Twiga yaikung'uta Ethiopia 3-1

PingPong

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
926
160
Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imeifunga timu ya taifa ya Ethiopia kwa mabao matatu kwa moja.
Mchezo huo umefanyika mjini Addis Ababa.
Mwenyekiti wa chama cha soka cha wanawake nchini Tanzania, Lina Mhando amekiambia kipindi cha Michezo na Wachezaji cha BBC kuwa goli la kwanza limefungwa na Esther Chamburuma.
Amesema bao la pili limefungwa na Mwanahamisi Omari la tatu kufungwa na Asha Rashid.
Timu hizo zitakutana tena wiki mbili zijazo, katika mechi itakayochezwa mjini Dar es Salaam.
Atakayeibuka mshindi baada ya mechi hizo mbili atacheza na Eritrea, kufuatia timu ya Kenya kuamua kujiondoa katika mechi hizo za kufuzu.

source: BBCswahili.com
 
Hongereni lakni sijajua utarstibu. Ukimkojolea mtu si hadi akunyie ndo atakua amekushinda
 
afadhali ya hawa dada zetu wanafanya kitu kinachooneka, sio wakina Nsajigwa kila siku mambo yaleyale, hongereni sana twiga stars.
 
Kwa kweli wamujitahidi sana inawa kimchezo walizidiwa katika kipindi cha kwana dakika 15 za mwanzo.wamijitahidi sana hawa twiga.Hilo goli la ethiopia ni la kupewa maana hata hao wenyewe wanasema ni la kupewa na refa.Nachoweza kusema tuna kpa mzuri sana sana.
 
Back
Top Bottom