Uaminifu umekuwa changamoto sana kuanzia kwenye mahusiano, ndoa, taasisi hadi serikalini

Apr 19, 2018
83
112
Tuko kwenye dunia ambayo inakuwa kwa kasi kiteknolojia lakini bahati mbaya upande wa maadili haufanyi vizuri kabisa.

Naomba tujadiliane juu ya suala nyeti sana "Uaminifu!" Kwa kweli hili limekuwa changamoto sana kuanzia kwenye mahusiano, ndoa, Taasisi hadi Serikalini, kote ni utata.

Sasa kasheshe inakuja kwa watu ambao wanatafuta wenzao wa kusaidiana katika eneo fulani la Maisha iwe kiuchumi au kijamii kwa mfano inapofikia wakati unahitaji;

Mwenza wa biashara (A business partner)
Mwenza wa ndoa (Marriage couple)
Mfanyakazi wa taasisi yako au biashara yako, hasa vitengo nyeti kama watunza fedha na wengineo.

Swali linalokuja ni: "Nimwamini nani?"

UKWELI NI KWAMBA;
Maisha kuna wakati lazima utahitaji mtu wa kukushika mkono au kushikana mikono ili mwende hatua ya juu sana.

Angalia watu wote waliofanikiwa, hawajafika hapo kimiujiza lazima waliwapata watu "waaminifu" katika kufanya nao jambo fulani ndo maana jambo hilo limefanikiwa.

Angalia kampuni kubwa zote, biashara zinazotamba, Taasisi zilizosimama, ndoa zilizo imara n.k, wote wamekutana na wenza wenye umoja na uaminifu ndo maana wamevuka milima na mabonde mpaka kufika hapo walipo.

SASA TUNAFANYAJE?
Kwa kweli, si rahisi kumpata binadamu ambaye 100% kakamilika, lakini cha kujiuliza, mbona wenzetu hao ma-guru maeneo fulani fulani wamewapata watu wa kufanya nao maendeleo na wametoboa? Wametoboaje?

1. Utake usitake kuamini mtu ni lazima, labda ukatafute sayari yako. Kuna jukumu fulani kwenye jamii, familia au Taasisi lazima utamwamini mtu na kumkabidhi tu.

Lakini; waliofanikiwa wanaamini na kuhakiki. Yes, kwa sababu ili tuendelee lazima tuaminiane, basi isiwe shari, unamwamini mtu halafu unahakiki kama ulichokiamini ndicho au ghorogoshi.

Unafanyaje? Wekeaneni malengo hususa kwa muda hususa halafu muambizane wazi kabisa kuwa lengo fulani na fulani lisipofanikiwa kufika tarehe fulani basi hapo "uaminifu" wangu kwako utakuwa wa shaka, na hatutaweza kwenda pamoja.

(Naomba nisieleweke vibaya, hivyo vitu mnavyoviweka kwenye malengo hakikisha ni vitu vilivyo ndani ya uwezo wa huyo mtu unayetaka kufanya naye kitu fulani, usizidishe uwezo wake, hapo utavuruga mambo)

2. Kaa na mtu mwenye mtazamo sawa na wa kwako. Usitafute patner ambaye wakati wewe uko sayari ya zebaki, mwenzako yuko pluto kimtazamo. Hapo ukimwambia jua linatoa joto kali, atakwambia jua lina baridi kali kwelikweli. Na kumbe mmetofautiana mitazamo.

Na ikiwezekana muwe mnashabihiana vipenda roho, kama mnapenda mpira basi wote muwe hivyo "washabiki wa mpira", Kama wasoma riwaya, basi angalau na mwenzio awe hivyo, mtu wa riwaya.

Kwanini? Kwa sababu mkiwa mna vitu vingi vinavyoendana, muda mwingi mtakuwa mnawasiliana.

Kwa mfano; Mkurugenzi Joshi na Mfanyakazi wake John. Wanakutana kazini saa 2 asubuhi wanatoka saa 9. Lakini kwa sababu wote ni washabiki wa mpira, wanaongozana uwanja wa taifa kuangalia soka mpaka majira ya saa 1 jioni.

Lakini wakati huohuo Hemedi naye ni mfanyakazi kwenye kampuni hiyo hiyo ya akina John, Ila yeye hapendi Mpira, akitoaka zake kazini anaenda zake nyumbani kuangalia Movie.

Ukweli ni kwamba taasisi yoyote ile inakuwa endapo kuna uwazi na mawasiliano miongoni mwa wafanyakazi. Hivyo basi, mchango wa John kwenye kampuni hiyo lazima utakuwa mkubwa ukimlinganisha na Hemedi, kwa sababu John ana ukaribu zaidi na bosi wake na ana kiwango kikubwa cha imani juu yake ukimlinganisha na Hemedi.

ITAENDELEA...

Naomba mchango wako, wewe mwenzetu uzoefu wako ni upi juu ya kupata mtu Mwaminifu wa kufanya naye kazi au jambo fulani la msingi katika maisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wa kumuamini ni wewe mwenyewe.

Muamini wewe tu..na usimuamini mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unataka kuanzisha kampuni, bado utafanya kila kitu wewe? Cashier wewe, Hr wewe, Masoko wewe, mpaka Usafi wewe?
Maana Dhumuni la huu uzi ni kuambizana tufanyaje kumpata mtu wa kufanya naye kazi ikafanikiwa? Hata kama miaka kadhaa mpaka Business yenu inasimama!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna jambo jema kama kumpata mtu anaekuamini. mwanamke anaekubali kubeba ujauzito wako bila ndoa amekuamini sana, na hata ukimuelezea dreams zako anakusapoti kwa moyo wote. Mungu azidi kumtia nguvu huyu mwanamke, sijutii kuwa nae.
 
Hakuna jambo jema kama kumpata mtu anaekuamini. mwanamke anaekubali kubeba ujauzito wako bila ndoa amekuamini sana, na hata ukimuelezea dreams zako anakusapoti kwa moyo wote. Mungu azidi kumtia nguvu huyu mwanamke, sijutii kuwa nae.
Sawa braza,akija kukusaliti usisite pia kuja kutuhabarisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom