Tz,Kenya and Uganda enducation system, which one is better?

Mbeba Maono

Senior Member
Jun 24, 2008
108
7
Hivi jamani, naombeni mnieleweshe, Tanzania na Uganda, tunaingia University tukiwa form six, lakini Kenya wanaingia university wakiwa form four? Kuna usawa hapo? Kwanini system ya education in East Africa isiwe moja ili kuwe ne muingiliano wa wanafunzi? you know, kwamfano kwasaba, utakuwa wanafunzi wengi sana wa uganda wamejaa Tumaini university na Dar,lakini wakenya hawapo labda kwa Masters,ila sio undergraduate. tatizo ni kwamba, they don't qualify to be admitted here with a form four education. Kama kweli kuna malengo ya kuweka east Africa community au federation wanayosema, basi, kuna umuhimu haya mambo yaanze kushughulikiwa mapema.

hata hivyo, haiwezekani mtu aliyetoka chuo kikuu cha Nairobi awe sawa na aliyetoka chuo kikuu cha Kampala/makerere au Dar es salaam, kwasababu mmoja aliingia akiwa form four, wakati mwingine aliingia akiwa form six. mmojawapo hapo ataonekana ana quality nzuri zaidi kuliko yule wa Kenya? je hapo kuna ukweli wowote? kama sielewi kwa kuongea hivi, hebu mwenye uelewa anieleweshe basi.
 
Nilikuwa sijui kama kenya wanaingia universsty baada ya form four. ninachojua mimi tofauti ya Tanzania, Uganda na Kenya ni kwamba primary school kwao ni miaka nane na siyo saba kama Tz na Uganda. kama ndivyo ni kwamba Wakenya wanasoma miaka 12 ili kwenda university wakati Watanzania na Waganda ni miaka 13.
 
hata hivyo, haiwezekani mtu aliyetoka chuo kikuu cha Nairobi awe sawa na aliyetoka chuo kikuu cha Kampala/makerere au Dar es salaam, kwasababu mmoja aliingia akiwa form four, wakati mwingine aliingia akiwa form six.

Elimu anayepata mtu chuo kikuu, AKISHA KUBALIWA [ kummanisha anazo quolifications zinazohitajika kwa kile anacho tumai kukisomea ], haibagui ulikotoka wala uliko somea.

La kuelewa ni kwamba dunia nzima kuna mifumo tofauti ya elimu za msingi hadi secondary [Ona http://en.wikipedia.org/wiki/Twelfth_grade].

Mwanafunzi akisha fika kilele cha mfumo unaofuatwa kwao anaweza akajiunga na chuo kikuu chochote duniani bora awe na grades zinazohitajika.

Naamini kuna WaGanda, WaTZ, WaKenya, Wanaigeria etc Cornel, Stanford, MIT, Havard,Aberdeen, Cambridge, Edinburgh, Glasgow, Oxford, Moscow State University, Moscow Institute of Physics and Technology, Rostov State University, Nayanova University na vyuo vingine vingi duniani. Hii inamaana mifumo yote hii inakubalika ingawa tofauti, sikumaanisha moja ni duni kulinganishwa na nyingine.

Ninavyo elewa ni kwamba kila nchi ita adopt mfumo ambao kwao unawafaidi, mara nyingi chaguo hili linaongozwa na industries zilizoko. kwa mfano ni vyuo vingapi Africa vina major ya "Leisure Studies".
 
Mkuu, fanya utafiti wako wooote, angalia kama pale udsm kuna wanafunzi wa undergraduate from Kenya. hawapo. pia mimi ninao marafiki zangu wengi tu wa kenya, walipokuja hapa walishindwa kupokelewa, ikabidi wasome form five and form six kwanza kwa kuingia shule za hapa. ningeweza kukutajia majina kama ukipenda. wanaopokelewa hapa ni post graduate tuu. Nilishawai pia kutembelea function moja ilifanyika kwenye ubalozi wao hapa, jumuiya ya wanafunzi wa kenya(undergraduate waliosoma kwanza hapa form five na six na kukubaliwa) pamoja na watu wa masters wanao umoja wao. tatizo la kwanza kwenye malalamiko yao kwa selikali yao kwenye ubalozi huo lilikuwa difference kwenye mifumo ya elimu kwamba wakenya hawakubaliki. amini usiamini, fanya utafiti wako wote, wanakataliwa kabisa kuingia mpaka mtu awe form six. waganda kibao tunao, wakenya hamna. nilishawai kumwona mmoja tu amekubalika aliingia Habart kariuki unversity,kule mbezi beach, lakini sio vyuo vya selikali vya hapa tz.

Ninajivunia kuwa mtz....unaesema kuwa uganda wako juu kwa elimu, chuo chao kikuu cha makerere ambacho ndo cha kwanza, kina rank kwenye elfu nnee na zaidi duniani wakiwa na Nairobi, wakati Dar es salaam kidunia ina rank kwenye uelufu mbili na...., ukweli ni huo kwamba, wakenya undergraduate hawakubaliki. mimi nimeshuhudia kwa macho yangu. kama hauamini, unaweza kuniambia nikupe email yoyote ya mtu hapo wa kenya anaesoma hapa ili umuulize. wachache wanaosoma hapa ni wale ambao wamasoma kwanza hapa tz form five na six.

Ikumbukwe kuwa, wakenya wengi sana, na waganda wanapigania kusoma tz, kikubwa zaidi si kwaajili ya elimu yetu labda, ila kwasababu ya kiswahili. wengi wakisoma hapa wakirudi kwao huko huwa wanapata ujiko na soko kubwa sana kwasabu wanakuwa wanajua kiswahili cha kitz. hivyo wanapigana kufa na kupona ili wapate nafasi ya kuja kusoma tz kwenye kiswahili. so, selikali ya tz inatakiwa iwe inawaruhusu hata kama ni form four, yaani namaanisha kuwa hata kama wanapresent vyeti vya form four.....sheria ya vyuo vyetu vikuu inakataa lakini.
 
Back
Top Bottom