Twiga kuibiwa na kupelekwa nje kupitia kia kwanini isiwe ni ufisadi mbaya zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Twiga kuibiwa na kupelekwa nje kupitia kia kwanini isiwe ni ufisadi mbaya zaidi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by GJ Mwanakatwe, Apr 20, 2011.

 1. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna taarifa kwamba twiga wanne walisafirishwa kinyemela kupitia uwanja wa ndege wa KIA wiki mbili zilizopita kwenda ughaibuni.Hizi habari zinashangaza sana,yaani twiga walivyowakubwa wapitishwe KIA bila kuonekana na vyombo vya usalama uwanjani hapo? haiwezekani hata kidogo. Hii inaonekana kuna mtandao mrefu wa wizi wa maliasili za nchi, na huu ni ufisadi mbaya kuliko mingine kwa kuwa wanyama hao na wengine watakwisha halafu tutakosa mapato, ni afadhali waibe fedha tutapata fedha nyingine kuliko kuiba wanyama wetu, maana sasa itakuwa wanatuibia mtaji.Ni muhimu suala hili lifuatiliwe kwa karibu na wote walihusika wachukuliwe hatua kali za kisheria.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Oyaaaaaa,amka, acha kuota ndoto za mchana. Hakuna wizi hapa: ni biashara huria+coruption.
   
 3. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  this is really shameful from GAMA

  If I had a gun....:A S clock:
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hivi ndivyo munavyojidanganya, kama unajua agreements na regulation za kusafirisha wanyama (wildlife) huwezi hata siku moja ukasema mnyama wa porini anaweza kuibiwa na akasafirishwa crossborder kwa kutumia public transport. Elewa mambo ya "CITES" ambapo entry na exit zote zina zoosanitary inspectors ambao hapaswa ku-endorse exit na entry ya mnyama. Pia unapaswa kujua kuwa bei ya mnyama wa porini haifikii hata bei ya ng'ombe na vibari vya kuchua na kubeba si big deal. Kwa hayo machache niliyokueleza nakuonea huruma kwa kutumia "DOWN STAIRS" kujadiri hoja hapa janvini. Kwa kifupi jukwaa hili unalipaka sheet.
   
 5. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  sijui unaishi dunia ya ngapi ndugu na vibali vyako
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Amini usiamini magari ya ofisi ya waziri mkuu STK ndio hubeba nyara za nchi toka vijijini kama tunduru kuja dar kwa wachina!wenye biashara hizo ni wahindi na waarabu wenye kufadhili vilabu vikubwa vya mpira hapa nchini!sasa wewe waongea habari ya vibali.muulize mrema ile dhahabu aliyoikamata airport ilikua na vibali?na akaiachia.ndipo neno vigogo lilipoanzia
   
 7. M

  Makanyagio Senior Member

  #7
  Apr 20, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ama kweli hata watanzania tutauzwa bei chini ya ng'ombe
   
 8. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hii huwa inaniuma sana , ukiangalia Mnyama kama twiga ni aghalabu sana kupatikana duniani, lakini kwa hapa Tanzania lolote linaweza kutokea bora mradi uwe na pesa tu, huwa nabaki najiuliza kwamba kizazi kijacho, mfano mwanangu mimi , watarithi ama kujivunia nini na utajiri wa nchi hii, sababu kila kitu kinachukuliwa na kwenda nje, madini, haya tena mara tunasikia Mbuga za wanyama zinauzwa kwa Waarabu na kugeuzwa ranchi, na mkae mkijua kwamba hawa waarabu wenyewe ni watu wabaguzi sana, Je kuna mtanzania hata mmoja ambaye anaweza kuwekeza katika sekta muhimu kama hiyo kwenye nchi zao? hata wakija na kuwekeza hapa hakuna wanalofanya zaidi ya kuua ndugu zetu, halafu serikali ya Kikwete inachekelea tu, Leo hii muirak ama Msukuma akikamatwa kwenye Mbuga akiwinda lazima akione cha moto na wakati ni maskini na ile ni mali yake. Inauma sana lakini hakuna jinsi.
   

