Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,215
- 21,392
Bondia wa zamani wa ujizo wa juu duniani Mike Tyson, amejikuta akipata mpenzi wake nchini Uingereza.
Mwandani huyo wa Mike anaitwa Aisleyne Horgan-Wallace ambae aliwahi kushiriki mashindano ya Big Brother yanayoandaliwa na kituo cha televisheni cha channel 4 cha Uingereza na kushika nafasi ya tatu mwaka 2006.
Tyson mwenye umri wa miaka 41 akiwa na mtoto Aisleyne ndani ya gari ya kukodi akiwa ameshikilia ua la Rose alilolinunua kutoka kwa mchuuzi wa mtaani.Hio ni baada ya kutoka katika ukumbi wa starehe uitwao China White,eneo la Soho katikati ya jiji la London, ikiwa ni saa tisa unusu asubuhi ya Jumapili.
Tyson si mgeni sana na Uingereza,huwa anatembelea London kila mara kushiriki katika vipindi viitwavyo "Talk Show" ambavyo unaweza kuona kupitia katika tovuti yenye link ifuatayo:
http://www.tysontalk.com/index.html
Tovuti hii hushirikiana na radio ya Talk Sport cha Uingereza.