Tz tunatumia mfumo gani wa matangazo ya tv?

Shaycas

JF-Expert Member
Feb 13, 2009
906
110
Habari zenu waungwana.
Napenda kujua Tz tunatumia mfumo gani wa matangazo ya tv kama PAL, NTSC etc.
Tafadhali naombeni msaada kwani kuna Smart Tv moja nataka kuchukua lakini wameniambia kuwa inatumia mfumo wa NTSC tu , hivyo niangalie kama system hiyo inafanyika huku kwetu kabla ya kuchukua.
Ahsante kwa mawazo na misaada.
 
Mkuu naunga nawe ili nami niibie ujuzi
maana teknolojia sio siri kwasasa ina kasi.
 
Ni Swali zuri sana na limekaa kitalaaam sana. Sio kila Mtu anayeweza kuyajua haya Mambo PAL/NTSC. NTSC hutumika sana na Nchi za Western kama Vile USA CANADA ect. kwa hapa Bongo Sisi huwa tunatumia PAL.

NTSC-National Television System Committee
PAL-
Phase Alternating Line
 
kwahiyo ukichukua ya NTSC haitofanya kazi?
 
Itafanya kazi lakini itakuwa na shida kwenye color

Nashukuru kwa majibu yako mazuri.
Shida ya rangi inakuwaje, yaani inakuwepo na kupotea au inakuwa black n white kwa picha zote na wakati wote?
 
Mfumo wa digital katika matangazo ya tv hauna maana yoyoye kwa mfumo huu yaani PAL, NTSC?
 
Nyie vipi. Hayo mambo ya VHS Tapes bado mnayo. Nowdays siyo ishu. Hizo multi system zilikwepo kitambo.
 
Wewe vipi, kwani zamani unapoangalia tv lazima upitishe kwenye VHS player? kwa lugha rahisi ni hivi radio freq za FM haziwezi sikika kwenye AM band ndivyo ilivyo kwa NTSC na PAL. PAL inashindwa ku-decode signal za NTSC na NTSC kwenda PAL haiwezekani.
 
Ni Swali zuri sana na limekaa kitalaaam sana. Sio kila Mtu anayeweza kuyajua haya Mambo PAL/NTSC. NTSC hutumika sana na Nchi za Western kama Vile USA CANADA ect. kwa hapa Bongo Sisi huwa tunatumia PAL.

NTSC-National Television System Committee
PAL-
Phase Alternating Line

Napenda watu makini kama ww,tunatakiwa kila mwenye utaalam awasaidie wananchi wenzake,Thanks Guru.
 
PAL Vs NTSC haina maana sana kwenye mfumo wa Digital hasa kwa upande wa rangi, ila kuna matatizo ya compatibility mengine kwenye framerate na kwenye resolution ya picha, pia inamater utakonnect vipi hiyo tv kwa composite cables za kizamani au kwa HDMI.

Na mwisho Digital Systems za Marekani na TZ hazipo compatible so TV yako haitaweza kunasa stesheni za Bongo mpaka utumie decoder.
Kwa kifupi bila kujua ni nini exactly unataka ufanye na specs za vifaa vyote ni vigumu kusema.
Nakushauri usinunue.
 
Kang Nashukuru kwa majibu yako mazuri sana. Njnachotaka kufanya ni kununua Samsung smart tv. Nilitaka kununua moja kwa moja toka Korea, ,wakaniambia kuwa TV zao ni ktk mfumo wa NTSC ni angalie kama zinafanya kazi huku kabla ya kuagiza.
Ahsante na naamini kuwa utanipa mwanga zaidi.
 
South Korea ni nchi inayotumia mfumo kama Marekani NTSC kwa analog na ATSC kwa Digital, na hata umeme wao ni tofauti kidogo.
Hivo kama hiyo TV inatengenezwa ka ajili ya soko la South Korea basi haitafaa. Unachotaka ni model inayotengenezwa kwa ajili ya Soko la Western Europe au bora zaidi soko la Africa. Nenda Mobile Phones | Televisions | Notebooks | Refrigeration - SAMSUNG AFRICA_EN hizo zitakuwa zanafaa Bongo
 
Ndg nimecheck tv system na kwamba ni
DTV Tuner/Digital Cable Tuner/Analog Tuner. Hapo nimeishiwa nguvu maana sijaelewa chochote zaidi ya kusoma tu.
Je system hiyo vp kwa hapa kwetu inafaa?
Samahani kwa usumbufu.
 
DTV Tuner ni Digital Tuner yaani ya kukamata channel za Digital, Standard za Digital ni tofauti kutegemea na nchi, hivyo Samsung wanatengeneza TV ile ile kasoro moja inasupport Digital system za Marekani nyingine inasupport system za Ulaya, nyingine za Bongo. Ndo maana unakuta model number zinatofautiana kidogo lakini TV inaonekana ni ile ile, system za ndani ni tofauti kidogo.

Same kwa analog tuner, ila hii haina maana sana maana analog hatutatumia Bongo tena.

Cha muhimu ni kuchagua model kwenye site ya Samsung niliyokupa, hii ni AFRICA site, na hakikisha unanunua model number hiyo hiyo ili kuepuka matatizo ukiileta bongo.
 
Back
Top Bottom