Twiga stars walala 3-0 kwa wacameroon

Mtade_Halisi

Member
Feb 23, 2008
28
0
Timu soka ya Taifa ya wanawake a.k.a Twiga stars jioni hii imelala 3-0 mbele ya wadada wa cameroon.hadi Kipindi cha kwanza Cameroon walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0. Mabao mengine mawili yalipatikana kipindi cha pili hivyo kuiweka Twiga stars katika wakati mgumu kufuzu mashindano ya Africa.Twiga stars wanahitaji ushindi wa mabao 4-0 ili kuweza kufuzu watakapopambana na wacameroon hao kule Younde kwenye ngwe ya marudiano. Pata picha toka taifa kwa mujibu wa Michuzi blog...
 

Attachments

  • cameronvstwiga.JPG
    cameronvstwiga.JPG
    102.7 KB · Views: 84
Leo nimewaona hawa dada Ikulu wakitiwa moyo!

Sasa may be Cameroon basi wasiende --watafungwa mno bao nyingi na ni kupoteza nauli bure!
 
Akizungumza na Lete RAHA, Mkwasa alisema jijini katikati ya wiki akiwa amekata tamaa kuwa anawasubiri wapinzani wao tu, na ameridhika na mechi za kirafiki na timu za shule za michezo na timu za kujifurahisha.

``Tumeridhika maana hatuwezi kulazimisha kupatikana kwa mechi, na ninaamini hizi mechi tulizocheza na vijana wadogo wa academy zitatusaidia kwa kuwa zimetuweka fiti na hata mimi nimerekebisha baadhi ya makosa niliyokuwa nimeyaona mwanzo,``alisema Mkwasa ambaye ana uzoefu mkubwa katika soka ya wanaume.

Lete Raha
2008-02-17 09:34:03
By Mwandishi Wetu
.

Cameroon ni moja kati ya timu mbili za football ya wanawake, zilizo bora kabisa ktk bara la Africa, nyingine ni Nigeria. hivyo isitukatishe tamaa, kwani kinachotakiwa ni maandalizi mazuri. hata Mkwasa (coach) alishakata tamaa mapema kutokana na uduni wa maandalizi. suala la kuitwa ikulu halina mchango wa maana kiufundi, maandalizi makini ndiyo muhimu.
 
Kocha naye maneno meeengi! Halafu kwa visingizio anaongoza. Mie nadhani ili kuokoa hasara na kipigo cha aibu kwa Taifa, huko Yaunde bora wasiende; tusubiri kulipa faini tu basi.
 
Back
Top Bottom