uaminifu katika ndoa.

Makene

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,475
282
wadau tufunguke kuhusu nani kati ya mume na mke anayesababisha kutoweka kwa uaminifu katika ndoa, ambazo tunazishuhudia zikiwekwa nadhiri za uaminifu kwa mbwembwe na matangazo ya kutosha.
Je kosa linaanza lini wakati wa uchumba, baada ya kuoana au baada ya miaka kupita?
Je walaumiwe walezi wao, au mawifi na mashemeji ndugu au ni marafiki zao?
Tujitahidi kuwa wakweli.
 
wadau tufunguke kuhusu nani kati ya mume na mke anayesababisha kutoweka kwa uaminifu katika ndoa, ambazo tunazishuhudia zikiwekwa nadhiri za uaminifu kwa mbwembwe na matangazo ya kutosha.
Je kosa linaanza lini wakati wa uchumba, baada ya kuoana au baada ya miaka kupita?
Je walaumiwe walezi wao, au mawifi na mashemeji ndugu au ni marafiki zao?
Tujitahidi kuwa wakweli.
Kosa linaanzia wakati wa uchumba, ndoa nyingi zimefungwa kutokana na uamsho wa tamaa na wala sio upendo wa dhati wa wanandoa.....Mwisho kile alichotamani kikiisha au kubadilika then ndoa imeisha.
 
Chanzo ni maudhi ndani ya ndoa baada ya kuchokana.
Maudhi yapi yanachangia, na nani mwanzilishi wa hayo maudhi, je ni wao au ndugu au marafiki?
Na je ni vitu gani vinavyotamaniwa na wenzi, ambavyo wakisha vipata hamu inakwisha, kiasi kwamba hawavitamani tena?
Na ni vitu gani huisha au kupotea baada ya wenzi kukaa pamoja?
 
Ni tamaa zaidi na kukosa subira kwa wakati.
Ni vitu gani vinavyotamaniwa, fedha, mali, tamaa ya vitu, tamaa ya ngono ya kawaida, isiyo ya kawaida?
Na je wanakosa subira kwa mambo yapi, ya maisha, ya kazi ya ndoa, au familia.
 
Ukishakuwa chini ya sheria wewe ni mtumwa wa sheria. Hakuna anayependa kuwa mtumwa!!!!! It is as simple as that. Tatizo watu wengi hawakumbuki hili. Huweka viapo bila kumaanisha. Wengine huoa au kuolewa kwa sababu umri umekwenda, wengine kwa mashinikizo ya wazazi/walezi/marafiki n.k Lakini ukweli unaouma ni kwamba watu wawili waliolelewa mazingira tofauti wenye mitizamo tofauti wenye uelewa tofauti wanapolazimishwa (maana wako chini ya sheria hata kama wanadhani wameridhia) kuishi pamoja, moto lazima uwake (japo muda na athari zaweza kutofautiana) kwamba unapenda ama hupendi.
 
Ni vitu gani vinavyotamaniwa, fedha, mali, tamaa ya vitu, tamaa ya ngono ya kawaida, isiyo ya kawaida?
Na je wanakosa subira kwa mambo yapi, ya maisha, ya kazi ya ndoa, au familia.


In blue hizi ni mojawapo ya njia zinazovunja nyumba nyingi (ndoa)
Subira ambayo wengi hukosa hasa wakati wa shida kama magonjwa, uzazi
Sasa ile maana ya shida na raha ndo inapotowekea hapo,
 
Ndoa nyingi uaminifu haupo!!!! Unadhihirishwa na wale amboa kwa kwa bahati kama umeajiriwa na mnasafiri say katika mkutano wa miki moja!!! Vituko utaviona!!!! Hakika hakuna uaminifu katika ndoa na wanaume wanaongoza kwa kukosa uaminifu!! Si cha hela, si cha magonjwa, si cha hata mke kugombana na mume!! Ni hulka ya kuchapata au kutembeza mzizi nje tu!! Wanawake wachache wana cheat nje ha hapo ni lazima utakuta kuna ka-loope hole toka kwa mume!!! Mume akiwa anampenda mke kwa dhati with all malovee (hata kama unaiba nje usionyeshe kamwe) nakuhakikishia mkeo hatakubali kutongozeka kirahisi unless kama ulikuwa umeoa kiruka njia toka awali,
 
Nawasoma wadau,
Kiukweli watu hawapendi kupoteza sehemu ya uhuru wao, na kwamba nadhiri huwekwa kama taratibu zilivyo zoeleka. Je ni muhimu kuzingatia watu wa nje zaidi kuliko ninyi wahusika wawili? Je ni busara kuhangaikia namna gani watawafurahisha wageni walioalikwa siku ya ndoa badala ya kuhangaikia muungano wanaouanzisha?
Je wadau waume ndiyo chanzo cha kukosa uaminifu?
Je wake viruka njia huzaliwa au hufanywa hivyo na mazingira?
Je watu wajiandae kwa bima zipi zitakazoweza kulinda ahadi na ndoa zao? Tuzidi kuchangia.
 
Mi naona nitamaa.msaliti daima macho yake yanakuwa hayajatulia.yani hakuna kinachompita
 
chanzo chake ni tamaa vitu are you sure tamaa is the reason? how can you explain wanawake wanao honga wanaume?
Je kuwa na ukwasi kwa wake ni sababu ya kuwafanya wakose uaminifu? Au yaweza kuwa wanatafuta kitu wanachokikosa toka kwa wenzi wao hivyo kutumia ukwasi wao au wa waume zao kutafuta kuridhishwa kiakili na kihisia!
 
Chanzo ni kuingiwa na tamaa ambazo hua ni chachu za kuvunjika kwa ndoa nyingi, pia kutokumridhisha mwenzi wako kwa penzi taaamu ambalo litamfanya kuifurahia ndoa na kutojutia maamuzi yake ya kufunga ndoa.
  • JINSI YA KUYAMUDU HAYO

  1. Maneno matamu ambayo huambatana na ukweli huifanya ndoa kudumu.
  2. Zawadi za hapa na pale ambazo zitaendelea kuiimarisha ndoa.
  3. Kufikishana kileleni na sio mmoja akishafika kileleni basi game linaisha.
  4. Kukubaliana na hali mliyonayo.
  5. Kuepuka marafiki wabaya ambao watapelekea kuivunja ndoa yenu.
 
::
Kuondoka kwa uaminifu kwa mwanaume huanzia machoni.
::
Kuondoka kwa uaminifu kwa mwanamke huanzia moyoni.
::
 
saudari, asante kwa kutoa msaada kwa yanayopaswa kufanyika, lugha inayofaa, zawadi hata ya maneno 'asante', 'nakupenda', kusoma undani wa mahitaji ya kingono ya yule mwingine, kutotamani makuu na kujimudu ninyi kama ninyi bila kuruhusu watu wa nje waingilie na kuhusika na mambo yenu hasa ya undani.
tetra, hivyo waume wakikosa uaminifu wataonyesha kwa kuwa nao karibu hasa kimaongezi ila wake itahitaji mbinu gani kuweza kuteka mawazo ya moyoni?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom