Typing errors za smartphones

mangyi

JF-Expert Member
May 16, 2018
718
867
Salamuni wakuu. Ase kuna kitu flani huwa kinatokea sana kwenye hizi smartphones zetu na sometimes kinapelekea mtu kujikuta anajicheka, sometimes kupelekea kuomba msamaha kwa maneno mengi ili ueleweke na uliyemtumia ujumbe na sometimes inapelekea pia wewe kushushwa heshima, n.k. Hii kitu ni TYPING ERRORS BHANA.

Nimepita pita kwenye uzi mmoja, nimekutana na hii:-

"Wao wanasema saa nne asubuhi ndo renewal imepita wakati kwa ufahamu wangu muda renewal inaitwa ndo muda ule uke uliojiunga mara ya mwisho."

Hii inasentensi inayoeleweka ila haikukusudiwa kuwa hivyo. Badala ya ULE ULE imekuja ULE UKE

Hebu tujuze ni TYPING ERROR gani umewah kuiandika na ikaleta sentensi inayoeleweka lakini halikua kusudio lako kuandika hivyo na ikawa msala.

KUONGEZEA

Au kwenye zile isue za kutuma tuma picha za ajabu kwa washkaji, ukajikuta umetuma picha kwa mtu mnayeheshimiana au kwenye group flani serious.

2020
 
Mimi bwana, ile nashare video group flani la WhatsApp nikakosea nikashare sehemu mbili yaani wakati wa kuchek bahati mbaya nikaclick na sehemu nisio kusudia.

Kuja kucheki nimetuma na group jingine. Fasta Fasta nika delete. Dah si nikadelete for me badala ya for everyone.

Nilitamani nileft. Ile aibu.
 
Alafu unakuta watu walikua active kuchat ghafla wanastop

2020
 
Mnaomiliki Smartphones njooni huku ili na sie wengine tupate kujifunza kutoka kwenu
 
Kukosea siyo kwenye smartphone pekeyake bana...

Siunajua simu ndogo pale kwenye button ya namba 6 kuna herufi "mno"

Basi kujidai unajua kuchati fastafasta unataka uandike "kuna wawili tu" unajikuta umeandika "**** wawili tu" halafu ni majibu ulikuwa unarudisha kwa mshua baada ya kukuuliza "huko ulipo kuna wangapi mpaka sasa?"

Ndomana me sitakagi kujizoesha kuwasiliana kwa kutumia sms kwa watu wa heshima... hata wakinitumiaga sms basi mimi ni lazima nipige simu tu kwakweli tukumbane kwenye sababu nyingine tu za makosa ya kawaida lakini siyo humo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa nachati na binti yangu kumsaidia kujibu hoja fulani. Sentensi iliyokusudiwa ilikuwa "ukiandika ndiyo yanahitajika maelezo ya kina" hapo kwenye neno kina likajiandikak**a.
Aisee, nilihangaika kusimamisha sms haikuwezekana. Nikaanza kuichukia simu.
Kila mmoja akawa kimya. Niliwaza mtoto atanielewaje? Nitarudije home? Halafu tulikuwa tunakaa wawili tu. Baadaye aliendelea na kuchati, nikamjibu niko busy asubiri nimalize kazi nitampigia. Mawasiliano yaliendelea bila mjadala wa lile kosa. Nikikumbuka huwa najisikia aibu kwa mwanangu.
 
Mimi bwana, ile nashare video group flani la WhatsApp nikakosea nikashare sehemu mbili yaani wakati wa kuchek bahati mbaya nikaclick na sehemu nisio kusudia.

Kuja kucheki nimetuma na group jingine. Fasta Fasta nika delete. Dah si nikadelete for me badala ya for everyone.

Nilitamani nileft. Ile aibu.
hiyo delete for me imenikuta majuzi tu. Bahati yangu hakikuwa kitu kibaya.
Ninachoshukuru mimi huwa nina sheria zangu sikai na picha au video za ajabu kwenye simu yangu.
 
Nilikuwa nachati na binti yangu kumsaidia kujibu hoja fulani. Sentensi iliyokusudiwa ilikuwa "ukiandika ndiyo yanahitajika maelezo ya kina" hapo kwenye neno kina likajiandikak**a.
Aisee, nilihangaika kusimamisha sms haikuwezekana. Nikaanza kuichukia simu.
Kila mmoja akawa kimya. Niliwaza mtoto atanielewaje? Nitarudije home? Halafu tulikuwa tunakaa wawili tu. Baadaye aliendelea na kuchati, nikamjibu niko busy asubiri nimalize kazi nitampigia. Mawasiliano yaliendelea bila mjadala wa lile kosa. Nikikumbuka huwa najisikia aibu kwa mwanangu.
hatar sana aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom