U- turn ya wabunge waCCM

kituma12

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
301
122
Habari za mchana wanaJF

Kama kuna kitendo kinanikera kwa wabunge wangu waCCM (nasema wangu kwa sababu mimi pia ni mwanachama), ni hili la kuungana kwa vitu visivyo kuwa na maana. Wabunge wangu hawa wamekuwa wakiungana pindi mbunge wa upinzani anapotopewa bungeni au kunapo kuwa na hoja inayokugusa maslahi yao, kama kuna tukio lolote ambalo wabunge wa CCM wamewahi kuungana kwa maslahi ya taifa naomba kufahamishwa!

Maana mara ya mwisho waliponikatisha tamaa ni pale walipokataa rasimu ya Warioba (rasimu ya wananchi) na kujipitishia ya kwao.

Wabunge badilikeni hapo bungeni sio makazi ya milele siku moja na nyie mtakuwa mnaangalia bunge kama mimi tu kwenye TV.
 
Bora hata ukimwi utameza dawa za kurefusha maisha, sio ccm ambao wanapenda kuungana kupitisha mambo ya hovyo alafu, baadae wanaungana tena kuyapinga refer swala la Mchanga yaani hata hawaeleweki.
 
Angalia mkuu!Kama kweli ni mwana CCM ama hukijui vizuri chama chako na kama unakijua basi jiandae kuitwa MSALITI.
 
wamejitoa ufahamu tu kwa kumfurahisha fulani, wanajua sana wanachofanya ni kosa ila wanaungana kumfurhisha bwana yule aliekemea mbunge wa ccm kumpa mpinzani dakika za kuzungumza, nchi ina viongozi wa ajabu kweli kweli, ndio maana kila siku upumbavu unafanyika huko bungeni halafu wanakuja na hoja za uzalendo wanaposhtuka jua limezama.
 
Hakuna snakes wa hatari kama hizi namba, na sasa hivi wakiamka asubuhi wanaulizana baba ameamkaje leo ili waendane na miruzi ya baba!!!! Inahitaji moyo wa chuma kuwa kwenye mjengo mmoja wa hizi nambari!!!!!
 
Habari za mchana wanaJF

Kama kuna kitendo kinanikera kwa wabunge wangu waCCM (nasema wangu kwa sababu mimi pia ni mwanachama), ni hili la kuungana kwa vitu visivyo kuwa na maana. Wabunge wangu hawa wamekuwa wakiungana pindi mbunge wa upinzani anapotopewa bungeni au kunapo kuwa na hoja inayokugusa maslahi yao, kama kuna tukio lolote ambalo wabunge wa CCM wamewahi kuungana kwa maslahi ya taifa naomba kufahamishwa!

Maana mara ya mwisho waliponikatisha tamaa ni pale walipokataa rasimu ya Warioba (rasimu ya wananchi) na kujipitishia ya kwao.

Wabunge badilikeni hapo bungeni sio makazi ya milele siku moja na nyie mtakuwa mnaangalia bunge kama mimi tu kwenye TV.
Hujui Parliamentary Politics (Hujui Siasa za Bunge - Chama Dola Siku Zote Husimama na Serikali Yake)
 
Angalia mkuu!Kama kweli ni mwana CCM ama hukijui vizuri chama chako na kama unakijua basi jiandae kuitwa MSALITI.
Nahilo ndo kosa kubwa sana wa wabunge waCCM kuonekana wasaliti, unakuwaje msaliti wakati unatetea wananchi walio kupeleka bungeni na maslai ya taifa kwa ujumla??
 
Back
Top Bottom