Tz yetu, ukishindwa kwenye uchaguz unapewa ukuu wa mkoa au ubalozi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tz yetu, ukishindwa kwenye uchaguz unapewa ukuu wa mkoa au ubalozi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIDAYA, Dec 22, 2011.

 1. KIDAYA

  KIDAYA New Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  HIVI karibuni Rais Jakaya Kikwete amewateua mabalozi wapya wanane wakiwamo walikouwa mawaziri katika Serikali yake awamu ya kwanza na kuwapangia vituo vyao vya kazi.

  Walioteuliwa ni Phillip Marmo kuwa balozi nchini China, awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge.
  Marmo alianguka katika uchaguzi Jimboni Mbulu ambalo lilichukuliwa na mgombea wa Chadema, Mustafa Akunaay.

  Kwa upande wake, Dk Diodorus Kamala ambaye awali alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Nkenge amepangiwa kuwa balozi nchini Ubelgiji.

  Dk Kamala aliangushwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya chama chake, CCM

  Wengine ni Dk Batilda Salha Buriani ambaye aeteuliwa kuwa Balozi nchini Kenya ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).

  Katika uchaguzi wa mwaka jana, Dk Batilda aliangushwa na mgombea wa Chadema , Godbless Lema katika Jimbo la Arusha Mjini.

  Dk Ladislaus Komba ambaye ameteuliwa kuwa balozi nchini Uganda. Kabla ya hapo Dk Komba alikuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

  Pamoja na wengineo walioteuliwa, inaonyesha kuwa sasa Rais Kikwete ameamua kuwabeba viongozi ambao walishindwa kwenye uchaguzi mkuu kwanjia yoyote ile.

  Tuliona pia Rais aliwateua baadhi ya walioshindwa kwenye uchaguzi kuwa wakuu wa mikoa, wakiwamo Joel Bendera na na Mwantumu Mahiza.
  Kimsingi, haya ndikyo madhara ya madaraka makubwa aliyonayo rais kikatiba. Japo mwenyewe Rais Kikwete alipinga yeye siyo dikteta, lakini nafasi yake inamruhusu kuwa hivyo.
  Ndiyo maana tunadai mabadiliko ya Katiba ili uteuzi wa rais upitie Bungeni kuthibitishwa. Vinginevyo, uteuzi huo unaweza kutafsiriwa kuwa ni upendeleo wa rais kwa watu wake ambao hata kama wananchi kule wanakotoka hawawataki kwa kuwa walishindwa kuongoza, bado Rais atawabeba tu.
  Kwani hakuna watu wengine wakupewa hizo nafasi hadi wale wale walioongoza miaka nenda rudi ndiyo washike?
   
Loading...