Type of suprise for engegement ring | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Type of suprise for engegement ring

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by CM, May 28, 2009.

 1. C

  CM Member

  #1
  May 28, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salamu waheshimiwa na wachangia hoja katika JAMII FORUM na kwingineko.
  Kwa kifupi nategemea kumvisha mchumba wangu pete ya uchumba hivi karibu kwa hiyo naomba mnisaidie hizo aina/tendo hilo kwa ajili ya kumfanya na yeye ashangazwe na hilo jambo maana si wote huwa wanavalishwa pete ya uchumba.
  Nawashukuru sana na nnamategemeo mtanisaidia kwa hilo
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,916
  Likes Received: 214
  Trophy Points: 160
  Jaribu kumvalisha hiyo pete akiwa usingizini, kesho yake akiamka utamwona atakavyokuwa kwenye mood...

  Ila uwe na uhakika kweli kama atafurahia hiyo surprise yako, manake anaweza kubaki anakushangaa kwa kukurupuka.
   
 3. C

  CM Member

  #3
  May 29, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa wazo lako sio baya but tatizo hapo ni mtoto wa geti kali so hilo zoezi linaugumu wake. Yaani nachotaka kukifanya kisiwe siri kwa watu baki ila kwake ndio kiwe siri.

  Wadau naombeni mnisaidie maana siku ndizo hizo zina karibia, Na pete iko kwa sonara
   
 4. C

  CM Member

  #4
  Jun 1, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani wana Jamii naombeni mnisaidie ili niweze kumaliza zoezi hili.
  mwezangu ananiambia pete ya uchumba huwa inavalishwa kwa kushtukiziwa na sio inavalishwa kama pete ya ndoa au nyinginezo. Nimejaribu kumuomba na yeye atafute ili tuchague moa wapo. Na mimi nemeona ngoja nitafute kwa wanajamii wenzangu, Kwa kifupi nategemea kumvisha mchumba wangu pete ya uchumba hivi karibu kwa hiyo naomba mnisaidie hizo aina/tendo hilo kwa ajili ya kumfanya na yeye ashangazwe na hilo jambo maana si wote huwa wanavalishwa pete ya uchumba.
  Nawashukuru sana na nnamategemeo mtanisaidia kwa hilo
   
 5. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Kumbe mmeshaongelea tayari, hapo hakuna cha surprise kwa sababu anaitarajia tayari. Unaweza mvisha siku unatayoenda kutoa mahari kwako.
   
 6. C

  CM Member

  #6
  Jun 2, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nilikuwa nawazo hilo but kwa stail ipi? Namwita mbele za watu au tunaenda kona au inakuwaje hapo mtu wangu?
   
 7. GP

  GP JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  UMESHACHEMSHA HAPO, THEN ITS NOT A SURPRISE:D

  ila unaweza kufanya kama hivi:
  hapo labda subiri siku kadhaa zipite then mvishe, ila ukitaka ilete maana ya kumsuprise, then andaa sehemu moja cool sana, tafuta washikaji zako kadhaa, msizidi watu jumla 10 ambao yeye pia anawafahamu, ukiweza na mashosti wake 2 wa ukweli lakini hakikisha umewaambia kwamba THAT IS A SURPRISE TO THEIR FRIEND sio wamwambie tena itakua wameharibu.
  kisha hiyo siku mwombe mtoke kidogo kimtindo, wakati huo hao watu unawaambia wakae sehemu tofauti, mida ya jioni ndo mizuri, then ninyi mkishakaa hapo, wanakuja mmoja mmoja kwa time yake kama walikua hawajui kinachoendelea, then mnapiga stori kimtindo kisha unamwita mbele unamuintroduce unavyoweza kisha unamvisha pete wakati huo uwe umeshamwabia afumbe macho (ila nahisi anaweza akastukia coz ulimshamdokezea, thats the mistake)
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Aisee in that case mmeshaiweka surprise kwenye wakati mgumu, inaweza isiwe surprise tena.
  Sasa unachoweza kufanya ni hivi:
  mwambie rafiki yako au mtu mwingine yeyote aandae kashughuli kama birthday party etc. Then kwenye hiyo party katikati watoe nafasi kwa watu kutoa salam za birthday.wacha mtu wa kwanza atoe salam, then wa pili wewe kuwa kama mtu wa tatu hivi kuomba microphone. ukipewa microphone toa salam za birthday kama kawaida then mwishoni chomekea ishu ya kumvalisha pete mchumba wako. Wakati unapewa mike usiwe karibu naye sana, kuwa na umbali kama wa mita tano hivi toka aliko kakaa au kusimama yeye. Then wakati unatoa salam za birthday wangalie watu wote na usiwe nurvous. ukifikia hatua ya kumuomba umvishe pete inabidi umuangalie machoni na usubiri response yake.
  Mtu anayeandaa hiyo party ni vizuri awe mtu ambaye mchumba wako hamfahamu, ili asiweze kuhisi kuwa ni mchongo. Nyinyi muende kama mmealikwa tu.Na ni vizuri umwambie just a day or a few hours before the party kuwa kuna ishu ya party, inabidi u act kama huna ties zozote na hiyo party.
  Kazi kwako sasa jibaba,
  By the way... isije ikawa mchumba wako naye ni member wa JF, itakuwa zinga la movie la kihindi!!!!
   
 9. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Jamani hizi za siku hizi kali. Enzi zetu unaenda mbele ya wazazi mnakubaliana, mahari na mambo mengine. Then mambo ya pete yanabaki kwenu, wengi walikuwa hawavalishwi pete za uchumba ni ya ndoa tu. Siku hizi binti bila pete ya kito cha thamani du utaharibu, ni lazima. Enzi hio hata hela ya kununulia pete ilikuwa ni issue, maana mshahara ni kidogo. Ila as time went on mamsapu nilimvisha pete ya uchumba tulivyofanya aniversary yetu ya 20 years of marriage, and it was a ring of her choice with an expensive stone. Nilifurahi maana ningekuwa nimemvalisha huko nyuma isingekuwa ni pete ya thamani sana. Kwa kuwa nilikuwa nimeshamwambia kuwa nitamvalisha engagement-aniversary ring haikuwa ni suprise, ila alifurahi sana maana, alithaminika zaidi, mimi nianavyo. Na wewe kwa kuwa anajua unamvalisha pete siyo suprise, pengine suprise itakuwa the kind of pose.

  Nafurahi umefanya uamuzi mzuri wa kumvisha pete mchumba wako. It adds value to a relationship!!!
   
 10. dmaujanja1

  dmaujanja1 JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ZeMacopolo liIdea nimelipenda sana da!!!!. leta option nyingine kaka.
  kaka CM chukua hiyo mzee.
   
 11. dmaujanja1

  dmaujanja1 JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ZeMacopolo liIdea nimelipenda sana da!!!!. leta option nyingine kaka.
  kaka CM chukua hiyo mzee.
   
 12. C

  CM Member

  #12
  Jun 2, 2009
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru sana kwa kunipa ushauri wenu. Naomba msubiri nitawaeleza zoezi hilo liliendaje? Ila nitawakaribisha kwenye harusi naomba mnipe subira kidogo.

  AVACHE SANA
   
Loading...