Tz ilihukumiwa kuilipa kampuni ya China us 21.5 mil. Hukumu ilitolewa na Msuluhishi m-Tz mwaka 2007!!

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,018
..Haya someni habari ya gazeti la serikali Daily News.

..Serikali imekuwa ikilimwa faini hata mashauri yanapoamuliwa na wasuluhishi wa Kitanzania.

..shauri la serikali vs China State Construction Engineering Corporation liliamuliwa hapahapa Tz, na msuluhishi alikuwa ni Mtanzania, na bado serikali ilishindwa.

..Tanzania ilihukumiwa kumlipa mkandarasi Mchina usd 21.5 million.

..tusifikiri kwamba msuluhishi wa kimataifa ana nongwa na Tanzania. hata huko kwa msuluhishi wa kimataifa, Tanzania huwakilishwa/hutetewa na mawakili toka nje ya nchi wenye uzoefu na utendaji wa mahakama hiyo.

..someni habari nzima hapa chini.

Daily News said:
THE decision by the Tanzania National Roads Agency (TanRoads) to terminate the 48.97bn/- road contract on 154km Kagoma-Lusahunga way in Kagera Region is likely to cost government billions of shillings, following recommendations given by the Disputes Review Expert, Prof. A. S. Mawenya.

In the determination he made on June 15, this year, after hearing the dispute between the parties, Prof. Mawenya said TanRoads wrongly expelled the contractor, China State Construction Engineering Corporation from the site, resulting in wrongful termination of the contract.

Prof Mawenya, therefore, has recommended that TanRoads should pay the contractor a total sum of 21,469,811 US Dollars. The state agency had terminated the contract it signed with the Chinese contractor in 2006 for poor performance and failure to comply with contractual obligations.

In his award, the dispute review expert said TanRoads would pay 15,617,492 US dollars as damages for wrongful termination of the contract and other 42,215.86 US dollars as finance costs, resulting from delayed advance payments.

According to Prof Mawenya, TanRoads would also pay 1,776,432.80 US dollars as reimbursement of customs duty and VAT if the contractor would not have pursued tax exemption independently with the Tanzania Revenue Authority and other 350,000 dollars towards cost of review.

Furthermore, the dispute review expert recommended that TanRoads pay the contractor 2,500,000 US dollars as balance of money for works executed until the date of termination and other 23,115 US dollars as his 50 per cent share of the expert's costs of service.

The said amount, Prof Mawenya said, would attract interest rate of three per cent per annum with effect from February 8, last year, the date of expulsion on the damages and costs awarded and from June 15, this year on the other payments awarded till date of payment in full.

It is stated that the Chinese construction firm signed the contract on March 13, 2006. The project was to be completed in 39 months, including the initial three months mobilization period. Commencement was April 21, 2006 and the project was expected to be completed by July 20, this year.

TanRoads appointed International Consultants and Technocrats Pvt Limited of New Delhi, India as the engineer to supervise the project. On June 7, 2007, the engineer served the contractor a default notice pointing out unsatisfactory performance.

Thereafter, on January 25, last year, TanRoads issued a 14 notice of expulsion to the contractor, stating that they had persistently neglected to comply wit its obligations under the contract, including failure to achieve average progress of five per cent per month.

The contractor allegedly failed to attain the average progress of seven per cent per month in order to catch up the lost time, instead it achieved only 1.5 per cent and failed to fully mobilize equipment needed for double shift working and to complete the mobilization of resources.

However, the Chinese contractor disputed the claims and, through its advocate Dilip Kesaria, took the matter to the Disputes Review Expert, as per the contract and sought his written recommendation on the matter.

cc BAK, Petro E. Mselewa , tindo, jingalao, TUJITEGEMEE, MTAZAMO, Pohamba, masopakyindi, Richard
 
Serikali ni ya hovyo sana.

Nimejiwazia namna inavyo wadai wanafunzi walio kua wanufaika wa mikopo ( HELSB ), wakichelewa kidogo riba hiyo juu kabisa, makato juu kabisaa, na mikwala juu kabisa hata kwa asie na kazi nae akarejeshe pesa.

Acha nayo ilipe iache siasa kwenye issue muhimu kama izi, tusije jikuta tumo shimoni wote
 
Kwa kweli kama tulilia bomu, tumepata bomu na kama kawaida tunao wajinga wanaoshangilia kulishika bomu bila kujua athari ya kufanya hivyo.

Safari hii sijui watamlaumu nani wakati madeni yanazidi kuongezeka kwa maamuzi ya kijinga ya kukurupuka hovyo kama vile hatuna akili.

Ishara zilionekana toka mapema kabisa lakini hatukuweza kugutuka kuepusha balaa...ukimuona mzazi mwenzako anasita kukuunga mkono, ujue kuna tatizo.
 
..ni vizuri tukaelimishana jinsi mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa mikataba ya biashara inavyofanya kazi.

..kwa uelewa wangu Tz inaposhtakiwa huku huteua mawakili wa kimataifa wenye uzoefu na mahakama hiyo kutuwakilisha.

..ni nina uhakika zipo kesi ambazo tumeshinda, na zipo ambazo tumeshindwa.

..kwa hiyo wale wanaodai mahakama hiyo ni ya wazungu au kifisadi wamelenga kuwapotosha waTz.

