Twendeni Watanzania tukapigie kura mlima Kilimanjaro na hifadhi yetu ya Serengeti

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
TWENDENI WATANZANIA TUKAPIGIE KURA MLIMA KILIMANJARO NA HIFADHI YETU YA SERENGETI.

Kwa mara nyingine tena Mlima wetu adhimu kabisa wa Kilimanjaro na Hifadhi yetu ya Taifa ya Serengeti imechaguliwa kuwania tuzo za Utalii duniani (World Travel Awards 2021) ambapo Mlima Kilimanjaro umechaguliwa kuwania tuzo ya Kivutio Bora zaidi Afrika (Africa's Leading Tourist Attraction) na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo imechaguliwa kuwania tuzo ya Hifadhi Bora zaidi Africa (African's Leading National Park).

JINSI YA KUPIGA KURA.

Fungua tovuti ya www.worldtravelawards.com/vote kisha jisajili halafu chagua bara la Afrika kisha chagua vipengele vya Africa ambapo kipengele cha Hifadhi bora zaidi Afrika (African's Leading National Park 2021) chagua Serengeti National Park, Tanzania na Kipengele cha Kivutio Bora zaidi Afrika ( African's Leading Tourist Attraction 2021) chagua Mount Kilimanjaro, Tanzania.

Mwisho wa kupiga kura ni Septemba 01, 2021.

#Watanzania twende tukaionyeshe dunia uzuri wa nchi yetu Tanzania kwa kupigia kura vivutio vyetu katika tuzo hizo za dunia.

Bwanku M Bwanku
 

Attachments

  • VID-20210814-WA0013.mp4
    26.4 MB
Kura sipigi hata muda wangu siupotezi kwenda huko.

Hii nchi ilikofika sioni umuhimu wa kuendelea kuipenda wala kuwa mzalendo

acha hao wachache walioko kwenye mnyororo wa keki ya taifa waendelee kufurahia nchi.
Unasubiri nini kuamia Afghanistan, wabongo kwa viherehere hatujambo.

Hapo ata ukiambiwa uandamane km 2 tu hutakubali
 
Kitakacho tangaza Mlima Kilimanjaro na hifadhi ya Serengeti ni demokrasia,uhuru wa watu pamoja na utawala bora.

Nchi ambayo Serekali imeitangazia dunia kuwa ina gaidi hatari sana(yaani Freeman Mbowe)itawezaje kuvutia wawekezaji pamoja na watalii?

Tuweke taasisi na mifumo yetu sawa kwanza ndipo Dunia itatuamini.

Umeelewa Bwana mleta uzi?
 
Kura sipigi hata muda wangu siupotezi kwenda huko.

Hii nchi ilikofika sioni umuhimu wa kuendelea kuipenda wala kuwa mzalendo

acha hao wachache walioko kwenye mnyororo wa keki ya taifa waendelee kufurahia nchi.
Mkuu Nenda somalia,ikiwezekana Mimi nitakupa nauli kabisa

Shubamiti!!
 
Si bora hizo kura tumpigie Hamza ili sanamu yake iwekwe kwenye kilele cha Kilimanjaro?

Au nasema uongo ndugu zangu
 
Back
Top Bottom