Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
Katika kuokoa jahazi na kujaribu kuweka mwelekeo... ili tuweze kufocus..
Hapana; Resume ya Tyson ni ndefu zaidi ya hapo ingawa ni ile ya old guard. Ameshashika madaraka mbalimbali serikalini kuliko watu wengi sana walioko serikalini.
Elimu: Darasa la nane Nyambitilwa Middle School kati ya mwaka 1964 na 1967 hivi sina uhakika.
Kazi na Uzoefu:
- Kutoka Shule - 1969 : Bwana Maendeleo wa tarafa moja huko Ukerewe
- 1969 - 1972: Katibu mtendaji wa TANU wilaya ya Musoma
- 1970-1975: Mbunge wa Mwibara.
Ushindi wake katika kinyang'anyiro cha ubunge ule ulikuwa wa bahati sana na nadhani kuwa hapo ndipo nyota ya Tyson ilipoanza kung'aa. Alishindana na mtu mmoja aliyekuwa anajulikana kama Muyenjwa ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Tarafa nadhani ya Kenkombyo ambako alikuwa amenyanyasa watu sana. Kwa hiyo watu wa maeneo yale hawakutaka kumpigia Muyenjwa kura, na hivyo kumpa Tyson ambaye walikuwa hawamjui.- 1972-1974: Waziri mdogo wa Kilimo.
- 1974-1983: Mkuu wa Mkoa wa Mara
Hapa Tyson alipata nafasi ya kumwoa mtoto wa Chifu Wanzagi na hivyo akwa ni mkwe wa Nyerere. Aliondolewa pale kutokana na skendo kadhaa zikiwamo za kutumia madaraka yake kuvuruga uchaguzi wa ubunge wa jimbo la Musoma mwaka 1980, na matumizi mabaya ya nafasi yake kujipatia huduma kutoka kiwanda cha MUTEX.- 1983-1984: Kazi Maalum Wizara ya Mambo ya Nje.
- 1984-1985: Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania huko Marekani, Washington DC.
Inasemekena katika kipindi hiki alijiendeleza kielimu na kujipatia digrii kadhaa za uzamili za utawala, uchumi na ushirikiano wa kimataifa: Master of Public Administration, Master of International Relations, na Master of Economic Planning.- 1985-1990: Mbunge wa Bunda.
Ubunge ule nao aliupata kinamna kwa vile kulikuwa na mvutano kati ya Mwenyekiti wa CCM wa Bunda (nadhani akiitwa Mnubi Salama) na Mbunge wa Bunda wakati huo Mugeta. Mwenyekiti akaendesha kampeini mapema kabisa kuwa watu wasimpigie kura Mugeta kwa sababu alishindwa kuleta maendeleo kwanye jimbo la Bunda. Watu wakawa wamekubaliana na mwenyekiti kuwa Mbunge yule ang'olewe. Lakini walikuwa hawajui kuwa nani atapambana naye. Ilipofika mwezi July 1985, Wassira akatangaza kugombea Bunda, ndipo Mwenyekiti aliposhtuka na kujaribu ku-reverse kampeini zake against Mugeta lakini ilikuwa too late.- 1985-1990: Waziri mdogo wa Tawala za Mikoa, na Serikali za Mitaa; Waziri wa Kilimo, Ushirika, Masoko.
Hapa sina uhakika na majina ya wizara alizoongoza ila najua mojawapo ilihusika pia na ushirika, ambapo alitumia madaraka yale kumfukuza kazi Meneja wa Bodi ya Pamba na kumteua kaka yake George Wassira kuikaimu indefinitely. Kipindi hicho aliachana na binti wa Wanzagi na kumwoa dada yake na Waryoba ambaye alikuwa waziri mkuu.- 1990-1994: Mkuu wa Mkoa wa Pwani:
Kipindi hicho hakuombea ubunge wa Bunda ili kumpisha Waryoba. Badala yake akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa nadhani wa Pwani. Inawezekana alihamishiwa mikoa kadhaa ila kipindi cha pili cha utawala wa Mwinyi, Bwana Tyson hakuwa waziri. Ninadhani kuwa katika mabadiliko ya serikali ya mwaka 1994 ambapo Msuya alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu badala ya Malecela, huyu tyson alipotenza nafasi yake ya ukuu wa mkoa; hata hivyo sina uhakika sawasawa.- 1995-1997: Mbunge wa Bunda.
Kwenye uchaguzi huo alienguliwa kwenye primaries za CCM ambapo walimpitisha Waryoba aliyekuwa incumbent ; Tyson akaamua kujiunga na NCCR-Mageuzi ambapo alitwaa kiti kile. Hata hivyo kwa vile alikuwa amecheza faulo nyingi sana kwenye kampeini za uchaguzi ule kama ilivyo kawaida yake, Mahakama Kuu ilitengua ushindi huo na kumzuia kugombea kwa miaka mitano. Kwa hiyo mwaka 2000 hakugombea hadi mwaka 2005 alipogombea tena.- 2005-Todate: Mbunge wa Bunda na Waziri kwenye awamu ya nne. Ameshaongoza Wizara mbili.