Two faces of the same coin! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Two faces of the same coin!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shinto, May 7, 2011.

 1. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimetafakari kwa makini juu ya maamuzi ya kamati kuu ya CDM kumshawishi Mbowe akiuzie chama magari chakavu, nimeona issue hii inashabihiana sana na lile jaribio la serikali kununua mitambo ya DOWANS! Hoja ya utetezi inayotolewa na CDM ni kuwa hayo magari yalichakaa katika shughuli za chama, haitofautiani na fact kwamba mitambo ya DOWANS ilikuja mipya tukaichakaza kwenye shughuli za serikali! Kichekesho wale waliopinga ununuzi wa mitambo ya DOWANS sasa wanaunga mkono ununuzi wa magari ya Mbowe! Ironically Zitto aliunga mkono ununuzi wa mitambo ya DOWANS sasa anapinga ununuzi wa magari ya Mbowe!
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Duh, watu mna kumbukumbu. Huo ni usanii wa kisiasa. Wanasiasa ni vigeugeu leo wanasema hivi kesho vile. Kununua magari chakavu tena toka kwa mwenyekiti ni ufisadi hakuna lugha nyingine zaidi ya hiyo. Afadhali hata mitambo ya DOWANS ilikuja kwa madhumuni ya umeme lakini magari ya Mbowe tunaambiwa yalikuja kwa ajili ya Biashara zake baadaye akayatoa yasaidie chama katika kampeni, ameona ruzuku imekuwa kubwa na pesa zipo anataka sasa Chama kiyanunue. Si alijitolea kukisaidia Chama sasa ya nini tena anasema yanunuliwe? Najua kuna watu walijitolea magari yao kwa ajili ya kampeni na yakatumika kwelikweli wengine walijitolea pikipiki zao kwa ajili ya Chama nazo zikachakaa; kwa hiyo ina maana nao wakiuzie chama hayo magari na pikipiki zao chakavu, si zimechakaa kwa shughuli za chama?
   
 3. c

  chama JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ufisadi ni ufisadi hauna kabila wala rangi; wanachadema hebu tupeni ufanunuzi kumbe nyie mnae Rostam? Tulisema siku nyingi Mbowe si mwanasiasa anachofuta ni maslahi yake kibiashara, leo ameanza na magari tukiwapa nchi mtaimaliza? Mkumbusheni Dr. Slaa aliongelee hili kwenye mikutano yake .

  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 4. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Wacha nikujibu tu ndugu yangu labda ni kuwa huelewwi au uwezo wako wa kufikiri umeishia hapo!
  tafakari kwanza haya..
  1. Ni nini shughuli za serekali na ni nini shughuli za chama,

  baada ya hapo sasa ni kuwa MBOWE alinunua magari kwa shughuli zake kwa hela yake kwa kuwa kulikuwa na uchaguzi akamua kutoa magari yatumike kwenye kampeni, Dowasn walikodisha mitambo kwa hela zetu toka BOT na wakatuuzia umeme na tuakawalipa wakachukua chao.
  Pia DOWANS walikuwa ni wafnay biashhara na sio shughuli za serekali.
   
 5. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #5
  May 8, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  watu wenye hoja dhaifu hua wanachomoa katawi tu kwenye maada na kushambulia mithili ya kiwavi jeshi! baada ya yote hayo then what
   
 6. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Acheni kutufanya wenzenu hatuna akili, kwenye sakata hili Mbowe ndiye anayeuza magari na Mbowe ndiye anayenunua! Huo ni ufisadi first degree! Iteni ufisadi ufisadi tuu, uwe wa kihindi au wa kichaga!
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hata Mbowe ni mfanya biashara, unachotetea nini?, kweli kupenda upofu!.
   
 8. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwa mtindo huu ukombozi Tanzania uko mbali. Hawa jamaa vinara wa kujifanya wanapinga ufisadi, wanavumilia na kutetea upuuzi huu?
   
 9. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #9
  May 9, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hakika ufisadi ni ufisadi tu na uitwe hivyo na siyo kupindisha. Kuna mgombea udiwani wa CHADEMA ambaye namjua alitumia pikipiki yake kupiga kampeni wakati wa uchaguzi na pikipiki ikafilia mbali na bahati mbay ahakufanikiwa kupata udiwani. Kwa sasa yuko hohe hahe, basi kama Chama kinanunua vitu chakavu vilivyotumika kwenye kampeni naomba tumuokoe na huyu ndugu yetu.
   
 10. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa ni waajabu sana leo nimeona kwenye magazeti wanamtaka Mwakyembe ajiuzulu kwa sababu kuna mtuhumiwa wao wa ufisadi kapewa cheo serikalini! Nikajiuliza, Mwakyembe akikubali watamliba mshahara na marupurupu ya unaibu waziri kama wanavyofanya kwa SLAA?
   
Loading...