  Attached Files:

 9. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Nakubalina na wewe kuwa watu wanaweza kubeba other trophies na si mnyama mkubwa kama twiga akiwa hai. Smugling ipo siku zote...............
   
 10. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Wacheni kumsakama Gama anavyosema ni kweli. Kwani kibali chenyewe ni shida? Thamani ya kibali cha CITES ni dola kumi, cha zoosanitary vile vile ni chini ya dola kumi, sasa kama umepata clearance kutoka huko unakompeleka shida yake ni nini? Ikiwa mwenye twiga anaweza kumsafirisha kwa gharama kubwa atashindwa kulipia hivyo vibali?

  Twiga mkubwa hawezi kusafirishwa bila ya vibali kwani hata ndege haikubali kubeba mnyama wa aina hiyo bila ya vibali vyake maalumu. Kwa hivyo twiga hawakuibiwa lakini wamepitishwa kwa ruhusa maalumu.
   
 11. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Baelezee baelewe, mashirika ya ndege makubwa kama KLM, Gulf, egypt na turkey crew wake wanajua procedures, huwezi kupakia mnyama hai bila genuine CiTES wakakupokea kwani kulingana na "internatinal convention on trading on endengered sppp" ndege inayobeba wildlife hai ambaye hana CITES inapaswa kumrudisha alikotoka, ndo maana katika mchango wangu wa kwanza nilisema twiga hawezi kuibiwa bali ukiona hivyo ujue ni muingiliano wa soko huria na coruption, wale wanaobisha kwa jazba hawawezi kunielewa kwasababu wana mawazo mgando, kuna mwingine ametoa mfano kuwa nyara zinasafirishwa kutoka mikoani kuletwa dar na magari ya serikali: jibu langu ni kuwa hii hoja na sahihi. Kwa nyongeza tu ni kuwa hata crossborder smugling ya trophies hufanywa na diplomats kwani hawa mizigo yao haikaguliwi.
   
 12. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hapo ndugu yangu kwenye blue/bold unakosea sana kusema hivyo, usifikirie bei ya nyama yake, fikiria watalii huja na kulipa pesa nyingi sana na kuwaangalia na kuwaacha wakiwa hai, hakuna mtalii aliyewahi kuja kuangalia ng'ombe au mbuzi ambazo kwa mtazamo wako bei ya nyama yake ipo juu kuliko nyama pori,
   
 13. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Acha maneno yako wewe!!! Hii imetokea tangu mwaka jana mwezi wa 11 na kesi ipo mahakamani kwa kuhoji watu wa aina tofauti kufuatana na shughulizao kule KIa
   
 14. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Hujaelewa hoja yangu, am sory typing error pia imeku-misread. Nazungumzia kiasi cha pesa cha kulipia mnyama hai ili umuchukue ni kidogo ukilinganisha na ng'ombe hai, na pia vibali vya kuchukua wanyama vinapatikana isipokuwa ni vigumu kusafirisha mnyama hai kupita kwenye viwanja vya ndege bila kibali (CITES) mara nyingine hata mashirika ya ndege hujiridhisha kuwa unakibali kwani kigundulika huko mbele ya safari ndege ilibeba mnyama huwajibika kumrudisha huyo nyama, nfano kuna ndege moja (mwakajana) kule marekani ambayo ikiwa hewani crew waligundua kuwa abiria mmoja (mtoto mdogo) alikuwa amebeba turttle mdogo, ndege iligeuza hewani kumrudisha yule turttle alikotokea. Nasisitiza kuwa unaweza kumuiba mnyama kutoka tz kwenda kenya kwa kumswaga lakini huwezi kumsafirisha crossborder kwa public transport kwani hata ukiacha maridhiano ya CITES lakini pia ni juhudi za kuzuia kusambaza magonjwa.
   
 15. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  powa nimekupata, good day
   
Loading...