Kuna madaktari wawili walizama katika bwawa lililopo katika maporomoko ya maji pale Sanje Water falls- Kilombero siku ya Jumamosi (April 11th, 2009). Madaktari hao ni walimu katika chuo cha Tanzania Training Centre for International Health (TTCIH) kilichopo Ifakara. Madaktari hao (marehemu Dr Alute na Dr Mujuni) walikwenda sehemu hiyo ya kitalii wakiwa na wenzao wawili lakini mmoja wao alishindwa kufika katika kilima hicho na hivyo kumuomba Guide amsindikize arudi na wenzake watatu wakaenda bila ya Guide. Walipofika kwenye bwawa lililopo kwenye maporomoko hayo mmoja alienda kwenye maji na kutaka apigwe picha na baada ya kupigwa picha mpiga picha alimuambia kuwa picha yake ilikuwa nzuri sana hivyo kwa hamasa wakati anataka kukimbilia kuiona picha yake akateleza na kusombwa na maji kuelekea sehemu ambako kuna maji yenye pressure kali yanayoelekea kwenye mapango. Mwenzake aliyekuwa anampiga picha alipotaka kwenda kumuokoa naye akasombwa na maji na yule wa tatu akakimbia kurudi walikotoka kuomba msaada.
Jitihada za kupata miili ya marehemu hazikufanikiwa hadi leo baada ya wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikosi cha Navy kuwasili na kufanikiwa kuyatoa maiti baada ya kukaa majini kwa muda wa takriban siku nne. Miili yao imeletwa St. Francis Designated District Hospital around saa kumi jioni hii.
Tukio hili linatoa fundisho kuwa ni muhimu kuchukua tahadhari tunapokwenda sehemu za hatari kama hizo. Ni muhimu pia kuwa na Guide na kufuata maelekezo yao.
Mungu aziweke roho za marehemu mahala pema peponi
AMEN