U20 na timu ya wanawake -lulu isiyojulikana na viongozi wa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

U20 na timu ya wanawake -lulu isiyojulikana na viongozi wa tanzania

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MTWA, Jul 14, 2010.

 1. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,026
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake, Charles Mkwasa, jana alitangaza kikosi chake cha wachezaji 25 kitakachoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake zitakazofanyika nchini Afrika Kusini kuanzia Oktoba. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkwasa alisema wachezaji nane wametokea katika timu zilizoshiriki mashindano ya UMISETA.
  ......."LAKINI sijaona kabisa msukumo wa viongozi wa mpira tanzania kwa timu hii wala ile ya U20. timu ya wakubwa tu ndo inaangaliwa licha ya kufanya madudu na kutofika mbali katika mashindano mengi".........

  Kabla ya kuanza kwa kambi hiyo Julai 17 timu hiyo itaondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Zanzibar kushuhudia uzinduzi wa filamu ya “Women Football” na kisha watarejea siku hiyo kwa ajili ya kambi.
  Akizungumzia wachezaji walioitwa kutoka katika mashindano ya UMISETA, Mkwasa alisema wengi wa wachezaji hao wanatoka mikoani na wameonyesha kiwango cha hali ya juu. “Wameonyesha kiwango cha hali ya juu na wanastahili kuwepo kwenye timu, ila kwa kuwa ni wanafunzi, kinachofanyika kwanza watakuja hapa Dar kwa majaribio na baadaye watarudi mikoani kwao kuendelea na shule na endapo tutaridhika na nao tunaweza kuwahamishia shule za hapa,” alisema Mkwasa.
  Alisema timu yake hiyo ambayo ilitarajiwa kuondoka nchini hivi karibuni kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mechi za kirafiki, wameahirisha safari hiyo ili kuwawezesha wachezaji kufanya usaili wa kupata pasi ya kwenda Marekani kwenye mechi nyingine za kirafiki.
  “Julai 21 tuna usaili wa kupata visa ya kwenda Marekani, kipindi ambacho tulitakiwa kuwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mechi za kirafiki... tumeahirisha kwa muda safari ya Afrika Kusini,” alisema.
  Mkwasa aliwataja wachezaji aliowateua kuwa ni, Sophia Mwasikili, Fatuma Omary Jawadu, Mwanaidi Tamba, Fatuma Swalehe, Fatuma Makwanya, Mwajuma Abdalah, Asha Rashid 'Mwalala', Ester Chabruma 'Lunyamila', Mwanahamisi Sharuwa, Pulkeria Charanji, na Hellen Tolla.
  Wengine ni Frodian Daudi, Zena Rashid, Eto Mlezi, Mary Masadi, Fatuma Salum, Maimuna Mkane, Fadhila Kigalawa, Neema Kuga, Evelyne Senkubo, Zahara Kaburure, Mwasiti Juma na Malyam Waziri.
  Mkwasa aliwataja wachezaji walioingia katika kikosi hicho ambao wamechaguliwa kutoka katika mashindano ya UMISETA na mikoa wanayotoka kwenye mabano kuwa ni, Mariam Azizi na Donisia Daniel (Dar), Semeni Abeid (Tanga) na Husna Ayoub (Bukoba).
  Wachezaji wengine ni, Amina Ali, Mwanaidi Salehe na Rehema Hussein (Kanda ya Mashariki) pamoja na Tatu Idd na Shamim Hamisi wote kutoka Kanda ya Kati.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Big up sana Twiga Stars (ndio jina lao?)
   
Loading...