..labda mwanasheria wetu, ndugu yetu Petro E. Mselewa anaweza kutupa maelezo ya jinsi mahakama ya usuluhishi ya migogoro ya kimataifa inavyofanya kazi. Utaratibu mzima wa kushughulikia/kuamua mashauri ukoje.
 
Mkuu JokaKuu nashukuru kwa mualiko kwenye mjadala huu. Nitarejea.
 
..ni vizuri tukaelimishana jinsi mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa mikataba ya biashara inavyofanya kazi.

..kwa uelewa wangu Tz inaposhtakiwa huku huteua mawakili wa kimataifa wenye uzoefu na mahakama hiyo kutuwakilisha.

..ni nina uhakika zipo kesi ambazo tumeshinda, na zipo ambazo tumeshindwa.

..kwa hiyo wale wanaodai mahakama hiyo ni ya wazungu au kifisadi wamelenga kuwapotosha waTz.

..labda mwanasheria wetu, ndugu yetu Petro E. Mselewa anaweza kutupa maelezo ya jinsi mahakama ya usuluhishi ya migogoro ya kimataifa inavyofanya kazi. Utaratibu mzima wa kushughulikia/kuamua mashauri ukoje.
Kati ya kesi tulizoshindwa na tulizoshindwa, tulizoshindwa ni nyingi sababu sisi ndio tunaofanya unlawful termination kitu kinachotufanye tukose utetezi wa msingi sababu hua tunakiuka makunaliano tuliyokubaliana wenyewe...
 
..ni vizuri tukaelimishana jinsi mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa mikataba ya biashara inavyofanya kazi.

..kwa uelewa wangu Tz inaposhtakiwa huku huteua mawakili wa kimataifa wenye uzoefu na mahakama hiyo kutuwakilisha.

..ni nina uhakika zipo kesi ambazo tumeshinda, na zipo ambazo tumeshindwa.

..kwa hiyo wale wanaodai mahakama hiyo ni ya wazungu au kifisadi wamelenga kuwapotosha waTz.

..labda mwanasheria wetu, ndugu yetu Petro E. Mselewa anaweza kutupa maelezo ya jinsi mahakama ya usuluhishi ya migogoro ya kimataifa inavyofanya kazi. Utaratibu mzima wa kushughulikia/kuamua mashauri ukoje.
Mkuu hakuna mahakama inayosikiliza upande mmoja. Tunakumbuka ipo ile ya IPTL? kama sikosei ilipiga kambi Sheraton wakati huo. Tulipeleka mawakili kushindwa na tukashindwa

Tunashindwa kesi si kwasababu ya kukosa mawakili wenye uzoefu na wakimataifa
Tuna sababu kuu mbili au tatu zinazoplekea hali hiyo

1. Mawakili wanaweza kuwa sehemu ya 'shauri' kiaina

2. Wanaweza kushindwa kwasababu ya hoja inayotokana na fyongo zilizofanyika

3. Tuna watu wasioweza kujieleza au kuelezea na hilo hupelekea mikataba ya ajabu

4. Serikali kudhani ina haki zote au ina uwezo wa kufanya lolote hata mbele ya haki za watu

Katika point ya 3, umemsikia msemaji wa serikali akizungumzia ndege iliyozuiwa Canada. Nilitegemea angekuja na hoja za kwanini imezuiliwa na tunafanya nini au haki yetu ipo wapi au hata kama tumekwama ni wapi

Msemaji akageuza issue nzima kuwa tatizo la ''wapinzani''.
Kwamba tuna matatizo kwasababu wapinzani wamesema au wameungana nao.

Hata kama wameungana nao penye haki itaonekana tu
Kwamba wapinzani wangekaa kimya suala hilo lingeisha, huu kama si utani ni uzezeta uliokithiri

Watu wa namna hii wanawezaje kujenga hoja mbele ya mahakama za watu wenye weledi?

Point ya 4, kwavile serikali ina uwezo wa kukamata watu Ijumaa na kuwalaza mahabusu bila sababu, kuna mentality kwamba ina uwezo wa kufanya hivyo katika mikataba ya kimataifa. Kwa mentality hiyo hakuna anayeangalia sheria bali kufikiri tu vyombo vya dola vipo bila kujua vinamhusu nani havimhusu nani

JokaKuu ule uzi wa 'nani anadhibitiwa'' umekwenda wapi?
 
Kuna watendaji ndani ya serikali wanadhani wapo juu ya sheria.
Maamuzi wanayoyafanya ndio yanakuja kuwageuka.
 
Ziko tunazoshindwa kihalali!

Zipo tunazoshindwa kwa kuwa Mahakama hizo zimeundwa na mtandao wa mafisadi!

Zipo tunazoshindwa kwa kuwa mawakili wetu ni sehemu ya ufisadi!

Yupo mtanzania alikuwa anasimamia mgodi kule nzega ambao ulileta songombingo na hadi leo hawajalipa mrabaha sasa hivi anatoa huduma za usuluhishi (arbitration) unategemea ukimpa kesi kuhusu mgodi au madini mtashinda?
 
Sasa orodhesheni kesi tulizo shindwa na kushinda tuone tudaiwa na kudai ngapi.
Weka na uwezo wetu wa kulipa tuone kama tutaweza jamaa mmoja ameniambia deni ligawiwe kwa kila Mtz tuchange.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo hawa akina "Jingalao" wanasema kila serikali inaposhindwa kesi, kunakuwa na mkono wa akina Lissu!
 
Back
Top Bottom