wa tanzania.

**** tofauti kubwa kati ya kuwa muislam na kuwa rais wa Tanzaia.
 
Kisheria kila mtu ana haki ya kupata dhamana, isipokuwa muuaji na mbakaji na wangine wanaofana na na hao, watu wanaotaka tuuane wenyewe kwa wenyewe wanafaa kuwa rumande.

ponda na uamsho ni zaidi ya mbakaji na muuaji
 
Wao walisahau kuna sheria za nchi na watawala wapo!!!
Duh afadhali kale kaupepo kafujo kamepita....
 
Kesi ya Ponda ina mkono wa mtu mzito sana anaeshinikiza asifukuzwe nchini....maana aliwatumia kina Ponda na wenzake kumsafishia njia ili kufika ambapo yupo sasa,ushauri na maamuzi yaliyopo ni kuimfukuza nchini na azuiliwe kuingia tena Tanzania.....sasa dhamila inamsumbua huyo kigogo!!!
 
Ni lini watu watakua hiari kutibiwa makengeza waliyonayo? Watawala siku zote ni watesi wa wanaukombozi. Watatumia magenge yasiyofahamika kutengeneza uzushi ili jamii iwachukie wanaukombozi. Ponda anaongoza madai ya haki za waislam na haki hizo haziwahusu watu wasiokuwa waislam. Uamsho wanadai maslahi ya nchi yao ambayo mafisadi hawako tayari kuachia udhalimu wao. Sasa hapa tutafakari; kwa nini Desmond Tutu hakuwaunga mkono makaburu? kwa nini wamisionari walioshughulikia roho enzi za ukoloni waliunga mkono wakoloni watesi? Ukiona kiongozi yeyote wa dini anaungana na serikali inayolalamikiwa na wananchi basi huyo ni puppet. Kiongozi wa dini anayechukia ufisadi haungi mkono serikali ya kifisadi. Kuchoma makanisa ni mbinu iliyotengenezwa kwa ustadi mkubwa na kuajiriwa vijana wakajiingiza katikati ya vijana wasio na ufahamu wa dini bila kuelewa agenda. lakini viongozi wa uamsho wala akina Ponda hawawezi kupanga agenda hiyo. Hamjaona makanisa yaliyogeuka misikiti? Sasa wakichoma watapata wapi majengo yatakayotumiwa na wakristo walioamua kwa hiari yao kuingia uislam na kuyafanya makanisa yao kuwa misikiti? Turuhusu akili zetu kufanya kazi kwa uhuru.
 
Wako ndani bado wanaendesha campaign zao za uchochezi,
Watasota sana!
 
Back
Top Bottom